Kwanini wanaume wengi wanaogopa kuoa?

Kibenje KK

JF-Expert Member
May 28, 2016
267
380
Wanawake hivi Mnajua sababu kwanini Wanaume wengi sikuhizi Hawaoi?

Nimekua nikiona makanisani Wanawake wanavyoenda mbele kuombewa ili wapate ndoa, Mchungaji akisema POKEA NDOA? utasikia Napokeaaaaaa lakini ndo kwanza wanaume wanaogopa. Sio kuwa wanaume hawataki kuoa ila kuna hizi sababu. 👇

1. Mwanaume Anapenda Mwanamke anayejiheshimu. Hakuna mwanaume anavutiwa na mwanamke mwenye maneno, utani kupitiliza, nguo zinazomuonyesha na kuchonga mwili wake.

2. Mwanaume Anapenda Mwanamke ambaye ni Mvumilivu. Si kila siku mambo yanaenda vizuri. Ukipata Mvumilivu kwanini usioe?

3. Mwanaume Anapenda Mwanamke anayejari na Kuthamini

4. Mwanaume Anapenda Mwanamke Mwenye Mawazo Chanya (Future Vision). Kuna mahali naweza kushindwa. Nisaidie.

5. Mwanaume anapenda Kutodharauliwa. Enyi wanawake waheshimu waume zenu.

6. Mwanaume Anapenda Maamuzi yake yaheshimiwe. Unaweza kumshauri lakini heshimu maamuzi yake.

7. Mwanaume Anapenda Mwanamke anaye Rizika.

8. Mwanaume ni kichwa, anapenda kuwa juu. Mpe nafasi yake.

9. Mwanaume anapenda Kusikilizwa

10. Mwanaume yoyote hapendi Mwanamke anayejiona na anayejiskia. Kha! I kuna wanawake wanajiona wa gharama sana. Unapaswa kujipa thamani ila usijisikie.

Mwanamke Bora ni Yule anayejua Thamani ya Mwanaume na si yule anayejua Kipato cha Mwanaume.
#kelvinkibenje
 
Wwww hvy hvy vyenye vibeg mgongon viwe na sifa hiz mamaang sidhan vijeur kwanz vinajiona vzr Sasa kwa mfumo huu tutafika kwel hakuna kuoaaaa tuwaache wajioeee
 
Mnaogopa kuoa au mnaogopa wanawake wenye tabia mbaya!

Hakuna utapata perfect, hao unaosema wawe na sifa hizo maana ake hayo mapungufu unayoyataja ndo wanaume hawataki kusikia au kuona.

Kwa sasa vutiwa nae oa halafu mtajuana ndani ya nyumba huko!

Usilipe mahari kwanza !
 
Wenye misabwada wameisha sasa unataka tuoe nani? Siyo kwamba tunaogopa kuoa ila tunasubiri ma under18 wenye chura wafike umri wa matumizi
 
Back
Top Bottom