Kwanini Wanawake wa sasa hawapendi kuanza sifuri kimaisha na Mwanaume

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,621
Sio kwamba wanawake wa sasa hawapendi kuanza na mwanaume from zero to hero.

Sio kweli kwamba wanawake wote wanataka kuwa na wanaume ambao tayari wameshafanikiwa. Wengi wanatamani kuanza na ampendae kuanzia chini mpaka juu ila tatizo liko hapa.

1: Anahofia kuanza sifuri na mwanaume ambae hana mipango ya kutoka kwenye hiyo sifuri.

2: Anahofia kuneng'eneka kutengeneza ngome ambayo taji la umalkia atakuja kutunukiwa mwingine.

Asilimia kubwa ya wanaume huwa wanaficha tabia zao wakiwa hawana kitu, na hubadilika wakijapata kitu. Na mwisho wanasahau aliyevumilia ukame kwa miaka 6, unaenda oa asiejua hata hizo pesa ulipataje.

Wapo ambao wanakuwa na wewe sio sababu anakupenda, no, bali kwasababu anajua hana hela hivyo hawezi kuwapata wale awatakao.

3: Anahofia mchango wake kutothaminika na kuja kuonekana kama hana la maana alilofanya kwako. Sababu wanaume wengi huwa wanasahau hata yale machache waliyosaidiwa na wanawake wao na kutumia mali zao kama kigezo cha kuwabeza na kuwadharau wake zao.

My point is, kama unataka mwanamke akuamini na akubali kuanza na wewe from zero to hero. Basi kuwa wazi juu ya mipango yako juu yake. Unampenda na una malengo nae? Au unataka kula, kula, kula, kula, kula, kula na kusepa?.

Siku zote mwanamke umri haumsubiri, kila anavyozidi kukua ndivyo anavyozidi kupata presha ya kukosa kuolewa. Ipi mipango yako juu yake? Na una uhakika nayo au unamuigizia tu? Anahitaji assurance.

Jifunze kuthamini na kumsifu kwa madogo anayokufanyia. Jifunze kushukuru kwa kila jema analofanya. Hiyo itamfanya aamini yuko na mtu sahihi ambae anaweza kumuamini, kumvumilia na kujenga nae maisha from zero.

Kuwa wazi juu ya plan zako za kimaisha. Unataka kutoboa kimaisha kwa kupitia njia gani? Unataka kufanya nini na nini? Biashara au kazi? Unataka kuanza kujenga au kununua gari?

Kumshirikisha itamfanya aamini kuwa unathamini uwepo wake katika maisha yako.

Hali hii itamfanya akuamini, kukushauri, kukuombea, na hata kukusupport.

Huwa wanakerekwa na ile hali ya kutopenda kumshirikisha ilihali siku ukiishiwa, unataka akusupport. Hili jambo huwafanya wajihisi kama huthamini uwepo wake kwako.

"Kwa MVULANA, mwanamke mwenye akili huwa ni tishio kwake. Ila kwa MWANAUME, mwanamke mwenye akili huwa ni rafiki, mshauri, msaidizi, na mpenzi wa maisha yake.".
 
Oohh......ila kwa kwelii na wanaume Sasa tumeamua.....hatutaki mwanamke alie kwenye zero kwa kwelii.......Yani nimkute kwenye zero nimtengeneze nimpe maisha afu ye aende kutunuku kitumbua kwa wengine!!!!....hapana.....mwanamke alie kwenye zero abaki tu kwao.
 
Yamekukuta wew,....hebu simulia uutue huo mzigo shingoni

Mwenyezi Mungu ametujaalia kusamehe ila kusahau ndo huwa ngumu. Ila inaumiza sana pale mtu anakua na wewe kwasababu ya kitu. Let it be inkind ama materially. Let it be mwanamke ama.mwanaume. ni dhambi jamani. Tumwogope Mungu. Ubaya ni kwamba wanawake tuna huruma sana. Huwa tunaaminigi atabadilika huyu. Siku akipata jaman
Kuwekeza upendo, muda na support za hapa na pape kisha mtu akipata jamani looh. Ndo life lkn
 
Dooh umeongea kwa uzuni mpaka nimefeel hiyo uzuni aisee .....pole Sanaa Dada mzuri
 
Back
Top Bottom