Kwanini Wananchi Wanamtumainia Rais Magufuli?

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana jf, nimeona bora nami nitoe mawazo yangu juu ya mitazamo iliyopo sasa hivi kwa hizi siku 100 za Rais Magufuli. Kuna wale wanaokubali kweli Rais atatupeleka mahali na wengine wanaobeza kuwa hajafanya chochote. Basi mimi nimeona nianzie katika swali lililopo hapi juu.
Mimi nafikiri watu wamepata matumaini si kwa maneno makali tu yanayotolewa na Mh. Rais kwenye hotuba bali ni mabadiliko yaliyopo sasa hivi kwenye sehemu mbalimbali za umma penye kutolewa huduma, kwa mfano mahospitalini na ofisi mbalimbali za serikali. Zamani ilikuwa ukiingia ofisi za watu unaonekana kama umepotea, hivi sasa ni mheshimiwa unakirimiwa kama mfalme. Hospitalini manesi walishakuwa Miungu watu kwa wagonjwa haikujalisha unaumwa kiasi gani ilikuwa ni kukalipiwa kwa kwenda mbele lakini sasa hivi kwa wale ambao tumeshafika mahospitalini hata kama sisi wenyewe si wagonjwa lakini hata kuwasalimia ndugu zetu tumeona mabadiliko.
Watu wanahoji juu ya mfumko wa bei, hivi kweli hata wewe ukipewa Urais unaweza shusha mfumko wa bei kwa miezi 3? Au watu wanafikiri ni kitendo cha Rais kuamuru sasa bei shuka? Hebu hata wewe fikiria tu hizi sababu mbili tu za mfumko wa bei ungeweza kuzishughulikia vipi?
1: Kupanda bei za vyakula ukizingatia sasa hivi si kipindi cha mavuno. Mwenye solution atupe.
2:Kupanda kwa thamani ya dola ukizingatia una-import zaidi kuliko ku-export. Mwenye solution atupe, kwa sababu huwezi kunambia kwamba ndani ya miezi mitatu Rais anaweza kuandaa ya ku-export zaidi kuliko ku-import.
Ndugu zangu Watanzania nchi yetu ina changamoto sana kuliko watu wanavyofikiri. Mimi mpaka sasa hivi namuona Rais anahangaika na kurudisha mahali pake utumishi bora wa umma ambao utaondoa ubadhilifu na unyonyaji ambao umechangia kiasi kikubwa kuwepo kwa matabaka ambayo mwisho wa siku yangetufikisha pabaya, masikini wa kutupwa na matajiri waliopindukia. Hebu fikiria ni unyonyaji gani huo uliopo, mfanyabiashara ya mafuta anawauzia walaji wa mwisho wa bidhaa yake kwa bei sawa na bidhaa iliyolipiwa kodi ilhali yeye kakwepa kodi ambayo serikali ingemrejeshea mlaji huyo kwa kukusanya kodi na hiyo pesa ya kodi ingetumika katika huduma mbalimbali za kijamii. Leo ndo mambo ambayo bado anahangaika nayo lakini kuna mtu bado anabeza haoni kitu! Tuungeni mkono juhudi hizi ili Rais serikali yake ifikie kwenye kushughulikia mambo ambyo yana matokeo ya moja kwa moja kwenye maisha ya Mtanzania mmoja mmoja(individual) kama vile mfumko wa bei ambayo ni process, ukosefu wa ajira ambayo pia ni process kwani si mambo ya kulala leo kesho ukaamka umesolve.
Rai yangu kwa Watanzania wenzangu hata sisi tubadilike siasa zimetuzidi, hatutaenda popote tutabaki kuhangaika kutatua mambo ya kisiasa siku zinaenda.
 
nguvu mchango.

http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Upo sahihi kabisa. Wanao beza hawafai kabisa
 
kuna aliyekuwa rafiki yangu sana ni marehemu sasa anaitwa Frank Sumbizi aliwahi kusema, nchi inataka kiongozi mwenye dhamira ya kweli na anayesimamia maneno yake nami naiona kwa JP. Pumzika kwa Amani Mjomba Mjomba Sumbizi!
 
Back
Top Bottom