Kwanini wanafunzi wengi wanafeli?unajua kunanini nyuma ya pazia?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wanafunzi wengi wanafeli?unajua kunanini nyuma ya pazia??

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by K-killer, Feb 10, 2012.

 1. K-killer

  K-killer Senior Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakuu,imekua ni jambo la ajabu sana kua unaweza kuona baadhi ya wanafunzi huwa wanafaulu karibu mihula yote wanayokuaga darasani na vidato mbali mbali lakini inakuaga vigumu sana wanafunzi hawa kufaulu form4 au form6 hata kama wanaakili au hufaulu kwa wastani basi wakifika form4 au form6 unakuta wanapata division4 au zero kabisa,wakati mitiani mingine yakuwapima unakuta wanaweza pata division1 au division2.

  Swali linakuja,Je inawezekana kweli mwanafunzi awe anafaulu hiyo mihula minginge lakini akifika finals za form4 au form6 anafeli kabisa kama hana akili?au kuna hujumu flani inafanyika na watendaji wa serikali dhidi ya wanafunzi?je kwanini kama ni kweli hawa watendaji wa serikali wanaodili na mitihani ya hawa wanafunzi huwa wanawafanyia hujuma wanafunzi na kuwafelisha mitihani hii ya form4 au form6?inawezekana kuwa ni kwasababu serikali inajaribu kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofaulu ili kukwepa kuongezeka kwa garama wanazotumia kuwapa wanafunzi walofaulu kama hawa wanafunzi wa vyuo ambao kutwa hata wao zile ela wanazopewa haziwatoshelezi na kila siku wanaleta migomo vyuoni.

  Tukiangalia kwa upana zaidi tunaona kwenye upande wa elimu serikali haijatilia mkazo katika swala la elimu,imekua haionyeshi jitihada kujitahidi wananchi wetu watanzania kuondokana na ujinga through education,lakini insted tumeshuhudia serikali yetu ikikandamiza sekta ya elimu bila kuisaidia kama inavyotakiwa kwa kujenga majengo mazuri yaa shule,kutoa vifaa na maabara ya kiwango cha juu shule ziwe na vifaa vyakutosha kukidhi na kua katika viwango vinavyoitajika.Je nitakua nakosea kusema serikali inafanya ivi makusudi ili tubaki kuwa wajinga na tusiendelee kujua lolote linaloendelea nchini kwa kutunyima taaluma ya msingi ya elimu?wanataka tubaki kuwa wajinga kila wasemalo tuone sawa kwakua hatujasoma?je mamilioni ya pesa wanayotumia unnecessarly kwa mapati yao na kadhalika,leo hii wangetumia hizo fedha kwa kujenga shule si tungekua na shule nyingi na karibu ya 80% wangekua wamefuta ujinga na wamesoma.Hii ni wazi serikali inapenda tuzidi kuwa wajinga na kutu discourage tujione wajinga hatuna akili,ndo maana wengi wanaofeli hata form4 au form6 wanaishia mtaani kama wazee wao hawana uwezo..Nawashilisha hoja,tuchanganue jamani ningependa kujua zaidi pia nanyi wenye michango yenu.Ni mtazamo tuu.Nawakilisha
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Walimu wanasema sababu kubwa ni mgomo wao baridi kwani kilio chao hakisikilinzi na serikali.
  Wanafunzi nao wanasema walimu hawafundishi vema mashuleni.
  Uswahilini wanasema watoto wengi hawana tena desturi ya kujisomea.
  Wazazi nao wanasema wako busy sana na shughuli zao kufuatilia cont. assessment za mitoto yao.

  Wengine wanasema wanafunzi wengi siku hizi wanapenda shortcut, like kuwa wasanii, kuwa masharobaro na kuandika mashairi kwa exam room.
   
Loading...