Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Karibia wanaCHADEMA wote unaweza kusema ni watoto wa mama mmoja na kuna kitu kinawaunganisha, nacho ni ubishi.
Kuna hili jambo la Uchaguzi, wanaCHADEMA wote husema kwamba wao hushinda uchaguzi na kwamba huibiwa kura, na mfano mzuri ni Uchaguzi uliopita, lkn kwa nini mahesabu hayaendani na madai yao ya kuibiwa kura?
Kwa mfano CHADEMA walipata Wabunge 30 tu wakati CCM walipata Wabunge zaidi ya 150 na wana chadema wote huyakubali matokeo ya Ubunge lkn husema kwamba walishinda kura za Urais na kwamba waliibiwa, sasa hili mtu mwenye akili anaweza kulielezea vipi? Iweje Mtanzania asiwaamini CHADEMA kwenye kuongoza Bunge halafu akawaamini kwenye kuongoza Nchi?
Ni kwa nini CHADEMA wanakuwa wabishi namna hii na hawataki kuukubali ukweli kwamba bado hawajaweza kukubalika na Watanzania kuongoza hii nchi? Kuishi kwa uongo hakuwasaidii kwani mnawafanya wanachama wenu waamini jambo ambalo halipo, na hivyo kupunguza nafasi huko mbele ya kujiboresha.
Waambieni ukweli watu wenu kwamba, tumeshindwa uchaguzi kwa sababu kura zetu hazikutosha lakini kwa kuongeza juhudi na maarifa tuna uwezo mkubwa wa kuongeza kura zetu chaguzi zijazo, huu ndiyo ukweli na wala siyo udhaifu kama mnavyofikiri.