JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,442
- 54,993
..Tundu Lissu amekuwepo machoni mwa jamii tangu akiwa kijana mdogo toka udsm miaka ya 90.
..alianza kujulikana ktk awamu ya Raisi Mkapa. Na harakati zake kutetea haki, misingi ya katiba, na utawala wa sheria, hapa nchini hazijakoma au kupungua kasi.
..Wakati wote huo sijawahi kusikia wana-ccm ktk ujumla wao wakimpongeza au kumshukuru Tundu Lissu kwa jambo lolote lile.
..Yapo mambo ambayo Tundu Lissu huyasemea na serekali au ccm huyapinga. Na propaganda kali sana hufanyika kuonyesha kuwa Tundu Lissu ni mtu mbaya, hatari, au hata mjinga.
..Lakini muda ukipita chama na serekali huyachukua mambo hayohayo na kuyatekeleza lakini hatujapata kusikia wakimshukuru au kumpongeza Tundu Lissu kwa kuwafungulia njia.
..Labda niwakumbushe jambo moja ambalo wengi limewapita kimya-kimya. Ni suala la utaratibu wa MICHANGO isiyikoma lililokuwa limeshika kasi wakati wa utawala wa JK.
..Tundu Lissu alisimama kidete kupinga michango hiyo na haswa kama kulikuwa hakuna UTARATIBU mzuri ktk makusanyo na matumizi.
..Kama mtakumbuka CCM walimuandama kweli kweli wakidai Tundu Lissu ni mpinga maendeleo. Leo hii Raisi Magufuli amechukua wazo ambalo Lissu alikuwa akilipigania kwa muda mrefu na kwa gharama ya shutuma na kejeli za kila aina.
..Ni jambo jema kwamba wana ccm kwa moyo mmoja wameunga mkono kitendo cha Raisi kuiga mawazo ya Tundu Lissu.
..Lakini inanishangaza hakuna mwana-ccm aliyekumbuka kumshukuru Lissu kwa kufungua njia kwa Raisi Magufuli kufuta michango ya hovyo-hovyo hapa nchini.
..Ni kweli Tundu Lissu ana mapungufu yake kama binadamu yeyote yule.
..Lakini naamini kwa kiwango kikubwa, na cha kupigiwa mfano ametumia elimu, muda, na nguvu zake, kutetea HAKI kwa nia ya kuboresha maisha ya kila Mtanzania.
..MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
Cc MTAZAMO, Mag3