Arabian queen
JF-Expert Member
- Nov 23, 2016
- 2,557
- 4,824
Katika Kijiji cha Tombo, Kaunti ndogo ya Kakamega kaskazini, kuna mama mwenye upweke mwingi.
Bwanake alienda jijini Mombasa kutafuta riziki, hali ambayo imegeuka kuwa dhiki.
Bi Shikwekwe alibubujikwa na machozi alipokuwa akinihadithia jinsi bwanake alivyonaswa na kidosho wa Mombasa.
Baada ya kumsikiza kwa makini, niliamua kufanya utafiti kuhusu kwanini wanaume kutoka bara wanawapenda vidosho wa Pwani.
Ni nini ambacho wanawake wa Pwani hufanya ambacho wenzao hawajui?
Hili ndilo swali nilililowauliza wanaume ambao wamekaa Pwani kwa muda mrefu, bila kurudi nyumbani kuona familia zao.
Wanaume hao walisema kuwa mabinti wa Pwani ni warembo sana na pia wana heshima ya kupigiwa mfano.
Waliwamiminia sifa tele kama vile; kinga kwa kila ndwele, ghala la baraka, mabawabu wa penzi na chemichemi ya furaha.
Warembo wa Pwani ni vivuli juani na miavuli mvuani. Wao ni mwanga gizani, mavazi vulini na ngao vitani.
Wanafahamu fika mahitaji ya kujirembesha, na matamshi yao ni kama muziki sikioni na asali kwa ulimi wa mume.
Wanaume hao walisema kuwa wanawake wa Pwani ni amani rohoni, na pia ni kama chakula cha moyo.
“Sifa hizo ndizo sababu sitamani kurudi nyumbani. Siwezi ishi na mwanake ambaye haniheshimu, hajui kunipikia na hana madaha ndoani,” alisema mwanamume mmoja.
Aidha, walisema kuwa wanawake kutoka bara wanapaswa kuwaiga wenzao wa Pwani iwapo wanataka ndoa zao zidumu.