Kwanini walioshindwa chaguzi ndo hupewa madaraka ya juu CCM?

mjuaji

Senior Member
Apr 6, 2012
166
22
Msekwa baada ya kushindwa uspika akawa makamu wa m/kiti bara.Nape aliposhindwa kura za maoni ubunge akawa mwenezi Taifa.Mangula aliposhindwa mwenyekiti Iringa kapewa makamu CCM bara.Rose Migiro aliposhindwa ukatibu UN kalamba cheo CCM.Bendera Joel kapewa ukuu wa mkoa
 
CCM haindeshwi kufuatana na umma unavyotaka,bali hufuata uswahiba ktk ufisadi,mtoa rushwa,kulipana fadhila!
 
... wanapovua gamba wangeanza na hawa failures kwanza kuwang'oa. mie mtu ambaye hajachaguliwa na watu kwangu sio kiongozi "Leader" bali ni manager tuu. kuwa meneja ni rahisi kwa mtu yeyote aliyesoma na ana akili lakin ni tatizo kuubwa kama ni kilaza kama Nape(sumba school failure)
 
Slaa aliposhindwa upadri kanisani akapewa ukatibu mkuu wa chadema taifa na kuteuliwa kugombea urais au?
 
Kwa sababu wana hasira sana na watajitoa kwenye chama kama wasipo pewa madaraka!

Mfano ni Nnauye Jr aliposhindwa na yule mama kwenye kura za maoni alipanic sana hivyo waliona wamtulize na ukatibu weneze! Lasivyo ccj ingeshapata usajili muda mrefu!
 
Last edited by a moderator:
Slaa aliposhindwa upadri kanisani akapewa ukatibu mkuu wa chadema taifa na kuteuliwa kugombea urais au?
Ritz azidi kupokea wafuasi, mwingine huyu! CCM kweli dampo.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ndio dalili tosha ya kujua kuwa CCM inawenyewe kwani unapeana uraji. Ndio maana unaona wameona hakuna watu wengine wenyeupeo wa kufikiria zaidi ya wazee MANGULA na KINANA. kwa harakaharaka na hakili nyepesi nyepesi unaweza kufikiri Watanzania wanashida ya sura za watu ndani ya CCM. Watanzania shida yao na ugonvi wao na CCM ni mfumo fisadi na Uswahiba ndani ya Ufamilialization uliopo kwa sasa. Kamwe CCM wasitegemee lolote kwa kubadili watu ndani ya chama bali wajikite kujichunguza ndani ya mfumo wao mbovu. Waliofail kwenye chaguzi za CCM wanapewa madaraka makubwa kwa sababu wanakuwa wamepewa ahadi za nyazifa. Kinachokuja kutumalza wapigakura ni pale aliyekataliwa anapokuja kuwa mkuu wa mkoa au wa wilaya kuwaongoza waliomkataa. Hapo utakuta kiongozi kama huyo hana mapenzi na anaowaongoza na anajua cheo hicho ni cha uswahiba.....
 
ndo siasa zilivyo hata wewe ukiwa mwanasiasa basi utapata nafasi kwa wanasiasa wenzako, mh. SLAA aliponyimwa kugombea ubunge kupitia ccm, akahamia CDM na kuteuliwa kugombea na akashinda, mkewe bi ROSE KAMILI aligombea nafasi ya ubunge ndani ya ccm,aliposhindwa akahamia CDM, na kuteuliwa kugombea akashindwa, mh shibuda alikataliwa ccm ,akaibuka cdm akashinda, MH Ntagazwa alipobwagwa ccm ,akahamia CDM ,mlolongo ni mrefu hizo ndo tabia za wanasiasa, maana hata wagombea walioshindwa ktk majimbo ndo waliopewa upendeleo wa nafasi za upendeleo CDM kwa wanawake.
 
Back
Top Bottom