Kwanini wanaosifia awamu ya 5 ni viongozi tu na sio wananchi wa kawaida?

BIGURUBE

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
6,743
4,227
Kwa Utafiti wangu mdogo niliofanya naona awamu hii ya 5 wale wanaoisifia na kuipamba ni either viongozi wa nchi DC, RCs, DEDs, mawaziri au wanachama wa ccm tena wanaoishi kutegemea siasa, sijaona mwamko wa wananchi ww kawaida wakitoa sifa kwa serikali yao!

Hapa ninachokiona ni kuwa serikali hii ya chini ya JIWE inajitahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo miradi mikubwa ila imewasahau wananchi wa kawaida wanaozidi kuwa masikini wa kutupwa!

Ukiangalia tatizo la ajira linazidi kukua Kila mwaka, vijana wanamaliza vyuo bila kuajiriwa, sekta binafsi hali ni mbaya Kila cku biashara zinafungwa na wafanyakazi wanapunguzwa kazi!
 
wanalipwa kusifia, ni kama kikosi cha propaganda, bwana yule anadhani watanzania ni wajinga sana kiasi kwamba kama akisifiwa sana na hao vigagula wake basi wananchi pia watashawishika kumpenda, mimi binafsi nimetembea huku na kule hapa nchini kwetu na niseme huyu ndio rais asiyependwa zaidi kuwahi kutokea, kila mtu anamlalamikia yeye kwa kila tatizo, picha yake ya ukatili na roho mbaya imeshakaa vichwani mwa wananchi.
 
Na huo ndio ukweli anae sifia namba 5 ananufaika nayo akina kajamba naniii tumejawa sumu wakati ni ukuta nalo litapita ila inahitaji mauvumilivu ya hali ya juu mwaka wa 4 sasa ajira nazisikia tu zikihubiriwa kwenye screen mpaka namkumbuka mzee wa msoga
 
wanalipwa kusifia, ni kama kikosi cha propaganda, bwana yule anadhani watanzania ni wajinga sana kiasi kwamba kama akisifiwa sana na hao vigagula wake basi wananchi pia watashawishika kumpenda, mimi binafsi nimetembea huku na kule hapa nchini kwetu na niseme huyu ndio rais asiyependwa zaidi kuwahi kutokea, kila mtu anamlalamikia yeye kwa kila tatizo, picha yake ya ukatili na roho mbaya imeshakaa vichwani mwa wananchi.
Wakati ni ukuta nae atapita ila anachotufanyia wa Tz Mungu anamuona
 
Wananchi wa Kawaida wapo lakini ukiwachunguza kwa Undani utagundua wana Matatizo
kama sio ya Akili basi unaweza kukuta ni ya kitabia, Mfano kuna mmoja ambaye hapo kabla
nilikuwa namheshimu sana lakini toka nimegundua kuwa ni shoga ingawa ni kwa Usiri sana
sina hamu nae.
 
Halafu kuna praise team iliyoko kwenye payroll na praise team bendera fuata upepo
na tupo sisi ambao ni sincere pia. Bongo nchi masikini sana, tukibembelezana hatutaenda popote. Kampuni kama Facebook ina thamani kubwa kuliko nchi yetu ndo nini sasa? Mimi tukifika budget ya $200+ billion na tukawa hatuna maisha mazuri tutaacha kupongeza. Tupo watu ≈mill 60 na budget yetu kwa mwaka ni chini ya $60 billion, maisha mazuri tutayapataje? Ukiwa unaishi bongo leo inabidi ukubali kuna hali ngumu
 
Hawezi kuwateua wote pia hawezi kusifiwa na wote.

Those who eat national cake ndio good praise team
 
Ukimsifia JIWE utaendelea kukalia SITI mpaka mwisho na ukimchallenge tu siku hiyo hiyo hata saa 7 usiku GERSON MSIGWA na EMMANUEL BUYOELA utaona Press Release zao,Kwahiyo viongozi washajua kula na "KIPOFU".
 
Kuna wakati huwa nawaza bora tuongozwe na marais waislamu tu badala ya hawa wakristu (wakatoliki) wenzetu. Kuna dalili ya uungwana na ubinadamu kwa hawa wenzetu bila shaka.

Mifano ipo hai kabisa. Wakati wa Nyerere, maisha ya watanzania yalikuwa ni ya mateso makuu! Yslijawa na ubinafsi tu kiasi hadi tetesi zinasema alikuwa anaangalia mwenyewe tu tv pale ilkulu huku akitutaka wengine wote tusikilize redio ya propaganda za chama na serikali RTD.

Kaja Mwinyi, watanzania wengi tukaishi maisha mazuri huku pesa ikiwa nje nje! Alipoingia Mkapa, na yeye akatuletea Ukapa wake! Hela ikawa adimu kweli kweli! Alipoingia mzee wa Msoga, kama kawa hela ikarudi kwa wananchi! watumishi wa umma tulipandishwa madaraja kwa wakati, incriment kila mwaka ilikuwepo kama kawaida, aliongeza mshahara, nk.

Sasa ameingia huyu mkatoliki mwingine, na yeye anaturudisha tena kule kule kwa watangulizi wake! Hivi hii hali ni ya bahati mbaya au ni kutofautiana tu kwa mioyo kati ya hawa wenzetu wa upande wa mashariki na sisi wa magharibi? Mbona wakristu tuna roho za kibinafsi na kikatili sana?
 
Back
Top Bottom