Kwanini wana-ccm[raisi,spika] wanapinga kila jambo la Tundu Lissu? Kwanini hawamsifii hata kwa machache? Je hana jema alilofanya kwa Tz?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,215
2,000
..Tundu Lissu amekuwepo machoni mwa jamii tangu akiwa kijana mdogo toka udsm miaka ya 90.

..alianza kujulikana ktk awamu ya Raisi Mkapa. Na harakati zake kutetea haki, misingi ya katiba, na utawala wa sheria, hapa nchini hazijakoma au kupungua kasi.

..Wakati wote huo sijawahi kusikia wana-ccm ktk ujumla wao wakimpongeza au kumshukuru Tundu Lissu kwa jambo lolote lile.

..Yapo mambo ambayo Tundu Lissu huyasemea na serekali au ccm huyapinga. Na propaganda kali sana hufanyika kuonyesha kuwa Tundu Lissu ni mtu mbaya, hatari, au hata mjinga.

..Lakini muda ukipita chama na serekali huyachukua mambo hayohayo na kuyatekeleza lakini hatujapata kusikia wakimshukuru au kumpongeza Tundu Lissu kwa kuwafungulia njia.

..Labda niwakumbushe jambo moja ambalo wengi limewapita kimya-kimya. Ni suala la utaratibu wa MICHANGO isiyikoma lililokuwa limeshika kasi wakati wa utawala wa JK.

..Tundu Lissu alisimama kidete kupinga michango hiyo na haswa kama kulikuwa hakuna UTARATIBU mzuri ktk makusanyo na matumizi.

..Kama mtakumbuka CCM walimuandama kweli kweli wakidai Tundu Lissu ni mpinga maendeleo. Leo hii Raisi Magufuli amechukua wazo ambalo Lissu alikuwa akilipigania kwa muda mrefu na kwa gharama ya shutuma na kejeli za kila aina.

..Ni jambo jema kwamba wana ccm kwa moyo mmoja wameunga mkono kitendo cha Raisi kuiga mawazo ya Tundu Lissu.

..Lakini inanishangaza hakuna mwana-ccm aliyekumbuka kumshukuru Lissu kwa kufungua njia kwa Raisi Magufuli kufuta michango ya hovyo-hovyo hapa nchini.

..Ni kweli Tundu Lissu ana mapungufu yake kama binadamu yeyote yule.

..Lakini naamini kwa kiwango kikubwa, na cha kupigiwa mfano ametumia elimu, muda, na nguvu zake, kutetea HAKI kwa nia ya kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

..MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.

Cc MTAZAMO, Mag3
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Huwa nawashangaa sana hawa watu.Tena ni bora hata wapinzani sometimes hupongeza ila jiulize ni lini wao,hasa JPM, aliwahia sifia mazuri ya wapinzani.

Hawa watu waondoke tu na Mungu awezeshe kuondoka kwao.

Enough is enough.

Watoke tu.
 

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
5,389
2,000
Huwa nawashangaa sana hawa watu.Tena ni bora hata wapinzani sometimes hupongeza ila jiulize ni lini wao,hasa JPM, aliwahia sifia mazuri ya wapinzani.

Hawa watu waondoke tu na Mungu awezeshe kuondoka kwao.

Enough is enough.

Watoke tu.
kusifia si mpaka aongee,kuwaweka Waitara,Katambi,kafulila Kwny timu yake ni kukubali Wapinzani achana na wachungaji FEki wakina msigwa
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,698
2,000
LIssu hawezi kusifiwa na CCM kwani anajua kucheza na CCM. Wanadai hana madhara lakini kila siku duwa na mipango yao ni kutaka kumuondoa Lissu!
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,698
2,000
kusifia si mpaka aongee...
Sijui nyie watu akili zenu mmezifungia kwenye kibindo gani? Kusifu kunatokana na neno sifa ambako ni lazima sifa zitolewe ama kwa maandishi ama kwa mdomo. Yaani kuteua hao watapia hatima ndiyo unaona amesefia?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,215
2,000
kusifia si mpaka aongee,kuwaweka Waitara,Katambi,kafulila Kwny timu yake ni kukubali Wapinzani achana na wachungaji FEki wakina msigwa

..lets be a bit more serious.

..kwa hiyo wapinzani kuwachukua Lowassa, na Nyalandu, ndiyo wamesifia ccm?

..swali langu liko palepale, naomba unijibu.
 

J U G A N I A

JF-Expert Member
May 30, 2015
651
250
Acha uongo wewe, Rais hajawahi kuwasifia wabunge wa upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
sijui unauliza swali au unaeleza? kama unaeleza ni kwamba rais amewahi kusifia wapinzani...David Kafulila amewahi kusifiwa na kupewa mkono wa pongezi na mhe. rais. Kama sikosei kati ya marais wote ni JPM peke yake ndiye amewahi kusifia wapinzani pale wanapofanya mazuri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom