Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
- Thread starter
- #21
Acha kuleta uzi wa upotoshaji kutaka kuonyesha mambo ni mazuri wakati sio kweli. Lete mnyonge ambaye amefaidika na utawala wa awamu huu, mpaka aone tofauti kubwa na siku za nyuma. Kinachofanyika hivi sasa ni kunyima uhuru wa wananchi kupaza sauti, kisha wanaishia kulishwa maneno na serikali ili kuhadaa umma kwamba mambo sasa ni mazuri.
Kuna uminywaji mkubwa wa vyombo vya habari, na taarifa pekee zinazotakiwa kuwafikia wananchi na miradi ya serikali, kisha miradi hiyo ndio inatumika kuzibia maumivu ya wananchi wasisikike kile hasa kinachowasibu. Ukweli ni kuwa hali za wananchi ni mbaya kuliko kawaida, japo kweli kuna miundombinu inaendelea. Uzuri ni kuwa propaganda haziwezi kufunika ukweli wa hali halisi za wananchi.
Wewe mtu mzima unakubalije mtu akujaze maneno ya kusema? Kuna watu hata huyo Magufuli hawajawahi kumuona live, lakini huwezi kuwaambia kitu kwa sababu effect ya anachofanya is far reaching. They can feel it from where they are.