Kwanini wanaoamini Mungu wanapenda kutisha watu na kuwa wakali wanapoulizwa maswali magumu?

young MathematiciAn

Senior Member
Oct 31, 2016
160
361
Kwa muda mrefu nimekuwa natafakari hivi kwanini watu wanaoamini uwepo wa Mungu wakiulizwa maswali hasa yale magumu huishia kutukana na kutishia watu na huwa wakali mithili ya mbogo aliyefukuzwa na Nyati wenzie .

Mara nyingi huwa hawajibu hoja bali wanamshambulia mtu na kumtisha utaenda motoni wewe ,subiri ufe utaona au wewe ni mpumbavu wakitoa aya inayosema mpumbavu moyoni husema hakuna Mungu.

Nimefanya utafiti na kugundua 99% ya wanao amini Mungu hawawezi kufanya mdahalo,kujibu hoja.Ukimuuliza swali au kumtolea hoja ngumu lazima atoke nje ya mada hapo utatishwa utageuzwa kuwa sisimuzi mara subiri ufe uone utakavyounguzwa,utakejeliwa,utatukanwa.


Mbona wanafikra huru wasioamini Mungu wapo calm, hutoa hoja na kujibu bila panic.


Kwanini huwa hivyo wadau wa Jamii Forum shida inakuaga wapi ?
 
Kuna kitabu nilisoma kinaitwa "When bad things happen to good people"
kilifungua sana uelewa wangu!

Ukiona unauliza maswali MTU anakua mkali jua huyo bado hajayajua maandiko vizuri
 
young MathematiciAn,
ili uwe muumini mzuri unatakiwa uwe na upungufu kuhoji, nao hukunyima uwezo wa kufikiri, tokeo ni kukosa majibu ukiulizwa, na kutoa majibu ya mkato na yasiojidhi.
 
Kuna jambo moja ambalo baadhi yetu huwa hatuelewi au hatuelewani
Ni hivi

Si kila swali, linafaa kujibiwa

Si kila swali, lijibiwe kama utakavyo wewe

Utofauti wa akili na ufikiri kwa Binaadam, huleta maana tosha ya mipaka ya akili kwa mwanada

Akili ina mipaka, kama yalivyo macho kuwa na mipaka katika kuona

Akili inamapungufu
Basi mwenye kuifanya akili yake ni Dalili tosha, huyo atakuwa anaonyesha rangi halisi ya mapungufu yake
 
mtu amwaminie Mungu kweli awezi kuwa mkali aulizwapo kwa busara na kama swali liko kwa muundo mzuri wa uulizaji!
ila ukali unakuja pale tu mtu aulizapo swali ambalo ni wazi kabisa linamkashifu Mungu!
hii ni sawa na mtu kumkashifu mzazi wako we unadhani utakuwa mpole na wakati umeumbwa na hasira?
 
Kujibu hoja hizo inataka mtu awe na elimu au kasoma au kafundishwa.
Sio kwamba mtu anajua kila swali lakini akiona unapotosha au kutokuafiki anacho amini hapo ndio ngumi zinaanza haha

Hata wewe ukiambiwa huyo Baba sio baba yako mzazi ingawa unalijua hilo lakini ukiambiwa prove it itabidi utupe ngumi
Hilo tu

Na takwimu za 99% sidhani kama ni sawa
 
Mim naamnin Mungu yupo.....na ushahidi wake wote umejengwa juu ya msingi wa imani...zaidi ya hapo hakuna udhihirisho wa asilimia 100...mwisho wa siku utachukizwa hata kusikia neno Mungu...kuna maswali ambayo waweza kujibiwa ila kuna mengine hakuna mwanadamu wa kuweza kuyajibu..Kumbu kumbu la torati 29:29
 
Back
Top Bottom