Elections 2010 Kwanini Wanaoshindwa kutoka CCM wanataka kura zihesabiwe upya? wanatufundisha nini?

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,816
11,192
Napata tabu sana kuelewa hawa wagombea wa CCM ambao karibia wote wakishindwa wanataka kurudia kuhesabu au wanakataa matokeo

tunajifunza nini kutoka CCM? kwamba wao huwa hawashindi kihalali?

Au wengi wao walishinda primaries kwa mtindo huo?
 
Wakihesabu upya, Kura za CCM zinakuwa zimeongezeka kwa vile zinazaliana. Kama vile Mahanga angefanikiwa kuingiza yale mabunda ya kura alizokamatwa nazo angesema tuhesabu upya, ungekuta ameshinda kwa kishindo 80% kama kawaida ya maajigambo ya CCM!!!! Kule wanakokuwa wameshinda, hakuna kuchelewesha matookeo wala kuhesabu upya. Tafakari
 
what? Mahanga alikua na kura za kuchakachua?
 
Wakihesabu upya, Kura za CCM zinakuwa zimeongezeka kwa vile zinazaliana. Kama vile Mahanga angefanikiwa kuingiza yale mabunda ya kura alizokamatwa nazo angesema tuhesabu upya, ungekuta ameshinda kwa kishindo 80% kama kawaida ya maajigambo ya CCM!!!! Kule wanakokuwa wameshinda, hakuna kuchelewesha matookeo wala kuhesabu upya. Tafakari
Ukweli ni kwamba CCM bila kujua madhara ya watu wao kugomea matokeo, wanatuonyesha jinsi wasivyokua waadilifu na wezi wakubwa wa kura... wanatia kinyaa

ni kawaida ya mwizi, siku zote huhisi anaibiwa, and that is exactly what CCM is doing

Ombi langu ni kwamba vijana wasichoke kuzuia uchakachuaji... CCM wanatumia ile mbinu ya kuchelewesha vijana wachoke kulinda halafu waibe

ikibidi tufanye harambee kwa majimbo yenye matatizo na ntatoa mchango wangu
 
Kuna kura zinaingizwa wanapoleta masanduku sehemu nyingine. Halafu wanaporudia idadi inakuwa imebadilika. Hiyo ndiyo strategy yao kuchakachua. Inatakiwa kuwakatalia kabisa kuhesabu upya.
 
Ukweli unauma na siku zote CCM huwa ushindi hawaupati kiuhalali sasa kwa kuwa mwaka huu wameonja shubiri ya matokeo ya Ubunge wanaona ni kama vile haiwezekani na kitu kama hicho hakiwezekani kuna mtu aliwahi kusema demokrasia ya kweli itapatikana pale CCM itakapoondolewa madarakani sasa wanakuwa wagumu kukubali matokea kwa sababu wanaona kama ni miujiza kwao mambo yanayotokea
 
Back
Top Bottom