Kwanini wanatumbuliwa kwa fedhea?

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Watumishi wa umma na wateule wa Mhe.Rais wanatumbuliwa kwa fedhea kwa sababu ya kutenda kwa hisia siyo kwa utashi na ueledi waliojaaliwa na Mwenyenzi Mungu.

Wanaotenda kwa ueledi na utashi waliojaaliwa na Mwenyenzi Mungu hata wakitumbuliwa hawaondoki kwa fedhea bali wanaondoka kishujaa na kesho wanaporudi kwenye jamii wanapokelewa Kama shujaa.

Wanaotumikia hisia zao dhidi ya waliowateua Mara nyingi wanaondoka kwa fedhea na wanaishi na doa la fedhea milele yote.

Wapo watu walileta bao la mkono wakiamini watadumu milele kwenye serikali na chama matokeo yake leo hii tendo la wizi na dhuluma walilolifanya mwaka 2015 linawatesa wao na familia zao, MAANA Kati Yao wapo waliotumbuliwa kwenye uwaziri, wapo waliotumbuliwa kwenye vyeti feki, wapo waliotumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi na ambazo zilitengenezwa kisiasa na wengine siyo kutumbuliwa TU bali wamefarikk kwa mashinikizo ya damu.Wanateseka kwa sababu walisimamia hisia zao na kuwadhulumu baadhi ya wananchi haki zao kuanzia kata, Jimbo na hata urais.

Wabunge wa CCM waliolewa fika kwamba kikokotoo kitawatesa wananchi na hata kama hawakujua walielimishwa kwa kina na akina Marehemu Bulago wa kakonko lakini hawakutaka kusikia wakapitisha bungeni na waziri akatunga kanuni na kuzipitisha.

Badala ya Sheria na kanuni hizo kupita hazikuwaathiri wapinzani TU bali zilikwenda kuondoa kabisa trust ya wananchi kwa chama Cha mapinduzi. Kwa kuwa uchaguzi unakaribia na wananchi bila hata kusema adharani tayari Wana majeraha ya kikokotoo basi mwenye nchi akaona arudi kutekeleza maneno ya wapinzani na kufuta kikokotoo Cha 25% na kurejesha Cha zamani.

Je, ni kweli kwamba wabunge zaidi ya Mia tatu was CCM walishindwa kuona kwamba Sheria hii ni kandamizi kwa wananchi? Je wanasimamamia maslahi ya wananchi au maslahi Yao?Kama kwenye Jambo Kama hili wamewasaliti kabisa watumishi na wafanyakazi tutaamini vipi kwamba wanatuwakilisha?

Je, ni Rais ndio msikivu tu katika chama Cha mapinduzi?

Haya ya wafanyakazi ndiyo yaliyouza rasilimali na utajiri wa wananchi kwa mabepari na Mabeberu, wanaccm hawapo kwa maslahi ya wengi Bali maslahi Yao binafsi na chama Chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesahau a napenda sifa ukabila undungu wivu majigambo na takataka zote ni zake


SWISSME
 
Back
Top Bottom