cheupedawa_
Member
- Aug 12, 2019
- 20
- 16
Nimejaribu kufuatilia kwa muda mrefu sasa, hili kundi la watu wachache wanaopigia kelele utendaji wa serikali ya awamu tano, nikagundua kuwa wengi wao ni wale walipata kuwa vigogo kwa muda mrefu ndani ya chama tawala na serikali katika awamu zilizopita ambao tayari walikuwa wameshasimika mizizi yao katika mkondo wa upigaji, na wengine ni watoto wa vigogo hao au ndugu zao wa karibu walioathirika na maboresho ya mfumo mpya.
Najiuliza wakati wananchi wengi wanyonge walipokuwa wakilalamikia ugumu wa maisha, na kuomba mabadiliko makubwa ya kiuongozi serikalini hawa watu walikuwa wapi? Mbona hawakupiga kelele kama wanavyofanya sasa, wakati wanyonge wengi wakiwa wameridhika na nama serikali hii inavyoendeshwa?
Je, wakati rushwa ikiwa imetamalaki, huduma za msingi za kijamii kama vile afya zikiwa zinatolewa zaidi kwa walionacho; hawa wanaojiita Wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wapi? Je, kupata huduma bora za afya na huduma nyinginezo za kijamii si mambo yanayowahusu?
Tukumbuke vurugu zote za uchaguzi wa 2015 zilitokana na kile kilichodaiwa kuwa ni watu kuchoshwa na ugumu wa maisha, rushwa iliyokithiri na mengineyo, ambayo kwa awamu hii yamefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa; kipindi hicho wanaolalamika sasa walikaa kimya, na hawakuona kuwa hali hiyo ilihitaji kuisemea.
Tuliolalamikia mfumo uliopita, tujikumbushe tuliomba tupate nini kutoka kwa Rais ajaye, na kama tumekipata au laa; na tuwapuuze wanaotaka kutuvuruga.