Kama kuna anayefahamu maneno wanayoyatumia katika viapo hivyo ayaweke hapa ili tuyachambue. Wanakula viapo lakini bado wanapokea rushwa, mafisadi na waroho wa kujilimbikizia utajiri wa haraka haraka kupitia nyadhifa zao na siku zote hufanya maamuzi ambayo hayana maslahi kwa Tanzania.
Kuapa ni tradition ambayo ipo kwa miaka mingi. Swala zima la kuapa linaonyesha commitement yako toward public services. However, majority wa viongozi wanaapa then wanaingia madarakani wanafanya utombo.
Maneno wanayoyatumia ni kama ifuatavyo:
Mimi Bubu Msemaovyo ninaapa kwamba nitailinda na kuitetea katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwamba nitamshauri kwa hekima Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na kwa vyovyote sitatoa siri za baraza la mawaziri, ee Mwenyezi Mungu nisaidie.
Jamani nimejaribu tu ila kuna vijineno fulani fulani nimevisahau.
Kuwa mwanasiasa hakuhitaji kiapo. Ila kushika wadhifa unaohitaji kulinda na kutetea katiba ya nchi kunahitaji kiapo.
Hata hivyo, kumbuka kwamba definition ya mwanasiasa ni mtu anayeweza kuzungumza bila kusema kitu. Wanapoapa, usidhani kwamba kuna kitu wanasema, au kuna commitment ya kweli. They are just being themselves
Lakini kama hicho kiapo hakiwabani wakifanya makosa ni nini basi waape kuchukua nyadhifa za umma ?
Naomba wanasheria wanisaidie je Waziri anaweza kufunguliwa mashtaka kwa kufanya jambo kinyume cha kiapo, pia je kama ndio hivyo kwanini tusiwapeleke mahakamani badala ya kuunda tume ?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.