Kwanini wanawake wanatunza sana magari?

Wakuu habari za jumapili.
Ndugu hawa jinsia ya KE ni watunzaji sana wa vyombo vya moto kuliko sisi wanaume. Mfano sister yangu alinunua gari toyota ist 2015 ni namba C lakini mpaka sasa imesimama hatari hata hizi namba D mpya hazigusi na Brother mwingine yeye alidaka harrier 2018 lakin kaicheki utaona imeshapoteza upya imechoka choka.

Hawa jinsia ya KE ni watunzaji sana wa magari ni sababu gani inafanya sisi jinsia ya ME magari yetu yanawahi kuchoka na utakuta sometimes mmenunua gari pamoja na siku moja.

Nunua gari model moja na KE siku moja, afu baada ya mwaka mlinganishe utaona gari ya ME imechoka hawa KE wanaendeshaje gari?
ni waoga hawawezi kustahimili mikiki,wakati kufungua tu boneti shida,wengi wao ni kukamata starling tu halafu wanaendesha automatic
 
Siku mwanaume akiendesha gari ya mke wake...

Mume: Gari yako inamuda gani toka ianze kufanya (hapo unakuta miguu inagonga balaa)
Mke : kufanya nini tena?

Ila kwa nionavyo mimi, gari za wanawake ni safi kwa nje tu... Chafu ndani.
Na kuhusu gari kuchoka, kwani we ulishaona mwanamke yupi anajifunza drifting?? Anafuta kisahani?? au anaomba chumba?? Kama tu ukaaji wao ndiyo ule wa kutokuegamia seat.
 
Lita-haribikaje au kuchakaa wakati hata pancha tu hafunguwi tairi mpaka amuite mwanamume ambadilishie, akiambiwa ni bovu linavimba atampigia mwanamume (au Noss/ mchepuko) ampe jipya
Petrol yenyewe haweki kwa pesa yake
Safari ya kwenda kwao atajiuliza mara 10, aombe lift au mafuta, mara paap kambeba serengeti amuendeshee mpaka Kijijini kwa lakini ampe akiziona nyumba
Ni lini ulipewa lift na mwanamke hebu kaa barabarani uangalie madereva pembeni yao wanakaa kina nani ndipo uje tuendelee na majibu

Champagnee

Mwanamke akupe lift, si utakesha barabarani? 😂
 
Inategemea lakini mimi nilisafiri nilimuachia gari mtu jinsia ya KE nilikukuta amezidisha karibia 300km plus za kuchange oil
 
Inategemea lakini mimi nilisafiri nilimuachia gari mtu jinsia ya KE nilikukuta amezidisha karibia 300km plus za kuchange oil
Mambo ya oil hawayajuagi ilitakiwa umkabidhi na fundi angeua engine aise. Wengi Wao ni kuwasha na kusepa kukagua sijui maji upepo never.
 
Mambo ya oil hawayajuagi ilitakiwa umkabidhi na fundi angeua engine aise. Wengi Wao ni kuwasha na kusepa kukagua sijui maji upepo never.
Yaan toka siku io namshikishaga ki card cha service kabsa .Ila ndio niliamini gari za Mjapan zinavumilia kwa kwer
 
Kwa nje sawa na usafi wa ndani ila vitu muhimu kama kufanya service ni changamoto kwao ...muonekano unaweza kuwa uko vizuri ila majanga kwenye vitu vya msingi
 
Siku mwanaume akiendesha gari ya mke wake...

Mume: Gari yako inamuda gani toka ianze kufanya (hapo unakuta miguu inagonga balaa)
Mke : kufanya nini tena?

Ila kwa nionavyo mimi, gari za wanawake ni safi kwa nje tu... Chafu ndani.
Na kuhusu gari kuchoka, kwani we ulishaona mwanamke yupi anajifunza drifting?? Anafuta kisahani?? au anaomba chumba?? Kama tu ukaaji wao ndiyo ule wa kutokuegamia seat.
ni kweli gari zao wengi ndani ni chafu. Hivi ni kwanini asilimia kubwa huwa hawaegamii seat?
 
Back
Top Bottom