Kwanini wanaharakati wa Twitter ukiwa-challenge kidogo tu wanaku-block?

Kwanini wale wanaharakati wa Twitter hukiwachalenji kidogo tu kwenye hoja zao wanakutia ban,
Kwanini?

Kila wanachosema wao wanataka ukiunge mkono ukibishana nao tu tena kwa hoja wanakutia ban kwa nini?

Mimi sio mwanasiasa, na sio mwanachama wa chama chochote, huwa nasema kweli kwenye kweli, na kweli penye uongo.


Halafu ndio hao wanaharakati wanaotetea Uhuru wa kutoa maoni wakati wao hawapendi kusikia baadhi ya vitu flani fulani,

Wanajifanya ni magreat thinker wakati wako empty, Zero brain,

Ukiwajibu kwa fact wakiona kweli wamehelemewa wanakutia ban, usione, wala kureply kwenye post
zao shubamit.

Wanaharakati uchwara.

Nb:
Yule ndugu yao Kigogo aliyewasaliti aliniban kitambo kisa nimechallange , yule wakujiita Maltin M. M Nae kaniblock, yule mdada wao anaetukana tukana bila staa nae kaniblock,
Alafu wanajiita wanaharakati watetezi wa haki za binadamu.

Cc Zero IQ

Maria Sarungi alinipa kufuli hivyo hivyo,nilibaki kuduwaa,nilitegemea anipe ufafanuzi wa kina kwa kile alichokuwa anakiongelea,bila kujua sehemu aliyogusa walau nina ufahamu wa kutosha.Nilimuuliza kitu kidogo sana katika ile hoja,nikaambulia Kufuri.
 
Jielimishe: Twitter = mtandao wa kijamii ambao kimakosa umeuita "Tweeter" which instead means "mtu anayetwiti," na kile kinachopostiwa huitwa "tweet."

Kwenye mtandao huo kuna kitufe kinachomwezesha mtumiaji kumbloku mtu mwingine kwa sababu yoyote ile atakayoona inafaa. It is there for a reason, sio urembo.

Uzoefu unaonyesha kuwa "kila mfungwa hudai ameonewa, hakufanya kosa lililopelekea kufungwa." Likewise, kila mtu anayelimwa bloku Twitter hukimbilia kulalamika kuwa ameonewa.

Kukusaidia tu, mtu akikubloku kwenye mtandao wa kijamii sio kama amebloku mfumo wa hewa mwilini mwako. There’s more to life than Twitter. Move on with your life...

Sasa kama ni hivyo,huo uhuru wa kutoa maoni mnaoupigia kelele ni wa nini sasa,kama nyinyi Wanaharakati hampendi kusikia mawazo kinzani? Mnaita wengine Dikteta wakati huo huo na nyinyi mna udikteta kwenye anga zenu.Nilidhani una tweet ili upate maoni ya watu,vinginevyo hakukuwa na haja kutuletea mawazo yako kama hutaki kusikia ya wengine.Pale siyo Kanisani kwamba tunasikiliza tu mahubiri na hatupaswi kuhoji au kujadili.
 
Back
Top Bottom