• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Kwanini wanaume wengi tuko magerezani/tunafungwa pingu. Kwanini wanawake wengi wapo makanisani wanatafuta nini?

Sigara Kali

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Messages
2,836
Points
2,000
Sigara Kali

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined May 28, 2017
2,836 2,000
Nafanya kazi Karibu na kituo kikuu Cha police na ofisi kuu ya RPC

Kila ikifika Jumatatu napatwa na maumivu sana kwa ninayo yaona

Nawaona wanaume wenzangu wengi sana wamefungwa mashati,pingu ,wameshikwa tanganyika jeki wanapelekwa mahakamani

Nakaa nawaza sana kwa nini kila siku ni sie tu

Nimekaa hayo maeneo karibu na central kwa muda mrefu Ila sijawahi kuona mwanamke yoyote anatendewa vile

Je sisi wanaume ndo wenye makosa pekee hapa duniani hadi ifikie hatua ya kudhalilishwa na kuonekana hatuna utu wala thamani mbele ya jamii?

Nimetupwa selo za vituo kadhaa vya police hapa Tanzania kule nimekuta idadi kubwa ni wanaume wenzangu tunateseka usiku kucha.

Selo ya Wanawake wapo wachache tena wale wauza papuchi tu

Nikienda makanisani wengi ni wanawake kuliko wanaume je tatizo liko wapi? Hapa

Misikitini nashindwa kusema kwa sababu wanaume na Wanawake hatuchangamani

Sasa tuje huku upande wa pili inakuaje wenzetu wajae Makanisani halafu sie wanaume tujae selo za police na magereza mbalimbali.

Tujadili hapa Wananzengo wanaume tuna matatizo gani hadi wengi tuishie jela na wanawake wana matatizo gani hadi wengi waende Makanisani?
 
Suriya

Suriya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Messages
4,810
Points
2,000
Suriya

Suriya

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2015
4,810 2,000
Kasome biblia yako.

Hata dhambi haikuingia duniani kupitia mwanamke, alipokula tunda na Adamu ndipo wakagundua kuwa wapo uchi.
1 Wakorintho 11:3
[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

Shetani hushambulia mwanaume akijua na mwanamke atamkamata pia.
Lakin pia wanawake ni wepesi wa kuamini japo kuamin kwao kwa urahis kunawafanya pia na kudanganyw kirahis, lakin wasichana ni wepesi wa kuwa na Iman katika Mungu.

Wanaume tumekua wabishi sana but na sisi tukishika Imani tunashika kweli kweli na kuyumbishwa inakua ngumu tena, kwahiyo shetan hututafuta mapema..

LADIES PRAY FOR YOUR HUSBAND.
 
BUSH BIN LADEN

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Messages
754
Points
1,000
BUSH BIN LADEN

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2019
754 1,000
Tutakula kwa jasho wao watazaa kwa uchungu. Chakula kinapatikana nje wakati mimba inapatikana ndani. Nje ndo mikiki mikiki na mabalaa yaliko so katika kutafuta chakula ndo sometimes haya yanakukuta
 
Castle_Lite

Castle_Lite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Messages
461
Points
1,000
Castle_Lite

Castle_Lite

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2016
461 1,000
Nadhan iko Deep zaidi ya jinsi Mungu alivyoumba roho zetu wanawake/wanaume.

Wanaume wana ujasiri zaid ya wanawake, na ujasiri mwing hupelekea kufanya vitu visivyo sahihi.

Wanawake ni opposite na sisi.

Japo kuna baadhi wana roho ngumu kama Wanaume, na nadhan kwasababu wamerithi hizo roho toka kwa baba zao.
Maana mtu akifanana na Mzazi mmoja wapo arithi sura tu, atarithi had vitu vya ndani.

Iko zaid ya jinsi Muumba wetu alivyo tuumba.
 
Cesar michael

Cesar michael

Member
Joined
Jan 18, 2019
Messages
35
Points
125
Cesar michael

Cesar michael

Member
Joined Jan 18, 2019
35 125
Nafanya kazi Karibu na kituo kikuu Cha police na ofisi kuu ya RPC

Kila ikifika Jumatatu napatwa na maumivu sana kwa ninayo yaona

Nawaona wanaume wenzangu wengi sana wamefungwa mashati,pingu ,wameshikwa tanganyika jeki wanapelekwa mahakamani

Nakaa nawaza sana kwa nini kila siku ni sie tu

Nimekaa hayo maeneo karibu na central kwa muda mrefu Ila sijawahi kuona mwanamke yoyote anatendewa vile

Je sisi wanaume ndo wenye makosa pekee hapa duniani hadi ifikie hatua ya kudhalilishwa na kuonekana hatuna utu wala thamani mbele ya jamii?

Nimetupwa selo za vituo kadhaa vya police hapa Tanzania kule nimekuta idadi kubwa ni wanaume wenzangu tunateseka usiku kucha.

Selo ya Wanawake wapo wachache tena wale wauza papuchi tu

Nikienda makanisani wengi ni wanawake kuliko wanaume je tatizo liko wapi? Hapa

Misikitini nashindwa kusema kwa sababu wanaume na Wanawake hatuchangamani

Sasa tuje huku upande wa pili inakuaje wenzetu wajae Makanisani halafu sie wanaume tujae selo za police na magereza mbalimbali.

Tujadili hapa Wananzengo wanaume tuna matatizo gani hadi wengi tuishie jela na wanawake wana matatizo gani hadi wengi waende Makanisani?
Mi nadhani swala la mfumo dume ndilo hupelekea wanaume kukumbana na kash kash nyingi kutokana na kuelemewa na majukumu mengi na ndio maana ukiangalia ata waathirika wa dawa za kulevya asilimia kubwa ni wanaume, jela wanaume ndio wengi, vibaka mtaani n.k hivyo basi ile hali ya mwanaume kutingwa na majukumu yaliyoelemea upande mmoja yanaweza sababisha akafanya makosa kinyume na sheria na kuishia maeneo kama hayo

Lakini swala la wanawake kuwa wengi kanisani li atokana na wanawake kuwa wepesi wa kushawishika na kuamini zaidi linapokuja swala la kiimani na ndio maana utakuta manabii wa kizazi hiki wanawateka wakina mama na watoto kisha kupitia wakina mama kuwa mabalozi wazuri watawashawishi waume zao na mwisho wa siku ibada itahudhuriwa na familia nzima japo bado idadi inakuwa wanawake ndio wengi zaidi makanisani
 
Forum statistics

Threads 1,405,596
Members 532,052
Posts 34,490,138
Top