Kwanini wanaume wengine wanaogopa kuoa

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali
ya kawaida kabisa,
kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo
haya:

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo
mtarajiwa ukajitambulishe huko.
Kama
mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi
Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia
shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo
atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa
umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio
kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na
gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane
Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha
ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda
Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna
imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye
hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe
2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida
kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita
marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko
wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa
500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu
kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya
kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!

11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!

12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..."
700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za
harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000
maana utalia lia
sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili
watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la
bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000
uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi
watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila
utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa
uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji
kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar
ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa
wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black
kibishi 40,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana
akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so
utalipa malazi ya siku mbili 200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini
ya 800,000 kwa angalau siku 5.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote
iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za
nani?? 500,000!
 
!
!
Mie hayo yooote hayanipi tabu....tabu ni kwamba kuoa ni sawa na kujumlisha hasi au kuchukua gunia la njaa kuliweka ndani
 
Tunakoenda, Bila kukopa saccoss, ndoa mtazisikia kwenye bomba.

Gharama zimekuwa kubwa sana, lakini sio gharama za msingi. mbwembwe nyingi sana kwa kweli.

Hivi ukiwa na jamaa zenu kama 20 to 50 baada ya ibada ukaenda hotel ya maana mkala dinner then ikaishia hapo mtadhurika chochote? nafikiri tunapaswa kuleta mapinduzi nako huku, tunakoelekea ni kubaya (show off)
 
Ukiwaza gharama huwezi kuoa; wengine baada ya mapenzi kutuzidia tulipanga wenyewe kuoana na kukwepa gharama zingine.
 
Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali
ya kawaida kabisa,
kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo
haya:

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo
mtarajiwa ukajitambulishe huko.
Kama
mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi
Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia
shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo
atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa
umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio
kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na
gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane
Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha
ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda
Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna
imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye
hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe
2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida
kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita
marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko
wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa
500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu
kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya
kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!

11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!

12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..."
700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za
harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000
maana utalia lia
sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili
watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la
bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000
uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi
watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila
utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa
uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji
kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar
ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa
wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black
kibishi 40,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana
akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so
utalipa malazi ya siku mbili 200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini
ya 800,000 kwa angalau siku 5.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote
iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za
nani?? 500,000!

...duh! kwa gharama hizi! "ukichapiwa' lazima iwe siri ya ndani...!"
 
Hayo yalinitokea kipindi ndio nimetoka chuo tu wakati huo nafanya kazi Standard Chartered Bank mshahara wao ulikuwa wa ubabaishaji.Mshahara mzuri ulikuwa unatolewa kwa kujuana, unaweza ukawa una degree unalipwa sawa na form four.Basi si na mimi nilikuwa na mchumba akanishawishi niende kujitambulisha kwao basi nikapata mambo kama hayo ya kutembelea wandugu halafu wakataka harusi babu kubwa.Mimi nilichofanya nikuwakubalia tu ili wakubali kupokea mahari zangu kwanza.Basi baada ya kupokea nikamwambia mchumba wangu kwamba mambo wanayohitaji wazazi ya kutembeleana na harusi kubwa yatafanyika baada ya mwaka mmoja na nusu.

Mke wangu kwa kuhofia mabinti wa benki kumpindua basi akafanya maamuzi magumu ambayo hata mimi yalinishangaza akahamia kwangu moja kwa moja tukaenda kufunga ndoa bomani.

Ukipata binti anayejitambua na wewe ukawa unajitambua mambo yanakua simple.Ndani ya mwaka mmoja tukawa tayari tumeishajenga nyumba yetu muda huo wengine wanakomaa na harusi mimi niko kwangu kwenye nyumba yangu nakula good time.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom