Kwanini wanamsakama Waziri Simba - Jaji Werema

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,663
..naona Mwanasheria Mkuu Jaji Werema kaamua kununua kesi ya Sophia Simba.

..Jaji Werema amesemai:"Kwa nini wanamsakama Waziri Simba, wanisakame mimi siyo Waziri."

AG ahofu nchi kuwa na Rais mpenda vita

  • Ashangaa waliohoji madaraka makubwa ya Rais sasa wapinga

MUSWADA wa Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 umezidi kubainisha tofauti ya mitazamo kati ya Serikali na Bunge, ingawa pia tayari serikali iliridhia kuchomoa muswada huo ili ukafanyie kazi zaidi kama ambavyo Bunge limetaka, Raia Mwema limethibitisha.

Katika mazungumzo maalumu na Raia Mwema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema amehoji, itakuwaje siku nchi itakapokuwa na Rais anayependa vita na kushangazwa na watu waliokuwa wakidai mamlaka ya Rais ni makubwa mno, lakini leo wanapinga muswada huo.
Akihoji kujadili sheria kwa kuangalia uongozi wa sasa, Jaji Werema amesema: “Sio siku zote tutakuwa na marais wapole kama Mwalimu Julius Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete.”
Kwa mujibu wa mapendekezo ya muswada huo, uamuzi kuhusu usalama wa nchi na hasa wa kuamua nchi iingie vitani au la na nchi nyingine unatajwa kutolewa kwa kupigwa kura na wajumbe wa Baraza hilo ambao wanapswa kuwa 20.
Uamuzi wa kupiga kura, unatajwa kumnyang’anya mamlaka ya Rais ambayo kwa sasa Katiba inamtambua kuwa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu suala la usalama wa nchi.
Lakini wakati wabunge waliopinga muswada huo ambao baadhi ni wakongwe wa siasa nchini na viongozi wastaafu wanaamini muswada hauko sawa, AG anasema; “Sio siku zote tutakuwa na marais wapole kama Mwalimu Julius Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete,”
“Siku nyingine tunaweza kuwa na Rais anayependa vita kama mimi, nikisikia nchi inatuchokoza tu naamuru vita, nasema ni vita tu kilimo kwanza baadaye...itakuwaje kama sitapunguziwa madaraka?
“Zamani wakati tunapata uhuru tulimpa madaraka makubwa Rais kutokana na weakness ya system...sasa hivi ni miaka zaidi ya 40 tangu Uhuru mazingira ni tofauti hivyo ni lazima tubadilike, wanasema Katiba inavyunjwa mimi sioni inavunjwa wapi,” alisema.
Kwa upande wa hoja za wabunge kuhusu muswada huo, wameeleza kuwa licha ya kumnyang’anya mamlaka Rais, lakini pia usiri katika masuala ya usalama wa nchi usingeweza kudhibitiwa kutokana na baraza hilo kupendekezwa kuwa na idadi kubwa ya wajumbe.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, wakati wa kuchangia muswada huo alisema, sheria ambayo ingetungwa kutokana na muswada huo ingeweza kusababisha Rais wa Tanzania apinduliwe.
Mbunge huyo wa Wawi, Zanzibar alisema hakuna sehemu yoyote duniani inayopiga kura kuhusu masuala ya ulinzi hivyo muswada huo haufai.
“Suala la ulinzi ni time, ukichelewa dakika mbili umekosea...ulinzi bwana ni amri. hakuna sehemu duniani ulinzi unapigiwa kura” alisema Hamad Rashid.
Wakati mbunge huyo akiwa na mtazamo huo, Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo, aliibua hoja ya baraza hilo kuwa kubwa mno akitilia shaka uwezo wake wa kutunza siri za kiusalama na kusisitiza kuwa; kitaalamu, watu saba hadi tisa tu ndiyo wanaoweza kutunza siri za Serikali, wakizidi utakuwa ni sawa na mkutano wa hadhara.

Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo, amesema, Baraza la Usalama wa Taifa si kongamano au sehemu ya kujadiliana, ni mahali pa uamuzi na kwamba; Rais wa Tanzania ni Amiri Jeshi Mkuu, aachiwe madaraka yake ya kuamua kuhusu masuala ya ulinzi na usalama wa taifa. Akahoji; “Julius Nyerere alipoamua taifa liingie vitani Kagera, kongamano gani lilikaa?
Mbunge wa Mtera, John Malecela amesema, muswada huo umewasilishwa bungeni wakati usio muafaka, ukarekebishwe, upelekwe bungeni wakati unaostahili.

Malecela ametaka Rais aachiwe madaraka ya kuamua kuhusu masuala ya ulinzi wa nchi na ameuliza, ni wapi Rais aliyechaguliwa anakuwa na kamati kubwa ya kumshauri kuhusu masuala ya vita.
Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa aliukataa muswada huo si tu uliotaja kugongana na Katiba lakini pia alisema muundo wa Baraza la Usalama wa Taifa ni lazima uwe mzuri, hivyo wahusika waangalie nchi nyingine wanafanya nini.

Hata hivyo, takriban siku nne tangu muswada huo ukataliwe kwa hoja za aina hiyo za wabunge, Serikali kupitia AG inaeleza kuwa maoni ya wabunge yatazingatiwa maelezo ambayo hata hivyo yanaonyesha msisitizo wa umuhimu wa muswada huo kwa wakati huu.

Kuhusu hoja ya kuvunjwa Katiba kutokana na kuwasilishwa kwa muswada huo, AG ananukuu Idara ya 37 kifungu cha kwanza cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Ibara hiyo ya 37 (1) inasema; “Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.”

Jaji Werema anakanusha kwamba kuwasilishwa kwa muswada huo wenye mapendekezo yanayodaiwa na wabunge yanapora mamlaka ya Rais, kwa kunukuu kifungu hicho cha 37 (1) na hususan maneno yanayotamka; “....isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote.

Katika hatua nyingine, AG alihoji ni kwa nini anayeandamwa kutokana na kukataliwa kwa muswada huo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sofia Simba na si yeye, ambaye ni Mwanasheria Mkuu. “Kwa nini wanamsakama Waziri Simba, wanisakame mimi siyo Waziri,” alisema AG.
 
Unajua tangu mjadala huu unaanza nili risk kwenda against the stream hapa JF, the popular tide being kum bash Sophia Simba.

Now, that Sophia Simba is an airhead is granted, no debate on that.

Lakini nilikuwa nasema point hii hii anayoisema AG. Jamani kumpunguzia rais madaraka kuna ubaya gani? Kuondoa dictatorial decree kuna ubaya gani? Hata huyo Julius Ceasar alikuwa na Senate linamcheck ingawa alitaka kuwa dictator.

Nikaomba kuelimishwa maana sina details za muswada, je kuna mgongano wa katiba? Watu kimya.Dr. Slaa yuko wapi aje kutufafanualia inakuwaje mpinzani akatae rais kupunguziwa madaraka? Hili si ni moja ya maeneo tunayoyapigia kelele kila siku kwamba rais ana madaraka makubwa sana kiasi anakuwa kama kimungu mtu fulani hivi?

Nimeshukuru sana kwamba Jaji Werema ame own this issue.Mimi napenda sana mtu anayeweza ku step up to the plate na ku take ownership of issues, regardles on whether one is right or wrong, at least tunajua msimamo wa AG, na AG kaichukua hii issue kutoka mikononi mwa Simba (kichekesho ni kwamba AG wetu ni jaji, sasa ikija siku kuna conflict of interest kati ya Judiciary na executive atakuwa pahala pabaya sana, hii nchi ya ajabu kabisa, but that is a totally different animal warranting it's own thread).

Kwa hiyo nauliza wanaopinga hili baraza fundamenytally (ukiondoa hao wanaodebate number of members, that can always be adjusted) nawauliza, objection inatoka wapi?
 
Jamaa kakurupuka.

"Jamaa kakurupuka" is the height of obscurity.

Jamaa gani? Werema, Simba, Shellukindo, Sitta, Diallo, Malecela, Kiranga? Nani?

Kakurupuka kwa nini? Kivipi? Wapi? Kwa sababu gani unasema hivyo?

Angalia isije kuwa wewe ndiye unayekurupuka.
 
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, wakati wa kuchangia muswada huo alisema, sheria ambayo ingetungwa kutokana na muswada huo ingeweza kusababisha Rais wa Tanzania apinduliwe.
Mbunge huyo wa Wawi, Zanzibar alisema hakuna sehemu yoyote duniani inayopiga kura kuhusu masuala ya ulinzi hivyo muswada huo haufai.

For the United States, Article One, Section Eight of the Constitution says "Congress shall have power to ... declare War".

Wamarekani wana compromise iliyo workable kati ya the need for a speedy declaration of war if needes and the checks and balances of a national security council / congress.

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Declaration_of_war_by_the_United_States[/ame]

Huyu Hamad anajisemea tu.
 
Kiranga,

..kuna mahali Jaji Werema amedai kwamba Baraza la Usalama lipo, na linafanya kazi, tatizo halitambuliwi kisheria.

..nadhani huyu Mwanasheria Mkuu amekomaa na nimekuwa impressed na jinsi anavyoitetea hoja yake. katika kuchangia hoja hii tunapaswa kuangalia beyond mtoa hoja, ambaye ni Waziri Sophia Simba.
 
This is exactly what I am talking about. Kuna tendency ya ku-dumb down issues, let's deal with the fundamentals. Kuna tatizo gani kumpunguzia rais madaraka na kuondokana na udikteta?

Siku Tanzania ikipata mtu kichaa aliyejua kuficha makucha yake through the process of uchaguzi, halafu akawa rais mpenda vita zisizo adabu, tutamzuia vipi?
 
Hiyo ndio demokrasia. Waziri ni lazima aweze kuwashawishi wabunge juu ya kile anachakusudia kiwe sheria. Haya anayoyasema AG alipaswa amshauri/fundishe waziri ili aweze kuutetea muswada wake. Kusemea huku nje wakati waziri ameshaboronga hakusaidii sana.
 
Waziri so far anachodaiwa kuboronga ni kushindwa kutetea hoja.

Na waziri, despite kuwa airhead, hata kama angekuwa smart angekuwa na wakati mgumu kuutetea huu muswada. Let's face it, serikali ya Kikwete haiko enthusiastic kuhusu muswada huu.Muswada huu umetoka kwa AG, na hapa ndipo point yangu ya kwamba hizi appointments za Kikwete zinachekesha, kwa sababu inaonekana AG amekuja anafikiria legally zaidi ya politically.Basically tushukuru kwamba haya mambo yame work out in a serendipitous way.

Nasema Simba alikuwa na wakati mgumu kuutetea muswada huu kwa sababu hata angekuwa smart, fundamentally jinsi ya kuutetea muswada huu ni kusema kwamba rais ana mamlaka makubwa na sasa imefika wakati tuyapunguze.That is a very tricky statement kwa waziri wa Kikwete ku make kwa sababu inaweza ku open a can of worms.Ndiyo maana sishangai kwa waziri Simba kushindwa kuutetea muswada huu, kwa sababu hata mtu smart angepata shida.

Hapa, katika nchi inayoelewa checks and balances, wabunge walitakiwa kufurahi kwamba nguvu za kichwa cha mhimili wa executive zinapunguzwa na kuwa diluted kwa watu wengine.Lakini sisi hatuna bunge linalofuata checks and balances, sisi tuna bunge la party politics, na watu wanamuangalia rais si kama rais tu, bali pia kama mwenyekiti wa CCM, kwa hiyo kumpunguzia nguvu rais ni kuipunguzia nguvu rais, acheni rais awe demi god, CCM itakuwa chama cha demigods.Ndivyo tunavyofikiria.

Which puts Slaa in a very bad position.Kwa kujua yote haya, kwa nini na yeye ana support utumbo huu wa kukataa rais kupunguziwa madaraka? Is he trying to pull a Mrema?
 
Nasema Simba alikuwa na wakati mgumu kuutetea muswada huu kwa sababu hata angekuwa smart, fundamentally jinsi ya kuutetea muswada huu ni kusema kwamba rais ana mamlaka makubwa na sasa imefika wakati tuyapunguze.That is a very tricky statement kwa waziri wa Kikwete ku make kwa sababu inaweza ku open a can of worms.Ndiyo maana sishangai kwa waziri Simba kushindwa kuutetea muswada huu, kwa sababu hata mtu smart angepata shida

Nimekuelewa Kiranga.

Lakini huu muswada sio mara ya kwanza unakwama bungeni. Mimi naamini baraza la mawaziri chini ya uwenyekiti Rais linaufahamu hivyo sion huo ugumu wa waziri kuutetea ungetokea wapi.

Unless kama hiyo understanding yangu ya kwamba baraza la mawaziri including Rais walikuwa aware na muswada huo haiko sahihi.
 
Attorney general ought to be commended for his decision to come forward, amid members of parliament's uproar in the proposed bill, and call it for what it is – a spade a spade. I agree with him our constitution must be amended in order to bring check and balance in the office of the president. It is important to understand that just like other human beings, presidents are also flawed. Consequently, we must create a mechanism that will ensure that our president doesn't abuse his/her power. Wahenga once said, " power corrupts, and absolute power corrupts absolutely."
 
Nimekuelewa Kiranga.

Lakini huu muswada sio mara ya kwanza unakwama bungeni. Mimi naamini baraza la mawaziri chini ya uwenyekiti Rais linaufahamu hivyo sion huo ugumu wa waziri kuutetea ungetokea wapi.

Unless kama hiyo understanding yangu ya kwamba baraza la mawaziri including Rais walikuwa aware na muswada huo haiko sahihi.

Of course baraza la mawaziri linaujua huu muswada. Lakini inaonekana kama muswada huu unakuwa forced upon them kutoka kwa wasomi wa judiciary. Na katika pluses ninazoweza kumpa Kikwete, whether as some sheer Machiavellian calculations or genuine benevolence, ni hii ya kutokuwa kichwa kigumu kwenye mambo kama haya, in some ways ananikumbusha rais Mwinyi. Siwezi ku-picture mtu kama Mkapa akubali muswada huu ufike hata bungeni kirahisi rahisi hivi. Labda calculations za Kikwete zinamwambia auachie muswada huu uende bungeni akijua ana watu wake bungeni watakaoupinga vikali, hivyo Kikwete at the end of the day ataonekana benevolent, kwamba anaruhusu mabadiliko radical, lakini hapo hapo atakuwa na uhakika wa kutolipa gharama ya kuondolea madaraka.

Sasa hapa AG Werema inabidi aende very carefully, kwa sababu Tanzania hushindi argument kwa logic na kuwa na scholastic points, unashinda argument kwa politics hata kama ni upupu, unamsikia Shellukindo anakwambia "Nyerere alitanmgaza vita alihitaji baraza gani?" yaani jamaa anakuwa haelewi ile point ya AG kwamba tusitegemee kila uchaguzi tutapata rais kama Nyerere, anaweza kuibuka mchizi hapa akaleta vita watu tukashangaa.

Uki i over analyze hii, unaweza kuona kama vile CCM inaanza kukubali pole pole kwamba haiwezi kuwa madarakani daima, na siku moja upinzani utaweza kuja kuchukua Ikulu, sasa ni bora waanze kumpunguzia madaraka rais pole pole ili isije kuwa mtu kama Mtikila anachukua urais halafu anawatia jela politburo nzima ya CCM kwa uhaini. But that (the last para) could just be my over-analysis.
 
This is exactly what I am talking about. Kuna tendency ya ku-dumb down issues, let's deal with the fundamentals. Kuna tatizo gani kumpunguzia rais madaraka na kuondokana na udikteta?

Siku Tanzania ikipata mtu kichaa aliyejua kuficha makucha yake through the process of uchaguzi, halafu akawa rais mpenda vita zisizo adabu, tutamzuia vipi?
hebu wewe naye unanichefua na kiswa nglish naamini tuna uwezo hata wa kuelewa hiyo lugha ya kigeni japo kwa asilimia 40% hivyo chagua lugha katika mchango wako wa mawazo ya kutumia kama ni kiswahili au Kiingereza siyo unachanganya changanya mambo hapa ebo!!
siyo, you know mimi nilikuwa nadhani amen forget aaaaaa! hiyo ni nini sasa????????
 
hebu wewe naye unanichefua na kiswa nglish naamini tuna uwezo hata wa kuelewa hiyo lugha ya kigeni japo kwa asilimia 40% hivyo chagua ya kutumia kama ni kiswahili au Kiingereza siyo unachangany changanya mambo hapa ebo!!

Usinichafue nianze kukuingizia legal terms za kilatini na mifano relevant ya symmetry za siasa na quantum physics hapa.

Kama ulikimbia umande shauri yako, mimi sijui kiswahili fasaha na wala sijui kiingereza vizuri, kwa hiyo ili kuwasilisha hoja vizuri bila kuumiza kichwa siku nzima napanga cha kuandika kama vile nataka kutoa hotuba baraza la usalama la umoja wa mataifa, nakupa mchanganyiko huu.

Last time I checked hii haikuwa against JF rules. Lesson A, you can't bully a bully.

Kama huwezi/ hutaki kusoma niweke katika ignore list yako.
 
..naona Mwanasheria Mkuu Jaji Werema kaamua kununua kesi ya Sophia Simba.

..Jaji Werema amesemai:"Kwa nini wanamsakama Waziri Simba, wanisakame mimi siyo Waziri."

Huyu naye! Ndiyo wale wale wa kufuata mstari wa Serikali bila kutafakari kwa kina.
 
Huyu naye! Ndiyo wale wale wa kufuata mstari wa Serikali bila kutafakari kwa kina.

Ukiielewa hii issue kiundani, huwezi kusema Jaji Werema anafuata mstari wa serikali.

Hapa kuna ana apparent picture - AG kutetea muswada wa serikali ni kufuata line ya serikali- halafu kuna a deeper picture iliyo real, kwamba kiukweli serikali haitaki muswada huu upite.

Sasa usitake kufanya sarakasi za bunge la CCM zikuzuge ukafikiri apparent picture ndiyo real picture.

apparentdepthimage.png
 
.....

Lakini nilikuwa nasema point hii hii anayoisema AG. Jamani kumpunguzia rais madaraka kuna ubaya gani? Kuondoa dictatorial decree kuna ubaya gani?

Kipengele kilichofanya huo muswada ukawa objected sio kumpunguzia rais madaraka pekee.

Pamoja na mambo mengine, kuna issue ya confidentiality kwenye hilo proposed baraza la usalama. Ni kubwa utadhani mkutano wa hadhara au kikao cha bunge. They need to brainstorm who the must be-s in that baraza.

By they way I second kwamba huo muswada mzima ungepatikana ungekata mzizi wa fitina.

In general, Sophia kachemsha. Kama angekuwa anauelewa huo muswada vizuri angeusimamia na kujibu zile hoja properly. Kushindwa kwake kufanya hivyo ndiko kumepelekea muswada kupigwa chini.

Kwa mfano, ameshindwa hata kutetea hiyo hoja ya kwa nini Rais apunguziwe madaraka. Amedhihirisha kwamba alikuwa desa one-to-one au alikariri tu, au hakuusoma kabisa. Na kama ni kutaka check and balances ziwepo kwenye madaraka, basi mhusika wa kwanza ni yeye Sophia Simba.
 
Ukiielewa hii issue kiundani, huwezi kusema Jaji Werema anafuata mstari wa serikali.

Hapa kuna ana apparent picture - AG kutetea muswada wa serikali ni kufuata line ya serikali- halafu kuna a deeper picture iliyo real, kwamba kiukweli serikali haitaki muswada huu upite.

Sasa usitake kufanya sarakasi za bunge la CCM zikuzuge ukafikiri apparent picture ndiyo real picture.

apparentdepthimage.png

Werema kupewa hiyo nafasi hakulazimishwa kufuata mstari wa Serikali kila siku iendayo kwa Mungu siku nyingine kwa kutumia utaalam wake katika mambo ya sheria anatakiwa kuwa mkweli na kusema hapa tumevurunda ngoja turekebishe, labda ndiyo katika kutetea kitumbua chake wasikimwagie nchanga (isomeke mchanga)
 
Ama said:
Kipengele kilichofanya huo muswada ukawa objected sio kumpunguzia rais madaraka pekee.

Pamoja na mambo mengine, kuna issue ya confidentiality kwenye hilo proposed baraza la usalama. Ni kubwa utadhani mkutano wa hadhara au kikao cha bunge. They need to brainstorm who the must be-s in that baraza.

By they way I second kwamba huo muswada mzima ungepatikana ungekata mzizi wa fitina.

In general, Sophia kachemsha. Kama angekuwa anauelewa huo muswada vizuri angeusimamia na kujibu zile hoja properly. Kushindwa kwake kufanya hivyo ndiko kumepelekea muswada kupigwa chini.

Kwa mfano, ameshindwa hata kutetea hiyo hoja ya kwa nini Rais apunguziwe madaraka. Amedhihirisha kwamba alikuwa desa one-to-one au alikariri tu, au hakuusoma kabisa. Na kama ni kutaka check and balances ziwepo kwenye madaraka, basi mhusika wa kwanza ni yeye Sophia Simba.

Ama,

..lakini hata walioupinga mswaada huu wameshindwa kuielewa dhana nzima ya kumpunguzia madaraka Raisi. some of them have rubbished the entire bill, and claim that is something so absurd, they have never seen such a thing in their entire political life.

..Mwanasheria Mkuu amekuwa quoted akisema kwamba,Baraza la Usalama lipo na linafanya kazi, tatizo ni kwamba halipo pale kwa mujibu wa Sheria. sasa hawa waliopinga mswaada huu ina maana hawana habari na taarifa hizo? unless wadai kwamba baraza la usalama la sasa hivi si kubwa kama hilo lililopendekezwa ktk muswada.

..at the end of the day, Mbunge hapaswi kuupinga/kuunga mkono mswaada kwa kutegemea umahiri wa Waziri anayewasilisha mswaada bungeni. Wabunge nao wanapaswa kuusoma na kuutafakari mswaada kabla ya kuukubali au kuupinga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom