Kwanini wanaume 'waliorogwa' na 'kurogeka' vizuri na wake zao huwa wanakuwa 'Wabishi' ukitaka kuwasaidia na wakiona unawafuatilia wanaweza kukudhuru?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,418
108,517
Inasikitisha kweli kweli yaani Mwanaume analala Saa 7 Usiku na Kuamka Saa 9 Usiku ili aanze Kujiandaa na kuitafuta Vingunguti Machinjioni halafu bado kila akipata tu Mshahara wake anaupeleka wote kwa Mkewe na anapangiwa Bajeti ya Pesa yake anayotakiwa kuwa nayo Mfukoni mwake ama kwa Siku au kwa Wiki.

Mwanaume kwa mwaka mzima Ndugu zake wakija Kumtembelea na Kulala Kwake basi ni mara moja tu na wakichelewa Kuondoka anawahi Kuwakatia Tiketi zao waondoke. Lakini Ndugu za Mwanamke Ukoo mzima unaweza ukafululiza kuja Kwake na hata ukitaka wakitaka Kuondoka utaona Mwanaume anawapigia Magoti waendelee Kubakia hapo Kwake.

Inatia Huruma kweli kweli Mwanaume unateseka Kumtafutia Ugali Mkeo halafu bado tu ukirudi Nyumbani anakufokea kama Mtoto Mdogo na hata Siku ikitokea tu umeiba Hela kwa Bosi wako na ukamnunulia Zawadi ukimpelekea na kudhani ataifurahia na Kukushukuru akiipokea na kama hakuipenda atakuuliza Kidharau kuwa hii Zawadi umeokota au umepewa Msaada tu na Mtu?

Yaani pamoja na Matukio yote haya ya Kusikitisha bado ukitaka Kuliokoa 'Lijitu' linakuwa 'Libishi' na hata Kukutishia 'Kukupiga/Kukudhuru' kabisa.
 
Uneandika majibu kwenye "problem statement".....ni kwa sababu "wamerogwa na wamerogeka"
 
Hakuna cha kurogwa wala nini.

Uchawi ni mambo ya kufikirika tu.

Kwenye uhalisia hayapo.

Labda mwenzetu husomi vitabu hasa vya dini au unasoma Ila huelewi uchawi upo enzi na enzi na unaweza kulogwa ukatafuta tiba ukakosa kikubwa ni kuamini Mungu
 
mungu ni mwema atanilinda, wachawi hua wajanja sana wanapokua na wanajamii wakawaida huigiza hawaamin uchawi ili wapate kudadisi watu wakawaida wanaijuaje hiyo tasnia, inshort hawa watu wanajua igiza kama maafisa wa usalama.

We haya umeyajuaje mkuu
 
Mkuu nadhani wakati mwingine watu kama hao ni kuwaacha waishi maisha waliyoyachagua, na wake zao waliowachagua na wewe kushika hamsini zako. Huyo anaepelekeshwa na mke wake kama yeye haoni tatizo, basi unapoingilia hapo wewe ndio unakua tatizo.
 
Sasa kama umegundua 'wameogwa' na 'kurogeka', kwa nini usiondoe ulozi, halafu ukawashauri, na kuwaonesha walivyorogwa, kurogeka, na ulivyoondoa ulozi ili wajifunze na kukuelewa?
 
Aliyesema kurogwa ni mambo ya kufikiria na hayana uhalisia basi Mungu ni mambo ya kufikia kwa kuwa hakuna uhalisia. Ushauri : unavyoamini katika Mungu ni hivyohivyo katika uchawi
 
Wanaume wa hivyo,akili hua zinawarudia pale wanapoachwa na hao wake zao,hapo ndipo huanza kujuta mali na muda alioupoteza,

Ndoa ni ushirikiano wa Mume na Mke na sio mmoja kumnyoya mwingine.,
Ndoa ni kujiweka sawa,sio mmoja ajione yeye ni bora kuliko mwenzake,

Mke wa hivyo hafai,ni wakumuogopa,muda haumsubiri mtu,majuto huja baadae ila unakua umeshachelewa tena na kupoteza muda wako mwingi na nguvu zako.
 
Dah mkuu umenitia uchungu hasa,mm ni mhanga wa hili suala.
Mkuu,jitoe utumwani kabla hujachelewa,kwanini uishi jela? hiyo ni jela,kama hataki kubadilika tupa kule,Maisha ni mafupi sana,kwanini uishi kwa kuteseka? Wake up and live.
 
Tatizo ulianza wewe kumloga asiondoke. Yeye naye anakuroga usiondoke. Unamlaumu yeye na umeanza wewe.
 
Inasikitisha kweli kweli yaani Mwanaume analala Saa 7 Usiku na Kuamka Saa 9 Usiku ili aanze Kujiandaa na kuitafuta Vingunguti Machinjioni halafu bado kila akipata tu Mshahara wake anaupeleka wote kwa Mkewe na anapangiwa Bajeti ya Pesa yake anayotakiwa kuwa nayo Mfukoni mwake ama kwa Siku au kwa Wiki.

Mwanaume kwa mwaka mzima Ndugu zake wakija Kumtembelea na Kulala Kwake basi ni mara moja tu na wakichelewa Kuondoka anawahi Kuwakatia Tiketi zao waondoke. Lakini Ndugu za Mwanamke Ukoo mzima unaweza ukafululiza kuja Kwake na hata ukitaka wakitaka Kuondoka utaona Mwanaume anawapigia Magoti waendelee Kubakia hapo Kwake.

Inatia Huruma kweli kweli Mwanaume unateseka Kumtafutia Ugali Mkeo halafu bado tu ukirudi Nyumbani anakufokea kama Mtoto Mdogo na hata Siku ikitokea tu umeiba Hela kwa Bosi wako na ukamnunulia Zawadi ukimpelekea na kudhani ataifurahia na Kukushukuru akiipokea na kama hakuipenda atakuuliza Kidharau kuwa hii Zawadi umeokota au umepewa Msaada tu na Mtu?

Yaani pamoja na Matukio yote haya ya Kusikitisha bado ukitaka Kuliokoa 'Lijitu' linakuwa 'Libishi' na hata Kukutishia 'Kukupiga/Kukudhuru' kabisa.
Hilo sio limerogeka brethren,hilo limependa hadi halioni wala kusikia...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom