Kwanini wanaume wa Tanzania hufyatuka kwa hasira kali wake zao wakipoteza mapenzi kwao?

Kwanini wanaume wa Tanzania hufyatuka kwa hasira kali wake zao wakipoteza mapenzi kwao?

Sasa mapenzi yameisha si unavunja mahusiano unakua huru kulala na yoyote. Kwanini uchepuke? Unatetea umalaya?
Watanzania wengi kwenye ndoa na nje ya ndoa hawana ujasiri wa kuambiana ukweli huo kwamba mapenzi yameisha kila mtu ashike hamsini zake badala yake drama kama hizo za kuchepuka ndio inakuwa njia ya kutokea na kumaliza mahusiano.
 
Basi huo ndio msingi wa tatizo. Ungeimiza tujenge utamaduni wa kuambiana ukweli mapenzi yakiisha. Lakini kutetea kuchepuka you're wrong. Iwe kwenye mapenzi, biashara, urafiki n.k hakuna binadamu anaweza kuwa humble akisalitiwa
 
Mapenzi ni jambo linaloweza kuanza na kuisha hata kwa watu walio kwenye ndoa ila hapa Tanzania ni kama mwanamke akishaolewa hairuhusiwi mapenzi kwa mwanaume aliyemuoa yaishe.

Inashangaza watu wanaua watu, wanajeruhi na hadi kulawiti wanaume wenzao kwa sababu eti mke amechepuka!

Ile ahadi inayosemwa mtakuwa pamoja mpaka kifo kiwatenganishe huwa ni maneno tu kama katika kanga ila ukweli na uhalisia kwa binadamu haiko hivyo.

Wanaume wa Tanzania wametunga hadi msemo mke wa mtu ni sumu kwa hofu ya kuibiwa wake zao!
Ukichoka tengua kiapo, chukua talaka uwe huru na mambo yako, sio unalala kwa mume halafu unaliwa nje. Huo ni umalaya.
 
Back
Top Bottom