UTAFITI: Kilimanjaro yaongoza kwa kuwa na Wanawake wanene na wenye viribatumbo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuongoza kwa kuwa na wanawake wanene na wenye viribatumbo nchini, Dar imeshika nafasi ya pili, Mkurugenzi wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania Dk Germana Leyna amesema.

Sababu hasa zinazopelekea matatizo hayo, Ni kutozingatia lishe bora na mazoezi.
 
Huo utafiti unatusaidiaje na sisi tulioko huku. Vipi kuna fursa ya kuwakamua mafuta huko?! Vipi mtafiti kasemaje kuhusu viriba tumbo au serikali inawatafutia soko huko ulaya?!
 
Wale wanajua kutafuta pesa na kutumia pia. Sio magolikipa wale. So sishangai hii taarifa.
Though sio utaratibu mzuri kiafya.
 
Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuongoza kwa kuwa na wanawake wanene na wenye viribatumbo nchini, Dar imeshika nafasi ya pili, Mkurugenzi wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania Dk Germana Leyna amesema
Hii ni kweli,kuthibitisha hilo angalia michango ya watoto wao wanaochangia hapa jukwaani,ni full matusi ,kejeri na dharau,ni kwasababu ya madhara ya viriba tumbo vya wazazi wao
 
Majibu ya Utafiti Dar na kilimanjaro Ndio mikoa inayoongoza kuwa na wanawake wenye vitambi na viribatumbo
Je? Tatizo ni nini life style,ulaji mbovu au hali nzuri zmya kiuchumi
Karibuni tujadili
Take a picha
Capture%2B_2019-08-24-18-20-42.jpeg
 
Sijui umeweza kufanya kautafiti vizuri. Hao hao wa dar wenye tatizo hilo nadhani wametoka Kilim,anjaro. Hivyo nadhani ni vyema ukamalizia kuwa, Kilimanjaro ndo inaongoza
 
Lengo la utafiti huu lilikua ni nini?
Na je unatusaidia katika kuifikia Tanzania ya viwanda?
 
Na ndio mikoa inaongoza kwa ufahamu, utajiri, uelewa, ustaarabu na bata..........

Povu ruksa ila muhimu hasira zingine pelekeni kwa makaburu walioshikilia ndege yetu
 
kila taasisi na majukumu yake. Hii ni upande wa lishe, likija swala la uchumi na viwanda wanaohusika wataleta tafiti zao.
Lengo la utafiti huu lilikua ni nini?
Na je unatusaidia katika kuifikia Tanzania ya viwanda?
 
Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuongoza kwa kuwa na wanawake wanene na wenye viribatumbo nchini, Dar imeshika nafasi ya pili, Mkurugenzi wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania Dk Germana Leyna amesema
UTAFITI HUO HAUNA MAKOSA. UPO SAHIHI.
NA WALE WANAOCHANGIA MADA WAKASEMA NI BIA NA NYAMA PIA NI SAHIHI.
ONGEZA NA DESTURI YA HUKU, KWA WAMAMA WAZAZI, HUWA KUNA UTARATIBU MZURI WA KUWALISHA MITORI NA MAUJI YA MBEGE NA MAZIWA KWA AJILI YA UNYONYESHAJI WENYE UFANISI.

MAFUTA MENGI YA MKIA WA KONDOO KTK NDIZI NG'OMBE PEKECHA!! HUTUMIKA KAMA CHAKULA KIKUU KWA MAMA MZAZI ALIEJIFUNGUA NA NI KWA MUDA WA KUTOSHA.

HAPO KWELI MAMA ATAACHA KUTUTUMKA? TUMBO LITABAKI KAMA MWANZO?? PLUS AKISHAKAA SAWA NA KURUDI KTK BIASHARA ZAKE ANAENDELEA SASA KUTUPIA BIA & MBEGE NDIZI MCHEMSHO, SUPU NK... KAMA KAWAIDA.
(SIO WOTE LAKINI(

NAFIKIRI WATAFITI WAMEPATIA KTK HILO.
 
Back
Top Bottom