Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Labda kwa sasa hivi. Miaka hiyo wale waliosoma sekondari za ufundi masomo kama History, Geography na Biology walikuwa hawasomi/haafanyii mtihani form four. Nafikiri hata kwa wale wa michepuo ya biashara kuna baadhi ya hayo mosomo unayoita ya "msingi" hayakuwa ya msingi kwao.

But nakiri kuwa huenda nimepitwa na wakati sana.....na labda mambo yameshabadirika kwa sasa.
Ni kweli, Binafsi pale Ifunda masomo hayo niliyaacha tukiwa form two.
 
1. Huku mwanzoni unapata msingi tu wa masomo yote. Hivyo kupata msingi mzuri ndiyo kunafanya mtu awe na uelewa mzuri kwenye michepuo yake
Msingi unaanzia wapi na kuishia wapi? Kama msingi hauishii darasa la saba kwanini tuamini kuwa huo msingi (Phyisics na Chemistry) unaishia kidato cha pili? Kwanini wote wasisome hayo masomo mawili mpaka kidato cha nne?...
 
Mawazo mazuri sana, japo tafakari hili:

Mwanafunzi anasoma masomo yote hadi kidato cha pili na kuruhusiwa kuchagua michepuo anapoingia Kidato cha tatu, hasa kutokana na ukomavu wa kifikra katika huo umri(wastani wa miaka14-16)

Nataka pia nikuaminishe kuwa huu umri umefanyiwa tafiti kwamba ni mda maalumu wa kijana kuweza kujua anapenda nini kwa maana ya kwamba anaweza kufanya nini -huku akishauriana na academic mentors wake

Huu umri ni rahisi kujua mtoto ni talented katika eneo lipi, na chini ya umri huo mtoto huwa anapenda kila kitu akidhani anaweza kufanya kila kitu. Kupenda profession haina uhusiano wa moja kwa moja kwamba unaweza kuisoma

Hoja hii itakuwa na nguvu kama zitakuwepo tafiti kuonyesha kwamba kutokana na ukuaji wa teknolojia ya upashanaji habari, ama mabadiliko ya ukomavu kiuelewa, mtoto akiwa primary std 7 anakuwa amekomaa vya kutosha kuweza kuchepua.
 
Mwanafunzi anasoma masomo yote hadi kidato cha pili na kuruhusiwa kuchagua michepuo anapoingia Kidato cha tatu, hasa kutokana na ukomavu wa kifikra katika huo umri(wastani wa miaka14-16)
Mkuu, ni ukomavu wa kifikra pekee au pamoja na ufaulu wa kidato cha pili. Mwanafunzi anaweza akapata D katika somo la chemistry kisha akapata F katika physics kidato cha pili alafu akakubaliwa kusoma mchepuo wa sayansi hata kama akili yake imependa? Seriously?...
 
Nataka pia nikuaminishe kuwa huu umri umefanyiwa tafiti kwamba ni mda maalumu wa kijana kuweza kujua anapenda nini kwa maana ya kwamba anaweza kufanya nini -huku akishauriana na academic mentors wake
Anapenda nini na anamudu nini hayo ni mambo mawili tofauti sana mkuu. Kumbuka kama suala ni kupevuka kwa akili, contents za masomo ya darala la saba hayawezi kufanana na yale ya kidato cha pili hata kama yote yangekuwa yanafundishwa kwa lugha moja mkuu.

Hesabu za kidato cha pili zingekuwa zinafundishwa kwa mwanafunzi wa darasa la sita au saba, hapo sasa suala la ukomavu wa akili ndio lingeweza kuchukua nafasi, lakini mitihani hii hutungwa kwa kuzingatia ukomavu wa akili ya mwanafunzi kwa umri huo...
 
Huu umri ni rahisi kujua mtoto ni talented katika eneo lipi, na chini ya umri huo mtoto huwa anapenda kila kitu akidhani anaweza kufanya kila kitu. Kupenda profession haina uhusiano wa moja kwa moja kwamba unaweza kuisoma
Mkuu, mimi ninadhani mbinu zinazotumika katika kutambua kipaji cha mtoto kwa huku Afrika zipo outdated sana tofauti na wenzetu wazungu...
 
Hoja hii itakuwa na nguvu kama zitakuwepo tafiti kuonyesha kwamba kutokana na ukuaji wa teknolojia ya upashanaji habari, ama mabadiliko ya ukomavu kiuelewa, mtoto akiwa primary std 7 anakuwa amekomaa vya kutosha kuweza kuchepua.
Sawa mkuu kwa maana wataalam hupendi kusema "tafiti hupingwa kwa tafiti" na sio maneno matupu (Bare Words)
 
Kuchagua matoke kulingana na ufaulu ni ushamba.
Kote duniani kwa walikoendelea watoto hawachagui masomo ya kuendelea nayo kwa kulingana na ufaulu bali kwa masomo mtoto anayopenda kwa dhati kuyasomea.
Si sahihi mwanafunzi aweza kuwa influenced na mwalimu akachukua somo asiloweza tu kwa sababu ana mwalimu inspiring!! Uwezo wa masomo ndio unatakiwa kuamua

Mfano mtu aweza kuwa indpired na mwalimu wa muziki mwalimu Diamond akawa inspired kweli ikija performance zero!!!
 
Si sahihi mwanafunzi aweza kuwa influenced na mwalimu akachukua somo asiloweza tu kwa sababu ana mwalimu inspiring!! Uwezo wa masomo ndio unatakiwa kuamua
Somo kama huliwezi huliwezi tu hata akiletwa Mike Tyson kuja kufundisha boxing kamwe hutakuja kuwa bondia mzuri...
 
Uwezo wa masomo unatokana na nini?

Back
Top Bottom