Kwanini Wanakinondoni wamchague Salumu Mwalimu?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Hili ni swali linalohitaji majibu stahiki, na majibu haya yatatii kiu ya wanakinondoni kwa ujumla wake, na ifikapo siku ya uchaguzi hawatafanya makosa yatakaogharimu maisha yao kwakuwa dunia ya leo kura yako ndio maisha yako halisi.

Unga dukani, chumvi, sukara, mchele, kiberiti, mboga, mafuta ya taa na yakula, gesi na mkaa vitapatikana kutokana na namna ulivyopiga kura yako, elimu yako, ya mtoto wako na ya ndugu yako shuleni itapatikana kutokana na ulivyopiga kura yako, usafiri kwenda popote kinondoni na nje ya kinondoni utapatikana kutokana na kura yako, matibabu yako hospitalini yatapatikana kutokana na ulivyopigq kura, biashara zako zitafanyika kutokana na ulivyopiga kura yako.... Kwaujuma kura yako mwana kinondoni na yeyote katika jamhuri ya Muungano atambue siasa ni maisha yake halisi, na kura ndio uamuzi wa maisha yake.

Sababu za kuchagua UKAWA chini ya Salum Mwalimu wa Chadema zipo nyingi sana, lakini nitaeleza sababu KUU tu zitakazokuongoza wewe mwananchi wa Kinondoni kumpata Mbunge wako Mh Salum Mwalimu.

1. Kuendelea kuongoza jiji la Dar kupitia Ukawa mliyoiamini na kuipa madaraka ya kuongoza jiji la Dar, Uamuzi ule wa 2015 umeweza kuzaa jiji la Dar lenye mabadiliko chanya leo, Ambapo mafanikio yake ni kuona mambo Muhimu ya Miundombinu, elimu, Afya na Usalama katika jiji vimeendelea kuboreshwa chini ya UKAWA,

Kupitia UKAWA mliyoiamini 2015, leo jiji limefanikiwa kuwa na mabasi ya Mwendokasi ambao kwa miaka zaidi ya hamsini ya kutawaliwa na ccm jiji hili ilikuwa hadithi tu za kwenye makaratasi na hata uanzaji wa Mradi huo ulijaribu kuanzishwa chini ya uongozi wa Meya wa ccm aliyepita, ulionyesha kusuasua na kuzaa ufisadi tu wakuuza UDA, mpaka UKAWA tuliposhika jiji tukazuia ufisadi na mradi ukaisha na kuanza kutumika kama mnavyoona leo... Ujenzi na kukamilika kwa Daraja la Kigamboni, Ujenziwa Kuta za Fukwe pembezoni mwa Bahari, Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutani ya Ubunge na Tazara, Ujenzi wa maeneo ya kupumzikia katikati ya Jiji, Mradi Mpya wa Mabasi ya Mikoani kule Mbezi Kimara, Ujenzi na ukarabati wacmiundombinu ya barabara ndani ya jiji la Dar, Uratibu na Utoaji wa Ardhi ya Jiji kule Kigamboni maalumu kwa shughuli za viwanda vidogovidogo na biashara ya Magari nk.

Yote hayo yamefanywa chini ya Baraza la Madiwani wa Jiji linaloongozwa na UKAWA, sio Baraz la Mawaziri linaloongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, japo Mkuu wa Mkoa hupenda kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kujinadi kwamba yeye kafanya vile mara hivi, Uongozi wa Ukawa Jiji haupendi utendaji wa Show, bali kazi na taratibu... Mkuu wa Mkoa hana hata bajeti ya kununulia kalamu yake tu ya kuandikia vimemo, yenye ni mambo ya ulinzi na usalama tu na sio vinginevyo, mpaka kalamu yake ananunuliwa na Baraza la Madiwani jiji. Hili nawaomba muelewa, mradi wowote uliopo ndani ya Jiji la Dar, tambueni upo mikononi mwa Ukawa.

Ili kuendeleza mafanikio hayo, hakikisheni hampunguzi madiwani ndani ya Ukawa ambao ndio wanaoongoza jiji, kitendo tu cha kupunguza Mbunge ndani ya Jiji na kuwaongezea wingi wa wabunge ccm, basi wanakinondoni mtakuwa mmewasaliti wananchi wote wa jiji la Dar na kusababiji Meya wety wa jiji ashindwe kufanya kazi zake na mwisho tutaporwa jiji mchana kweupe.

2. Hali ya huduma za Afya katika jiji la Dar zimeimarishwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na miaka mitano ya nyuma ya utawala wa ccm katika jiji, Amani Hospital, Temeke Hospital, Mwananyamala Hospita, na Kisiwani Kigamboni Hospital zimeboresha huduma zao ambapo kwa zaidi ya 80% huduma kwa sasa zinatolewa kwa bima ya afya na kwa mfumo wa kiekektroniki, haya ni matunda na nguvu ya ufasini ya UKAWA, Hili halihitaji mtu awafafanulie, mnakiona kwa macho yenu mkifika kupata hudumu. Pia ndenda Muhimbili kuna mabadiliko makubwa, yote ni kwa sababu Ukawa ndio tunaoongoza jiji.

Ili kuendeleza mafanikio hayo, hakikisheni hampunguzi madiwani/Mbunge ndani ya Ukawa ambao ndio wanaoongoza jiji, kitendo tu cha kupunguza Mbunge ndani ya Jiji na kuwaongezea wingi wa wabunge ccm, basi wanakinondoni mtakuwa mmewasaliti wananchi wote wa jiji la Dar na kusababiji Meya wety wa jiji ashindwe kufanya kazi zake na mwisho tutaporwa jiji mchana kweupe.

Suala la Usalama nalo ni moja ya mambo yanayojadiliwa ndani ya Baraza la Madiwani wa Jiji, kwa namna ya pekee jiji la Dar Chini ya Ukawa limekuwa na matukio machache sana ya uhalifu, ustaarabu na kuheshimiana ndani ya jiji kumetamalaki vya kutosha.

3. Lakini hoja nyungine ya msingi kwa wanakinondoni ya kwa nini mmchague Salumu Mwalimu, ni kwamba, Taifa lipo kwenye mdororo wa demokrasia na uchumi, hali ya kitaifa imeletwa na CCM, hakuna mwanaccm anayeweza kutatua hali hii na kama atatokea basi huyo ni mlaghai tu kama kilivyo chama chake, Sehemu pekee wanakinondoni mnapoweza kutatulia hali hii ni kuongeza mbunge wa Upinzani pale Bungeni akawatete tu, Mtakuwa mashahidi, tangu uchaguzi upite ule uliomwingiza Mtulia kuwa Mbunge, mpaka leo yeye Mtulia hajawahi hata kurudi kuja kuwashukuru hata kwakikai cha ukoo tu, hii yote inatikana na katazo la ccm la mikutano ya kisasa, Katazo hilo ni batili kisheria kwamjibu wa sheria ya vyama vya siasa Tanzania.

Wananchi wa Kinondoni wengi hasa vijana wengi wenu mmekumbana na kesi za mirandaoni, na wengi wenu mna kesi mahakamani. Sisi UKAWA, tunaipinga sheria hiyo kwa nguvu zote, na ccm wanaipenda sheria hiyo kwa nguvu zao zote, kwakuwa wanaccm haiwagusi sheria hiyo hata wangetukana mitandaoni masaa 24/7. Vijana wa Upinzani wanaokumbana na sheria hii si kwamba wanatukana mtu au kufanya uhalifu kama vile wizi mtandaoni laa hasha, bali kosa letu kubwa ni kutoa maoni tofauti na chama cha mapinduzi na serikali yake, Maoni tofauti kwa ccm na serikali yake ni Matusi, utaletewa difenda zaidi ya 20 kisa post ya fb, twita au Jamiiforums, huku mpaka leo waliompiga Lissu hawajakamtwa mwezi wa tano sasa.

Ukimchagua Salumu Mwalimu yeye na wenzake wa upinzani pale Bungeni watatuwakilisha vizuri kuzuia miswada ya ajabu ajabu inayopitishwa kwa makofi na kugonga meza na Wabunge wa ccm wenye akili kama za Mtulia. Mkataeni kwa nguvu zote Mtlia na ccm yake, watawarudisha utumwani mkijichanganya tu mkawapa kura.

4. Kura yenu wanakinondini kwa Salumu Mwalimu liwe jibu tosha kwa ccm ilitoamua kununua Mbunge mliyemchagua 2015 kwa machozi na damu, kataani kwamba nyinyi wanakinondoni sio WAJINGA, bali wajinga ni CCM na Mtulia wao aliyeamua kuwasatili wanakinondoni. Kataeni kwa nguvu zote, na mtume ujumbe kwa njia ya kura kwamba wanakinondini hamkumtuma Mtulia kwenda kujiuza kama wajiuzavyo wale wenzetu wa kule kwa Macheni na uwanja wa fisi, bali mlimtuma mwakilishi wa wananchi wa Kinondoni kwaajili ya kuwakilisha matatizo yenu katika chombo kitakatifu cha maamuzi ambacho ni Bunge.

Hizi ni sehemu tu ya sababu kuu, lakini zipo sababu mamilioni ya kwa nini mmchague Salimu Mwakimu.... Kosa dogo tu mtakalofanya iwe kwakupiga kura kichama, ama kimahaba na kisha mkaipigia ccm, HATA MUNGU WENU ATAWALAANI KWA NGUVU ZOTE. Kwa bahati nzuri Mungu yupo nanyi katika MEMA, Hivyo hatawaacha MPOTEE.

CHAGUA SALUMU MWALIMU, CHAGUA UKAWA.

Na Yericko Nyerere

IMG-20180130-WA0166.jpg
 
CCM watachukua hilo jimbo la Kinondoni kwa muono wangu mimi binafsi.
 
Yericko nakupa pongezi la hili andiko lako, ila kitengo cha habari cha cdm kimelala usingizi mzito. Sioni wakitoa habari na ujumbe wa uchaguzi, dunia hii bila kutoa habari watu hawahamasiki. Kama hichi kitengo kitaendelea kulala ushindi unaouzungumzia itakuwa ni ndoto. Nimalizie, kuna tatizo na shida ya dhahiri ndani ya hicho kitengo.
 
Yericko nakupa pongezi la hili andiko lako, ila kitengo cha habari cha cdm kimelala usingizi mzito. Sioni wakitoa habari na ujumbe wa uchaguzi, dunia hii bila kutoa habari watu hawahamasiki. Kama hichi kitengo kitaendelea kulala ushindi unaouzungumzia itakuwa ni ndoto. Nimalizie, kuna tatizo na shida ya dhahiri ndani ya hicho kitengo.
Shukrani mkuu, Chadema ni watu na kila mtu apigane pale alipo kwa nguvu zake zote
 
Shukrani mkuu, Chadema ni watu na kila mtu apigane pale alipo kwa nguvu zake zote

Ni kweli ila hili halizuii idara maalum yenye wajibu ndani ya chama, kama tukiruhusu hivyo ni kubariki habari kupotoshwa na yoyote. Chombo rasmi cha habari ndani ya cdm kitekeleze wajibu wake, kisha sisi wengine tuwe na pukuanzia
 
Ni kweli ila hili halizuii idara maalum yenye wajibu ndani ya chama, kama tukiruhusu hivyo ni kubariki habari kupotoshwa na yoyote. Chombo rasmi cha habari ndani ya cdm kitekeleze wajibu wake, kisha sisi wengine tuwe na pukuanzia
Umesomeka mkuu
 
Back
Top Bottom