Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapouawa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe pia huuana?

lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
992
904
Wa salaam wanajamvi.

Swali langu ni hili: Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapo kojolewa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe hunyeana?

Hivi punde kumetokea mauaji ya kijana mweusi huko marekani yaliyofanywa na afisa wa polisi (ambaye ni mzungu) . Na kila mtu analijua hilo. Ila cha kushangaza zaidi ni pale tunaona watu wengi weusi kutoka pande mbalimbali za ulimwengu wakilaani tukio hilo.

Mbona haya manung'uniko hayashiki hatamu pale wamarekani weusi wanapo uana wao kwa wao.?

Hivi mnajua kuwa vifo vinavyotokana na mauaji ya watu weusi(wenyewe kwa wenyewe kuchomana "Visu" & "Risasi") ni vingi kuliko vile vinavyotokana na mauaji na watu weupe(wazungu kuua watu weusiy)?

Kwa nini kifo kinacho sababishwa na mzungu kionekane kina mzizi wa "Ubaguzi wa Rangi".?

Ninawaomba wamarekani" weusi" wapunguze kuendekenda ubaguzi wa rangi. Waamini kuwa kufa kwa mmarekani mweusi hakusababishwi na ubaguzi wa watu "weupe" bali ni mitazamo yao isiyo sahihi, pia wazingatie maisha ya watu weusi yaliyoangamia kutokana na watu weusi.

Kama kweli wanamaanisha wanaposema #BlackLivesMatter, basi waniksikie nisemavyo, huenda wakanielewa kabla hakuja kuchwa.

YMCMB Headquarters.
 
Hivyo vifo vinavyolalamikiwa ni vile vinavyotekelezwa na law enforcers kwa watu weusi. Hayo ya wao kutinduana visu mitaani huwezi kufananisha. Wana visa na visasi vyao huko mtaani na huwezi kuzuia. Law enforcer anatakiwa kulinda usalama wa kila mtu. Unaweza kueleza kwa wazi sababu ya kumwua kwa risasi mtu ambaye askari wawaili wamemdhibiti tena wamemlaza chini? Alikuwa tishio kiasi gani kwao? Heri wa huku wanatuambia majambazi yalikuwa yanajaribu kutoroka huku yakirusha risasi hata kama yanakuwa yamefungwa pingu.
 
Nadhani sina la kukupinga kwa unayo yasema. Nimaanishacho ni kuwa :- waache unafiki.

Unajua, watu weusi(Marekani) kujifanya kuthamini maisha ya mtu mweusi mwingine pale anapo uawa na mtu mweupe ni unafiki wa hali ya juu. Ikiwa wao kwa wao huuana kwa wingi mno.

Kwa nini hawathamini maisha yao, hata wawe wanauana kwa wingi, achilia mbali suala la kuuawa na law enforcers.

Waanze kwa kupaza sauti mauaji ya wao kwa wao nami ndipo nita waunga mkono wanapo paza sauti za mauaji yatokanayo na law enforcers.
 
Kimsingi haya ni mambo ya watu weusi wa marekani sidhani kama yanatuhusu sana. Wao wanajuana wenyewe sisi tunasoma tu kwenye vyombo vya habari pengine vyenye mlengo wa kupendelea upande mmoja au mwingine. Usipende kutoa matamko kwenye mambo ya watu usiyoyajua
 
Wa salaam wanajamvi.

Swali langu ni hili: Kwanini wamarekani weusi hulalamika wanapo kojolewa na wamarekani weupe, Ikiwa wao wenyewe hunyeana?

Hivi punde kumetokea mauaji ya kijana mweusi huko marekani yaliyofanywa na afisa wa polisi (ambaye ni mzungu) . Na kila mtu analijua hilo. Ila cha kushangaza zaidi ni pale tunaona watu wengi weusi kutoka pande mbalimbali za ulimwengu wakilaani tukio hilo.

Mbona haya manung'uniko hayashiki hatamu pale wamarekani weusi wanapo uana wao kwa wao.?

Hivi mnajua kuwa vifo vinavyotokana na mauaji ya watu weusi(wenyewe kwa wenyewe kuchomana "Visu" & "Risasi") ni vingi kuliko vile vinavyotokana na mauaji na watu weupe(wazungu kuua watu weusiy)?

Kwa nini kifo kinacho sababishwa na mzungu kionekane kina mzizi wa "Ubaguzi wa Rangi".?

Ninawaomba wamarekani" weusi" wapunguze kuendekenda ubaguzi wa rangi. Waamini kuwa kufa kwa mmarekani mweusi hakusababishwi na ubaguzi wa watu "weupe" bali ni mitazamo yao isiyo sahihi, pia wazingatie maisha ya watu weusi yaliyoangamia kutokana na watu weusi.

Kama kweli wanamaanisha wanaposema #BlackLivesMatter, basi waniksikie nisemavyo, huenda wakanielewa kabla hakuja kuchwa.

YMCMB Headquarters.
Umesahau kwamba hao polisi kazi yao si kuua mtu, wanatakiwa kuwa-protect, haijalishi kama wee ni mweusi au mweupe. Kama polisi anashindwa kuku protect what should you do? unachukua matters in your own hands.
 
Hauna adabu wala heshima kwa mtu mweusi. Umemsikiliza Pres Obama alichoongea? Usiwe jinga kutetea mauaji ya kinyama kabisa wanayofanyiwa watu weusi. Acha kuropoka dada.....huelewi uchungu watu wanaopitia.
 
Ni sawa kulalamika na kupaza sauti pale walipo ona mweusi mwenzao amefanyiwa yasiyo haki, ila naona kama hao hao wamarekani weusi wanatumia nguvu kubwa kupaza sauti kwenye mauaji yanayo husisha "interracial" zaidi kuliko yale mauaji ambayo wanafanyiana wao kwa wao (ambayo ni mengi zaidi).
 
Hauna adabu wala heshima kwa mtu mweusi. Umemsikiliza Pres Obama alichoongea? Usiwe jinga kutetea mauaji ya kinyama kabisa wanayofanyiwa watu weusi. Acha kuropoka dada.....huelewi uchungu watu wanaopitia.
Mawani yako yanaona unyama wanao "fanyiwa" wamarekani weusi, ila yanashindwa kuona unyama wanao "fanyiana" wamarekani weusi.
 
Hivyo vifo vinavyolalamikiwa ni vile vinavyotekelezwa na law enforcers kwa watu weusi. Hayo ya wao kutinduana visu mitaani huwezi kufananisha. Wana visa na visasi vyao huko mtaani na huwezi kuzuia. Law enforcer anatakiwa kulinda usalama wa kila mtu. Unaweza kueleza kwa wazi sababu ya kumwua kwa risasi mtu ambaye askari wawaili wamemdhibiti tena wamemlaza chini? Alikuwa tishio kiasi gani kwao? Heri wa huku wanatuambia majambazi yalikuwa yanajaribu kutoroka huku yakirusha risasi hata kama yanakuwa yamefungwa pingu.
Waambie manake ni kazi kuelezea jambo la wazi
 
Mawani yako yanaona unyama wanao "fanyiwa" wamarekani weusi, ila yanashindwa kuona unyama wanao "fanyiana" wamarekani weusi.

Usiwe jinga.....nani kakwambi weusi kwa weusi wakiuana watu hawaongei? Logic yako mbona inatia shaka.....unawaza nini? Kazi ya police ni kulinda raia si kuuwa. Uliangalia video ya wauaji ya jana? Uliwaza nini police anamuua yule mwanamume mbele ya binti yake mdogo tena bila sababu?
 
Wakati mwingine huwa siwaelewi binadamu, eti kwakuwa weusi wanauana wao kwa wao katika mambo yao, mantiki inatwambia jamii ikiwamo polisi wajitazame upya ili kukomesha mauaji hayo badala yake wapuuzi wanajenga hoja ya kuhalalisha mauaji ya wasio na hatia, kwakuwa weusi wanauana solution waueni wote
 
Usiwe jinga.....nani kakwambi weusi kwa weusi wakiuana watu hawaongei? Logic yako mbona inatia shaka.....unawaza nini? Kazi ya police ni kulinda raia si kuuwa. Uliangalia video ya wauaji ya jana? Uliwaza nini police anamuua yule mwanamume mbele ya binti yake mdogo tena bila sababu?
Mkuu usipandishe jazba! Usije kushindwa kucheka na watoto wako.

Hivi ushawahi kuona mitandao ya jamii ikiwa viral katika mithili hii haswa pale hawa wamarekani weusi wauanapo wao kwa wao...?

Umewahi labda kusikia Msanii maarufu huko marekani akikemea mauaji wanayofanyiana watu weusi...?

0na alichokisema BEYONCE....
0na alichokiongea CHRIS BROWN......

niaminicho ni kwamba wamarekani weusi hawapendi dharau ya kuonekana wanauawa na wamarekani weupe, kwao ni bora wauane wao kwa wao ili siku ipite.
 
Nilivyomuelewa Snoop na followers wake kwenye wall yake ni kwamba wanataka haki iwe inatendeka.

Mfano black on black crimes wauaji hufikishwa kortini lakini matukio haya ya juzi na yenye mfanano huo hakuna kinachofanyika kisa mzungu kaua mweusi.

Kingine,ikitokea mweusi akabambwa kwenye tukio hata kama asipokuwa na silaha au aki-surrender atatandikwa shaba tu tofauti na wanavyowaweka chini ya ulinzi weupe wenzao.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom