Kwanini wanawake wengi wazuri huishia mikononi mwa wanaume wasio wazuri kisura

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,407
2,000
Nimekuwa kwenye mtandao wa Facebook yapata takribani wiki 7 sasa tangu nijiunge.

Hivi majuzi nilijikuta inbox nachati na msichana kutoka New Zealand. Muonekano wa Chat haukuwa na makusudi ambayo unayoweza kuyafikiria hivi sasa.
Binafsi nilipenda jinsi tulivyokuwa tuna zungumzia kupitia chat.

Hivyo nikajikuta nikipendekeza anipe namba zake tuwasiliane What'sApp kirahisi.
Ghafla akadhani kuwa nataka kumtokea.
Akaamua kutuma picha akiwa ameambatanisha na ile ya mpenzi wake.Licha ya kuwa sikuwa na lengo lolote la kuanzisha mahusiano ya kimapenzi nikashangaa kuona Msichana mzuri kama yeye inakuwaje anamahusiano na mshkaji wa jinsi ile.
Sikutaka kuamini kirahisi, ila baada ya kuchimba kwa kina nikajidhibitishia bila chembe ya shaka kuwa, naam' yule ni Bwana 'ake.

Msichana huyu hapa:-


Jamaa yake huyu hapa:-


Nikaenda kwenye section ambayo anapost picha zake. Ni kweli nimekuta picha ya huyu Jamaa akiwa ameipost na kumsifia sana m'shkaji kuwa ndio mpenzi wa maisha yake.

Pia nikapata nafasi ya kufuatilia profile ya huyo M'shkaji wake ili nione kama huyo mshichana huenda labda alivutiwa na pesa za M'shkaji ila haikuwa hivyo.

Baada ya hayo, ilinibidi ni log off ili nipate nafasi ya kuwatafakari wadada walio wengi ambao kila kukicha wanawaza kuwa siku moja watapata kuolewa na Mwanaume 'Handsome'.

FUNDISHO:- (hasa kwako Mwanaume mwenzangu)

'Women Don't Mean What They Say'
 

Pr cure

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
1,862
2,000
unachokikataa wenzako wanakiona ruby, huyo Dada kuna kitu kapenda, ungeendelea kuchat nae ungejua vingi, sema alipokitumia hiyo picha ya Mshkaji, text yako ya mwisho nahsi ilikuwa

"end of conversion"
 

forumyangu

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,150
2,000
Nashanga watu wanambeza mleta mada hii kitu ipo tena sana.Wanawake wengi wazuri hupenda wanaume wabaya kwa sura kwa sababu huwaongezea sifa na kubainisha uzuri wake wakiwa pamoja.Ila kama anakuwa na mwanaume mzuri basi uzuri wake hautaonekana
 

ney kush

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
1,311
2,000
Nashanga watu wanambeza mleta mada hii kitu ipo tena sana.Wanawake wengi wazuri hupenda wanaume wabaya kwa sura kwa sababu huwaongezea sifa na kubainisha uzuri wake wakiwa pamoja.Ila kama anakuwa na mwanaume mzuri basi uzuri wake hautaonekana
INAWEZEKANA NA ISIWEZEKANE PIA.. NI MAWAZO YAKO NA HAYAPASWI KUPINGWA
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,298
2,000
Wanawake wazuri hupenda kujiona 'very special'
hutaka kuwa treated 'very special'
sasa kama na wewe ni very handsome si utakuwa na wadada wengi wanakutaka?
ni rahisi huyo mmoja kumuona wa kawaida tu...ukam treat kawaida..
ndo shida inaanzia hapo

Hao jamaa wa sura za kawaida hujishusha mno na kumfanya huyo dada ajione 'malkia fulani'
ndo maana hunasa huko...

ni kazi tu ambayo hata wewe ukiamua unaweza
ma hadnsome hawana mda huo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom