Kwanini wanaume wengi huwaogopa wanawake wenye sifa hizi?

1. Wasomi
2. Wenye uchumi mkubwa
3. Warembo kupitiliza
4. Walio wazidi umri (mwanamke mkubwa zaidi ya umri wa mwanaume)

Wenye sifa hizo hawabebeki labda utumie mbeleko ya mawingu au turubai
 
Effects zao zimeonekana! Hasa zile -ve, anataka na yeye awe kichwa,badala ya msaidiz kama maandik yanavysema.. Sasa sidhan kama Mwanaume anawez kuvumilia hayo.
 
Mmmh I can imagine jinsi gani unampeleka jamaa yako mchakamchaka. Maana ushasema tayari kwamba unasifa zote zilizotajwa hapo juu, na wanawake wengi hulewa sifa na kuanza command kwa mwanaume wake.

hata mi nilikuwa suelewi kwanini naogopwa sana, kumbe sababu ni hizo sifa zangu ulizozitaja hapo juu.<br />
Lakini kwanini tuogopwe na midume?
<br />
<br />
 
Nadhani ni mwelekeo wa hapa tanzania tu.. Kwingine ni tofauti kabisa..

Ila kuna shida na issue ya tatu ya uzuri.. Mwanamke akiwa mzuri sana huwa inawafanya kujisikia sana na kuwa na dharau..
Kwangu suala la umri sidhani kama ni shida..
Elimu siyo tatizo sana kama mnapendana ukweli na kuheshimiana.
 
Tumia vizuri mche uliopewa na Mungu,mwanamke ni mwanamke tu hata akiwa na nini hawezi kumbebesha mimba mwanaume,mpe dozi nene uone kama hatakueshimu ukiwa goi goi lazim akudharau.
 
1. Wasomi
2. Wenye uchumi mkubwa
3. Warembo kupitiliza
4. Walio wazidi umri (mwanamke mkubwa zaidi ya umri wa mwanaume)
napenda wanawake warembo sana, wenye uchumi mkubwa, wasomi na tuliosawa umri... Sipendi vitoto
 
Nadhani issue ya kutojiamini kwa wanaume wengi tumeshaizungumzia sana na watu wanaielewa. Labda tu sasa tuangalie kwa nini tusiwe tunajiamini? kuto kujiamini hakutokei hivihivi tu kama hakuna external influence..................... unaangalia jamii inasemaje juu ya kuoa wanawake wa aina flani (Ingekuwa ni jamii inayoencouradge sio ajabu sie tusio wasomi, masikini na wenye sura za kawaida tukabakia kunasaga lami mitaani kwa kukosa waume!!) but kwa kuwa jamii tuliyonayo ni ile ya nyumba iongozwe na mume KWA KILA KITU basi ni wazi watategemea mwanaume abebe jukumu lote la kutunza familia na ikijulikana kuwa mkewe msomi na ana kipato basi tayari mwanaume wake anavuliwa uanaume.


Lakini la pili ni kuwa hii kutojiamini kunatokana pia na matukio yatuzungukayo yanayosupport hii hoja. Kuna alosema kuwa wanawake wa aina hii huwa na dharau na majivuni. Ni kweli, wengi wao wako hivyo na hii ni kwa sababu wanajua kuwa wigo wao wa soko ni mpana kuliko Mwj1 maana na umasikini huu, jisura hili nikimpata mfadhili akanisetiri kimapenzi naanzia wapi kumletea nyodo? akiniacha ntampata wapi mwingine wakati hata dada hujambo barabarani siipati sembuse wa kunitamkia ndoa??

Lakini mkumbuke kuwa sio wanawake wote wenye sifa kama hizo hawafai, mkiamini hivi mtakuwa mnajidhulumu nafsi zenu. Kuna factors nyingine ambazo zinachangia tabia ya mtu mfano hulka, malezi na hata treatments mnazowatreat hawa viumbe jamani!!

Nafikiri kuna haja ya kufanya tafiti juu ya hili ili tuwe na evidence-based information kwa kweli maana sasa tukiisha sie wabaya kina kaka mtaoa kweli? Maana na siku hizi kila azaliwaye ni mzuri sijui Muumba wao anatumia matechnolojia ya kisasa kuwadesign!!! mwe!
 
Tumia vizuri mche uliopewa na Mungu,mwanamke ni mwanamke tu hata akiwa na nini hawezi kumbebesha mimba mwanaume,mpe dozi nene uone kama hatakueshimu ukiwa goi goi lazim akudharau.

Hahahah makubwa..na siku hizi mpaka mche huo ufike kwa muhusika ushafua nguo nyiiingi na kuchoka loh...............
 
Back
Top Bottom