Kwanini waliosoma UDSM wanapenda kuweka “UDSM alumnus/alumna” kwenye bio za social media?

hahahahaaaaaa, UDSM bhana lazima nirudi tena kuifaidi mlimani campus aise. I love campus life.
Yaani japo kuwa nilisoma mbali sana na huko na sasa mvii zinaninyemelea, lakini maisha yangu yote ya furaha ni kumbukumbu ya campus life
Campus life memory ya chuo kikuu katika maisha yangu ina furaha yake kulingana na kupata mtoto wa kwanza.
 
KCMC ndio nini mkuu, kwani ww hukutamani kwenda MUHAS, mm najua ulikwenda second hand university kwasababu marks zako hazikutosha. All in all hata MUHAS ilikua part ya UDSM na ndio maana walivyo jitenga wanafunzi wakipindi hicho waliomba kupewa vyeti vya UDSM
Muhas ya nn kama unamudu ada ya kcmc, me nimeapply muhas, kcmc,mchas na udom, kote ninauhakika wa kupata md Ila sipendelei muhas kwasababu ya stori nazopigiwa na baadhi ya wanaosoma huko, pia humuhumu jf, muhas nasikia watu wanasoma kwa stress, sup za njenje mitihani migumu isiyofuata medical criteria...
 
Kwasababu ni vyuo bora kwa hapa nchini to be proud of .

Hiyo sifa ndio imewafanya watu waende udsm na division 1 zao wakasomee digrii ambazo hazina soko.

Baadae wanajuta wanaona bora wangeenda ifm ama vyuo vya kati kusoma kozi zenye soko mwisho wake wamebaki mitaani wanajuta

Mfano mtu mwenye digrii ya accounts ya TIA ama IFM ana fursa kubwa kuliko mtu mwenye digrii ya political science ya udsm
 
Hata sisi tuliosoma Chuo Cha Nyuki Tabora tunakubali kuwa UDSM ni chuo bora zaidi hapa nchini. Ni ndoto ya karibu kila mtanzania kusoma pale. Kinachosababisha sisi wengine tujikute VETA ni ukosefu wa matokeo mazuri form six. Kupata nafasi baadhi ya kozi UDSM ni kimbembe. Mnaosema cha muhimu hela ni kujifariji tu ila hela bila degree ya UDSM ni mboga bila chumvi. Kama hukupita UDSM ukiwa undergraduate basi pambana ukapate hata postgraduate diploma kuondoa nuksi kwenye haya maisha.
 
Comment yako ingekuwa na ka uzuri Fulani, Ila nilipoona "MamaSamia2025, nimeshakuona bwege!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom