Kwanini wanyamapori wauzwe nje ya nchi? Hii biashara ina mashiko gani kwenye ulimwengu ulistaarabika?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,346
45,694
Biashara ya kuuza wanyamapori nje ya nchi ina faida gani yoyote ya maana kwa nchi?
Ni mapato kiasi gani yanayoweza kuhalalisha biashara ya aina hii.

Hawa wanyama nature imewafanya wawe hapa kwenye nchi hii. Huwa wanapungua au kuongezeka kwa kuliwa na wenzao, kufa au kuhama ecosystem huwa ina balance mambo hivyo lakini zaidi kuna uwindaji halali(barbaric lakini sheria inaruhusu), pia kuna ujangili ambao umeendelea kupunguza idadi yao miaka kwa miaka.

Katika hali kama hii kwa nini serikali iongezee kufanya biashara ya kuuza hawa wanyamapori nje waende kufungiwa kwenye zoo? Kuna kitu hakiko sawa kwenye akili za wanadamu kuhusu uelewa na kujali wanyama na mazingira kwa faida ya wote.

Nimemsikiliza waziri wa maliasili leo akitengeua taarifa iliyosambaa sana mtandaoni ya serikali kuruhusu TENA wanyamapori kuuzwa nje ya nchi! Sijaona la kusifia au kushangalia kwa sababu biashara yote ya kuuza wanyamapori nje ya nchi naona ingepesawa kuwa haramu kabisa kama vile ilivyo human trafficking.

Sheria ya bunge ya kuweka marufuku ya kudumu kuuza wanyamapori nje ya nchi inahitajika.
 
Upigaji tu. Watakuja kukuambia kwamba hii biashara ilikuwepo tangu enzi za Nyerere
 
Back
Top Bottom