Kwanini wanaume waliooa huacha kuwashirikisha wenza wao kwenye vyanzo vyao vya mapato?

Habari Wana jamvi,

Kwa wanaume mliooa naomba kuuliza ni kwanini haumshilikishi mkeo vyanzo vyako vya mapato?? Au ulikua unamshilikisha afu ukaacha why?

Ladies take note
unaweza kumshirikisha tu hamna shida, ila tambua wakati wewe ukipambana ili umudu kuihudumia familia yako nakupata maendeleo ya kiuchumi Yeye anawaza kukumiliki wewe na kila kilicho chako.
 
nashukuru Mungu sijabahatisha mwanamke wa Dizaini hiyo ndugu zangu anawapokea vizuri na kuwahudumia ipasavyo hadi niliwahi mchunguza, na nikimpa hela akaitume inatumwa yote hajawai ipunguza, mapungufu yapo tu na ndio yanayo tufanya tuwe na jicho jekundu maana anajua dakika 0 nambadilikia.
😅😅😅😅😅😅 hongera sana mkuu, mkeo kweli amekuwa ndugu yako
 
Kuna jamaa kafa afu uncle kabahatika mjengo wa bure...marehemu alimthamini mtu baki kuliko kumwambia mkewe kuhusu Mali zake.Jumba hilo alikuwa anajenga kisirisiri
Mjomba tu ndio alikuwa anajua?😅 safi ni ndugu yake haina ubaya hio aliojengewa mke inatosha
 
Kwasababu baadhi ya wanawake hawataki wanaume tusaidie familia zetu ila wanataka tuwatngenezee upande wa kwao akijua kipato chako anakipangia bajeti na lazma iwe ugomvi lakin pia likitokea tatzo fadhila zao kwetu ni kutudharau kudai talaka na kwenda mahakamani kudai kugawana mali ili kuhakikisha anakukomoa kabsa Sasa akijua vichochoro vyako vyote atakumaliza kirahisi anatakiwa asijue akiba wala unaingiza shingap ili angalau siku akianza uadui asikumalize ili aendelee na maisha yake kwa amani na wewe uendelee na maisha yako
Hahahahah umeongea kweli kabisa maana tukumbuke mapenzi huwa yanaisha na urafiki unakufa ila undugu haufagi!

Mke unayempenda na kumkabidhi michongo yako yote ni rahisi sana kuja kukumaliza yani maana akilianzisha huko dawati lazma atakuminya kende tu😅 yani atahakikisha amekomba kila ulichonacho una lodge zako mgawane, una hoteli napo ale share, una malori sijui coaster yani vyanzo vyote lazma ahakikishe kakukomesha.

Wanawake ni kuishi nao kwa akili na miongoni mwa vitu ambavyo ni vya kuwa navyo makini ni jasho lako na vyanzo vya pesa. Usije ukaishia kufa kwa stress! Limit michongo yako hata siku akianza vurugu mnaachana kiroho safi!

Kuna yale mapumbavu yanafunguaga joint account kabisa na wake zao😅 yani ushee pool ya pesa na mkeo? Upuuzi wa kiwango cha lami! Kujitaftia mabalaa tu.
 
Shida kama anakuhudumia ipasavyo wewe hayo hayakuhusu mwache na hela zake

Kikubwa malengo au mipango mikakati ya maisha yenu lazima uyajue haya kama huyajui mume anaamka anaamua tu anafanya nn anaenda site mwenyewe hakushirikishi hili ndio tatizo na sio kipato chake.
Kuna kitu umekigusa hapo, Mimi mara nyingi huwaga napishana kauli na mke wangu kwa suala kama Hilo... Siku hizi ananiuliza eti pesa hazioni naficha kwenye gari... Sasa na Mimi namuuliza swali niambie ni siku gani umelala na njaa, na siku gani ndani sijakupa akiba na Hela yako ya matumizi binafsi? Anakosa jibu maana hakuna hata siku moja ambayo kakosa anachikitaka kwa matumizi ya mwezi mzima. Ila ndo hivo hamridhiki mpaka muoneshwe pesa mkononi.
 
Kama unamshahara wa sh mill. 1.5 akikuuliza unalipwa sh ngapi mwambie sh mil 1. hiyo lak 5 ya ziada kila mwez ni ya kuhifadhiwa kwa ajili ya kuanzisha mirad ama ikitokea uhitaji wa fedha wa dharula ama kumnunulia zawadi mara moja moja.
 
NAOMBA NITOE YANGU YA MOYONI NA HII IMENIFIKA MIMI ,NATAKA IWASAIDIE WANAUME AMBAO WANATAKA KUOA.


nina mwaka wa 3 kwenye ndoa na maisha yangu ya ndoa ni ya furaha mke hana tatizo na ana akili ya maisha vzri tu.

Mke wako kujua mshahara wako haina shida kama ana akili ya maisha na akiba.
mimi mke wangu ni mchumi na mbahili kwenye hela kuliko hata mimi,yani naweza nkabaki na laki 2 ya mwisho mfukoni ,wife akijua hilo tunaingia katika state ya POWER MODE/BATTERY SAVER matumizi yanabanwa ili yafike mwisho wa mwezi.


SHIDA IPO HIVII.........

Kwa kuwa mshahara mke wangua anaujua ,kila expenditure ya hela lzma atake kujua yani wakuu nacheka kama mazuri ,

nikitoa 50k nihonge ka manzi ka pembeni ,atahoji ""ile 50k mbona siioni umenunua nini?""
nkienda pata maji matamu/bia nkaspend kama 80k kwa usiku mmoja ,ni ugomvi nyumbani kwamba nafuja hela

CHA KUSHANGAZA WAKUU.

mimi huwa natoa 75% ya mshahara naleta home ili ukae na 25% unabaki benki na mke anajua mgawanyo wa hela ,ila ataenda kuhesabu upya hela nilizoleta tena anaweka na MATE kwenye kidole azihesabu vzri kwa kifupi nisiwachoshe wakuu ni kama CAG / mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za nyumbani.
hata nkisema nilete ukali sa hv tyr kashaujua mshahara nirahisi kunifatilia sana.

NILICHOPANGA KUFANYA

nkipata post na promotion kazini ya nyongeza ya hela hatokuja kuijuaaa kwamweeee ,kamweeeee

kidume hata hela ya kuchepuka sina ,hili kosa la kujifanya HUSBAND MATERIAL SIYO ZURI JMN. MWANAUME NI MWENDO WA JICHO NYANYA TU

Mke ajue 75% ya salary ,Ndugu zako wajue 25% ya mshahar jiroge waambie ndugu unapokea milioni utajua haujui , mchepuko hapaswi kujua mshahara kbsaaa...

ova
 
Wanawake wanapenda control.

Akizijua pesa zako lazima atashika usukani na huwezi zuia sababu papuchi yake ni tamu sana.

Sasa utajikuta tu hata ndugu hutasaidia, rafiki hutakopesha bila kuamuandikia yeye proposal yenye sababu za msingi ni kwann unataka kufanya unalofanya.

Akijiliza liza akakukatikia halafu akaanza kuzipangia matumizi mtajikuta tu nyie ni mwili mmoja.

Afahamu 75% inatosha hii 25% ni kwa ajili yangu na ndugu zangu pengine na kusaidiana na marafiki wakipata tatizo.
Hahahahaha daaah
 
Mwaka juzi nilimshirikisha wife kwenye project moja bahati mbayà nikipata loss ya milioni kadhaa, ilikuwa hatari yaani wife alipiga kelele nikakosa amani, mwaka huu sijamshilikisha na nimepata loss kubwa zaidi ila nipo na furaha tu, na nimepanga sitamshirikisha tena
Mashost wasimcheke unafikiri mchezo lazima akinukishe
 
Sio wote mimi kwa mke wangu anajua kila kitu.hadi nikikosa anajua mana ntakuwa nimenuna siku nzima sina raha.ukiwa na mke anaejua maisha bora kumshirikisha kuliko kujifanya mbinafsi...rejea jamaa alieokota nyumba bunju.!!! Mume anagemshirikisha mkewe nyumba isingepotea baada ya kufa.kawanyima watoto haki yao.

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
Wewe ni mwanaume kamili...si haya mapoyoyo hayajui nafasi ya mwanamke!

Unakuta mwanaume linaishi na mwanamke kama dume mwenzie the way linamtreat...waii
 
Mimi nakumbuka kipindi naanza ajira matumizi binafsi ndani kwa mwezi laki 6 inaisha na hapo tunaishi mbali yeye town mimi bush kwenda mjini mara moja moja, nikajitoa kumfungulia biashara ya kama Milioni 6 hivi duka la nguo akaanza kunambia rafiki zake wanamshangaa kasoma ila anauza duka la nguo miezi 6 baadae biashara ikafa hakuna pesa wala nguo zilizopo kumuuliza eti kakopesha aliowakopa wamekimbia.


Viwalo vikayeya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom