Kwanini walio nje huwawia ngumu kurudi nyumbani? Tuwasaidiaje?

Kwa nini unafikiri kila mtu anataka maendeleo? Watu wengine washamua maisha haya mafupi maendeleo is overrated, wanajirusha tu, doing them. Kwa nini utake ku force principles zako za kumforce kila mtu atake maendeleo?

Tunarudi kule kule, mtu mzima hazuiwi kuvuta sigara chumbani kwake, hata kama sigara inaweza kusababisha kansa.

kiranga, I believe you are not one of them
 
Mkuu Luten
Umetafuta kesi kwa hiari yako mwenyewe, wakaa ughaibuni watakugawana vipande vipande ingawa hoja zako nyingi zina ukweli isipokuwa kwa wachache tu ambao wamepata kazi zinazolipa vizuri makaratasi yametulia na wana mchango mkubwa kwa familia zao nyumbani na kwa pato la taifa kwa fedha za kigeni na kwa hiyo hizo sababu zako haziwagusi kwa namna yoyote ila ni watu wameamua kuchapa kazi manake zinalipa.
Makondo

Najua kweli nimegusa wengi lakini kuna wakati lazima tuambiane ukweli hatuwezi kuendelea kwa vijana wote kuzamia nje lazima nchi au individuals tutafute namna ya ku wamotivate hawa warudi, zaidi ya kujidanganya kuwa vijana walio nje wanasaidia nyumbani kuliko vijana walio nyumbani.

Mimi wakati natafuta nauli ya kwenda nje(kwa sababu yeyote ile) nauli niliomba kwa mjomba, kwanza akaniambia hawezi kunipa nauli za kwenda kujitesa mwenyewe nje bora anipe nifanyie biashara, sababu alizozitoa ni kuwa anaijua ulaya ina mipango yake sisi tunaoenda huko tunaonekana kama mzigo kwao kwa hiyo wanatu treat immigrants kama second hand au scraper wanakutumia to the maximum kiasi kwamba hela utakayopata kwa mshahara karibu nusu yake utaiacha kwenye kodi na nusu iliyobaki utalazimika kulipa acommodations, chakula na mahitaji mengine at the end of the day hautabaki na kitu (savings) ndiyo maana kama mtu huna elimu maana yake huna kazi nzuri humchukua muda mrefu sana kuji establish huko. Baada ya maelezo hayo nilimuona uncle kama mzushi tu nikamng'ang'ania hadi akanipanauli, nilikuja kuamini maneno yake baada ya miezi sita tu ya mwanzo.
 
Unawezatujuza ulikaa nchi gani?
 
Sasa kuliko kuwasaidia walioko nnje ambao wameipunguzia serikali mzigo wa kuwabeba si bora kulelekeza nguvu kusaidia walioamua kubakii tanzania(wazalendo) ilhali wanaishi kama wako jehanamu?. Nina uhakika watz wanaoteseka ughaibuni ni wachache ukilinganisha na walioko hapa bongo.

Jiulize ni wasomi wangapi wamezagaa bongo hawana mbele wala nyuma?

Tuache mawazo ya ki jamaa. Ukiona green pasture nchi fulani kimbia bongo lasivyo utaishi Tanzania kwa kutegemea rushwa na magendo manake ndio mbinu kuu za "kutoka" bongo.
 
Makondo

Najua kweli nimegusa wengi lakini kuna wakati lazima tuambiane ukweli hatuwezi kuendelea kwa vijana wote kuzamia nje lazima nchi au individuals tutafute namna ya ku wamotivate hawa warudi, zaidi ya kujidanganya kuwa vijana walio nje wanasaidia nyumbani kuliko vijana walio nyumbani.

Mimi wakati natafuta nauli ya kwenda nje(kwa sababu yeyote ile) nauli niliomba kwa mjomba, kwanza akaniambia hawezi kunipa nauli za kwenda kujitesa mwenyewe nje bora anipe nifanyie biashara, sababu alizozitoa ni kuwa anaijua ulaya ina mipango yake sisi tunaoenda huko tunaonekana kama mzigo kwao kwa hiyo wanatu treat immigrants kama second hand au scraper wanakutumia to the maximum kiasi kwamba hela utakayopata kwa mshahara karibu nusu yake utaiacha kwenye kodi na nusu iliyobaki utalazimika kulipa acommodations, chakula na mahitaji mengine at the end of the day hautabaki na kitu (savings) ndiyo maana kama mtu huna elimu maana yake huna kazi nzuri humchukua muda mrefu sana kuji establish huko. Baada ya maelezo hayo nilimuona uncle kama mzushi tu nikamng'ang'ania hadi akanipanauli, nilikuja kuamini maneno yake baada ya miezi sita tu ya mwanzo.
Kwa maana hiyo unataka kusema kuna Tax Code ambayo ni Special kwa immigrants tu.
 
....ndiyo maana kama mtu huna elimu maana yake huna kazi nzuri humchukua muda mrefu sana kuji establish huko. Baada ya maelezo hayo nilimuona uncle kama mzushi tu nikamng'ang'ania hadi akanipanauli, nilikuja kuamini maneno yake baada ya miezi sita tu ya mwanzo.

Tatizo lako una jenerelizi sana,
 
Kwa nini unafikiri kumfanya mtu atake kurudi nyumbani ni kumsaidia? Hii condescending attitude inatoka wapi?

Different strokes for different folks. Mbona tunaona watu wanarudi nyumbani, only to come back to the west (wenye access at least)?

This is a continuation of the cornucopia of cliche embracing small-mindedness and lack of focus plaguing our society. Watu wenyewe walio west mostly si enterpreneurs, una kazi za kuwapa wakirudi na kutaka kufanya kazi katika professions zao?

Some of us actually believe that nationalism is overrated and can act as a hindrance to development just as it can be used for development.

Home is where you make it, and there is no reason to be limited by spatial proximity in this age of inter-continent spanning careers and homes.

Let's not limit ourselves by some medieval thinking. As long as it works for you, and it is not illegal, do you.

Mimi silazimishi watu walio Nanyumbu waje kiwanja, kwa nini watu walio nyumbani watushikie bango?

Wengine tushaona in our hearts of hearts Tanzania pako nyuma kwa decades kibao kwa maisha tunayotaka, and the best thing for us to do is to carry Tanzania within our hearts and bring it where we are. What's wrong with that?

Si kila mtu ana priorities zenu hizo za kuwa force feed na groupthink inayo revere nyumbani hata kama nyumbani kwenyewe hakubebeki. Wengine tuna deal na the essentials tu. Kwingine huko, you do you, I do me.

Mwisho tutaanza habari za kuangalia garbage ili tuone nani kala mayai nani kala kauzu. Tuacheni hizo. It just shows mtu hana cha kufanya.

Wakati wenzetu wanafikiria kuhama hii sayari kikinuka hapa, sie tuna question kuhama nchi !
Kiranga

Naheshimu mawazo yako lakini umeyatoa ukitawaliwa na emotions zaidi kuna sehemu zingine nikiri sikukuelewa unamaanisha nini.
Nilipobold, ninaposema watu kurudi sina maana ya kurudi likizo ya wiki moja au mwezi ni kukusanya alichochuma na kukirudisha nyumbani.

Unaposema wakirudi nitawapa kazi gani hili liko kwenye emotions zaidi unategemea nani aziandae hizo kazi kwa hao wageni watakaokuja nawaita wageni kwa sababu ni mgeni tu anayeandaliwa kama wao wako huko kwa miaka kumi unategemea nani awaandalie think about it.

Unaposema priority zenu una maana gani ninachoongea mimi ni mawazo yangu binafsi.

Kiranga tusiwe tunaiona Tanzania kama is a lost and failed state kuwa haiwezi kutoka ilipo kwa hiyo kilichobaki ni kuikimbia na kwenda kuishi nchi zilizojengwa na wengine, tuisaidie nchi yetu kwa kubaki Tanzania. Nitabaki Tanzania hata kama ni nchi masikini kiasi gani, kumbuka huwezi kumkataa mzazi wako kwa vile tu ni masikini ni wajibu wako kumsaidia.
 
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda mrefu sana bila kupata jibu, ingawa mimi pia nilikuwa huko lakini nilibahatika kurudi nyumbani. Uzoefu wangu unaniambia kuwa ukiona mtu amekaa nje zaidi ya miaka mitatu kama si mwanafunzi au mwana diplomasia kama vile balozi basi ujue kuna tatizo, baadhi ya sababu au matatizo ninayodhani yamemfika mtu kama huyo ni haya yafuatayo;

1. Amejilipua (kaomba ukaazi wa ukimbizi kwa kutumia nchi nyingine Asylum seekers)
2. VISA imeleta matatizo wakati huo huo hataki kurudi anaogopa immigrations (wengi wa type hii ni waliokuwa na student visa ime-expire).
3. Hana elimu kiasi kwamba akirudi nyumbani atafikia kazi aliyoiacha (wengi wa type hii ni wazamiaji wa meli nk).
4. Hana uzalendo na nchi yake anaona bora abebe box na kulipa kodi kule (carefree).
5. Ameoa au ameolewa na mzungu (nafikiri hawa ni njaa tu).
6. Aliondoka nyumbani TZ kwa matatizo wanasema kakimbia soo mfn (kutoroka kesi, mauaji, kubaka, uhaini, political issues, kukorofishana na familia kama kuuza nyumba, nk)
7. Anaona aibu kurudi kwa sababu aliyotegemea na aliyoyakuta ndivyo sivyo (miaka saba sasa imekatika hata shule aliyoahidi hakuna)
8. Hana thamani tena nyumbani labda hana wanaomtegemea (baba, mama, watoto) yeye ndiye familia kwahiyo anaona bora afie huko huko.
9. Hana makaratasi kabisa hajaomba asylum seekers wala nini anaishi kwa kukwepa immigrations maisha ya wasiwasi.
10. Kuna waliosema potelea mbali bora kuteseka Ulaya kuliko kuteseka Tanzania.
11. Mbaya zaidi ni wale wanaoona ujiko kuishi majuu ingawa hawana sababu yoyote ya kuzidi kukaa huko mali wanayo na uwezo wa kurudi wanao.

Ndugu wanaJF hizi ni baadhi tu ya sababu nilizoona kwanini wenzetu hawarudi nyumbani JE tuwasaidiaje?

Nawasilisha- Naomba samahani kwa nitakaowakwaza kwa namna yeyote ile.

Mkuu inawezekana una idea nzuri, tatizo ni jinzi ulivyoipresent. Kwa vile wewe umeshakaa nje na kurudi nyumbani labda ungewanufaisha sana wale walio nje at least kwa kujaribu kuwaeleza what have you done so far tokea urudi nyumbani. Badala yake naona kama ume jump straight kwenye conclusions na kuanza kumake assumptions ya sababu tena ambazo umesema unadhani ndizo zinazowakwaza watu wasirudi. Hii ina maana kuwa huna hata uhakika kama hizo ni sababu. Rather, unadhani. Sasa sijui hawa watu watasaidiwaje kama sababu ulizozitaja ni za kudhani.

Kwa mfano, unadhan kuwa moja ya sababu ni kuwa wengine hawana elimu kiasi kwamba wakirudi nyumbani watafikia kazi waliyoiacha. Sasa kwa mtu kama huyu utamsaidiaje? Uko tayari kumpa kazi au kumsomesha? Umependekeza organisation inayoweza kuwasaidia kurudi. Je, wewe uliitumia wakati unarudi? Nafikiri la muhimu zaidi, ni wewe kujaribu kuwaelezea wahusika what have you achieved to yourself or you have done to the nation so far tokea urudi. Then, jaribu kutumia hizo achievements to encourage them to come back. I think that would have been much better than listing sababu unazodhani then unauliza wanaJF tuwasaidiaje.

Pia tathmini sentensi yako ya mwisho. Pamoja na kuwa umetanguliza samahani it may actually mean the other way round. It could mean to others that they are an idiot and you're about to tell them so but politely. It could mean that you meant no offense but you're going to offend the targeted people. It could also be interpreted to mean that you're going to be an ass with this thread and you will regret it later. So, Mkuu be careful with your choice of words. If you honestly believe what you are saying is nothing but the truth, then there is no need kuomba samahani kwa utakaowakwaza simply because you will be saying the truth. JF is the home of great thinkers, and great thinkers don't make assumptions or unnecessarily apologies.

Respect Mkuu.
 
Kiranga

Naheshimu mawazo yako lakini umeyatoa ukitawaliwa na emotions zaidi kuna sehemu zingine nikiri sikuuelewa una maana gani.
Nilipobold ninaposema watu kurudi sina maana ya kurudi likizo ya wiki moja au mwezi ni kukusanya alichochuma na kukirudisha nyumbani.

Unaposema wakirudi nitawapa kazi gani hili liko kwenye emotions zaidi unategemea nani aziandae hizo kazi kwa hao wageni watakakaokuja nawaita wageni kwa sababu ni mgeni tu anayeandaliwa kama wao wako huko kwa miaka kumi unategemea nani awaandalie think about it.

Unaposema priority zenu una maana gani ninachoongea mimi ni mawazo yangu binafsi.

Kiranga tusiwe tunaiona Tanzania kama is a lost and failed state kuwa haiwezi kutoka ilipo kwa hiyo kilichobaki ni kuikimbia na kwenda kuishi nchi zilizojengwa na wengine, tuisaidie nchi yetu kwa kubaki Tanzania. Nitabaki Tanzania hata kama ni nchi masikini kiasi gani, kumbuka huwezi kumkataa mzazi wako kwa vile tu ni masikini utabaki umsaidie.

Luteni, hujajibu swali. Ulikuwa unakaa ulaya nchi gani?
 
Kiranga

Naheshimu mawazo yako lakini umeyatoa ukitawaliwa na emotions zaidi

Kati ya wanaotetea economic pragmatism na wanao embrace blind nationalism nani anafuata emotions? Wanaotaka watu walioenda kuchuma nje warudi nyumbani ili wakose kazi na kuishia kutazamana na kuzua matatizo mimi nawaona ndio wanaofuata emotions kuliko pragmatism.

kuna sehemu zingine nikiri sikuuelewa una maana gani.

Of course huelewi. Unatetea pre-globalization introvertion utanielewa vipi?
Nilipobold ninaposema watu kurudi sina maana ya kurudi likizo ya wiki moja au mwezi ni kukusanya alichochuma na kukirudisha nyumbani.

Nimeshasema mwanzo, home is where you make it. And again, what has to come back home anything to do with contributing back home in this age of electronic money transfer? Mtu wa New York anaweza kutuma funds kirahisi kwenda Dar au Mwanza kuliko mtu wa Musoma anavyoweza kutuma funds Dar.

Unaposema wakirudi nitawapa kazi gani hili liko kwenye emotions zaidi unategemea nani aziandae hizo kazi kwa hao wageni watakakaokuja nawaita wageni kwa sababu ni mgeni tu anayeandaliwa kama wao wako huko kwa miaka kumi unategemea nani awaandalie think about it.

Na wao kwa kukataa adha hii ya kuandaa ajira zao wenyewe ndiyo maana hawataki krudi, sasa tatizo liko wapi? Not everybody is cut out for enterpreneurship. Ukitaka warudi wape cha kufanya, kama huna cha kuwapa usiwabughudhi.

Unaposema priority zenu una maana gani ninachoongea mimi ni mawazo yangu binafsi.

Huna mawazo binafsi, sijaona wazo binafsi hata moja katika posts zako zote, ninaona Borg-like compliance tu.

Kiranga tusiwe tunaiona Tanzania kama is a lost and failed state kuwa haiwezi kutoka ilipo kwa hiyo kilichobaki ni kuikimbia na kwenda kuishi nchi zilizojengwa na wengine, tuisaidie nchi yetu kwa kubaki Tanzania.

Mimi hata siamini katika concept ya nation-state (sio Tanzania tu, the very idea of a nation state is running out of time and eventually will be moot, sadly I am rather futuristic for this idea to be perfectly understood clearly now), nishasema hii ni a political illusion inayotumiwa na wanasiasa kuwashikia akili sheeple. Sasa kwa nini unilazimishe niamini kitu ambacho hakiko pragmatic kwangu? I look at myself as a citizen of the world, I have the track record to make it happen at the global scale, so why do you want to limit me to Tanzania? Tanzania doesn't even have a stock market to speak of where I can tout my wares and expertize in a convenient way, kwa nini unaniandama wewe na mie hata sijakuomba ubadili maisha yako kwa ajili ya principles zangu?

Mahubiri haya yanatoka wapi? Moral authority ya kuwapangia watu maisha mnaitoa wapi?

Nitabaki Tanzania hata kama ni nchi masikini kiasi gani,

Sikuandami kwa hilo, na wewe rudisha ustaarabu huu kwa kutowandama walio nje.

kumbuka huwezi kumkataa mzazi wako kwa vile tu ni masikini utabaki umsaidie.

Hakuna anyemkataa mzazi, tunachokataa sisi ni kubakia nyumbani kwenye banda la uani bila shughuli wakati mji wa pili kuna kazi tele.
 
Mkuu labda tuangalie Priority za Mtu kwenye maisha yake..., Who is he responsible for; Kwa mawazo yangu he is responsible for the following in the following order:-
HIMSELF
HIS FAMILY
OTHERS
Sasa hapo kwenye Others ndio kuna (A persons Country)

Hivyo basi ninaamini kuwa a person should go or do anything ambacho kitamnufaisha yeye na familia yake, kama akiona huko aliko hata kama ni (TIMBUKTU) kunampatia maisha bora kuliko Bongo Fair Enough, Mwingine labda anapenda maisha na mandhari ya sehemu fulani, who are we to judge him or say otherwise....

By your Point unaweza ukasema kuwa Rostam ni Mzalendo zaidi sababu anaishi Bongo kuliko wabongo wanaoangaika huko nje ile wapate maisha bora au wawasaidie ndugu zao, This is a Global Village now..., Wherever you can make it, Go Ahead; After all bora tusambae kwenda kutafuta kuliko kubaki wote tunaangaliana....
 
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda mrefu sana bila kupata jibu, ingawa mimi pia nilikuwa huko lakini nilibahatika kurudi nyumbani. Uzoefu wangu unaniambia kuwa ukiona mtu amekaa nje zaidi ya miaka mitatu kama si mwanafunzi au mwana diplomasia kama vile balozi basi ujue kuna tatizo, baadhi ya sababu au matatizo ninayodhani yamemfika mtu kama huyo ni haya yafuatayo;

1. Amejilipua (kaomba ukaazi wa ukimbizi kwa kutumia nchi nyingine Asylum seekers)
2. VISA imeleta matatizo wakati huo huo hataki kurudi anaogopa immigrations (wengi wa type hii ni waliokuwa na student visa ime-expire).
3. Hana elimu kiasi kwamba akirudi nyumbani atafikia kazi aliyoiacha (wengi wa type hii ni wazamiaji wa meli nk).
4. Hana uzalendo na nchi yake anaona bora abebe box na kulipa kodi kule (carefree).
5. Ameoa au ameolewa na mzungu (nafikiri hawa ni njaa tu).
6. Aliondoka nyumbani TZ kwa matatizo wanasema kakimbia soo mfn (kutoroka kesi, mauaji, kubaka, uhaini, political issues, kukorofishana na familia kama kuuza nyumba, nk)
7. Anaona aibu kurudi kwa sababu aliyotegemea na aliyoyakuta ndivyo sivyo (miaka saba sasa imekatika hata shule aliyoahidi hakuna)
8. Hana thamani tena nyumbani labda hana wanaomtegemea (baba, mama, watoto) yeye ndiye familia kwahiyo anaona bora afie huko huko.
9. Hana makaratasi kabisa hajaomba asylum seekers wala nini anaishi kwa kukwepa immigrations maisha ya wasiwasi.
10. Kuna waliosema potelea mbali bora kuteseka Ulaya kuliko kuteseka Tanzania.
11. Mbaya zaidi ni wale wanaoona ujiko kuishi majuu ingawa hawana sababu yoyote ya kuzidi kukaa huko mali wanayo na uwezo wa kurudi wanao.

Ndugu wanaJF hizi ni baadhi tu ya sababu nilizoona kwanini wenzetu hawarudi nyumbani JE tuwasaidiaje?

Nawasilisha- Naomba samahani kwa nitakaowakwaza kwa namna yeyote ile.

Ujumbe wako ulikuwa mzuri sana Luteni, ila umeshindwa kuwa fair katika hiyo point yako,kabla haujaanza kusema kwamba watu hawa wameshindwa kurudi nyumbani lazima ujue ni sababu gani za msingi zilizowafanya mpaka sasa wawe nje ya nchi. kumbuka vilevile katika watu hao waliopo nje kuna madaraja ya aina mbalimbali, Mfano; Mabalozi, watumishi wa ofisi za ubalozi, wanafunzi ( ambao asilimia kubwa utakuta ni watoto wa vigogo walioko serikalini ), vilevile kuna Wasomi na Wanataaluma bila kusahau watu wengine walioko nje ya nchi kwa sababu za msingi, nasema ni za msingi sababu kama zisingekuwa za msingi wasingekuwa huko mpaka leo.

Uzalendo:

Hivi ni nini maana ya uzalendo? Mimi nadhani kuishi ndani ama nje ya nchi hakumfanyi mtu kuwa mzalendo, ndg Luteni jaribu kuipitia tena historia ya Tanzania na Afrika kwa ujumla utaona kwamba kuna kipindi hata wazalendo waliokuwa wakidai uhuru wa nchi zao waondoke sehemu mpaka nyingine kukamilisha lengo lao ( kwa leo naomba tusilizungumzie hili ). Mimi nadhani uzalendo ni matendo ya mtu na wala si maneno yake, hebu niambie ni watu wangapi waliopo Tanzania ni wazalendo wenye kuweza kufia nchi yao?, mfano ndani ya serikali ya Kikwete n. kuendelea, sioni hata mmoja zaidi ya nchi kuendeshwa kisiasa zaidi, ndio maana kila kukicha ni maandamano na migomo, watu wanashindwa kufanya kazi yao kama inavyopaswa sababu maslahi ni madogo na kazi wanayofanya ni kubwa sana, ndio maana wengi wao wanaamua kwenda kufanya kazi nje ya nchi sababu huko kuna maslahi zaidi na kazi zao zinathaminiwa, basi kama serikali itataka watu hawa warudi basi ni bora wawajengee mazingira mazuri ya kazi.

Kuhusu Maboksi:
sisi Watanzania tuna tabia ya kupenda kuchagua kazi na kudharau anachofanya mwingine, kwa hili hatutaendelea, sasa Luteni niambie mbeba maboksi wa hapo Kariakoo na anayebeba mfano New York ni yupi mwenye ujira zaidi? tunarudi palepale kwamba tatizo ni kutokuthaminiwa kile anachofanya mwenzako, hawa unaowaita wabeba maboksi karibu kila mwezi wanatuma pesa kuzisaidia familia zao, kuna mada tuliyokuwa tukiijadili hivi karibuni kama ukitaka kujua zaidi nadhani utaona ni kiasi gani wanachangia pato la taifa kwa Mwaka, pia hao hao wabeba maboksi ni wengi tu wameshaweka vitega uchumi katika nchi yao, halafu mtu kama huyo unamdharau, hebu fikiria mtu kama huyu angebaki kukaa tu kijiweni ama kufanya kazi inayompatia dola moja tu kwa siku unadhani angeiendelezaje jamii yake?

Kuoa ama kuolewa na Mzungu:

nadhani ni wachache sana watakaokubaliana na wewe kusema kwamba ukioa ama kuolewa na mzungu ni njaa, unaonyesha upeo mfinyu katika hili , ni utumwa wa kifikra kudhania kwamba Mtu mweupe ni bora zaidi kuliko wewe, na hili sio tatizo lako tu, ni tatizo la watanzania wengi tu ambao wakiona mzungu hudhani kwamba basi ni lazima atakuwa tajiri ama ana akili sana , mimi nadhani TV, Sinema na utamaduni wa Ki- magharibi unaharibu sana future yetu ya mbeleni, kwa mtu ambaye hajawahi kufika Mfano Ulaya ama Marekani hudhania kwamba vitu wanavyoviona kwenye Sinema ni halisi, Ukweli ni kwamba hata Ulaya kuna watu wanaombaomba mitaani, kuna watu hawana makazi ya kuishi, kuna watu hawana kazi , Kuna watu hawana elimu, hapa namaanisha hawapendi kusoma! hakuna maisha rahisi kwenye dunia hii.
 
The underlying first principle violated by the premise of this thread is.

You cannot decide another's destiny, nor can you stand in his/her shoes and see the world exactly the same.

Mtu mzima hakatazwi kuvuta sigara chumbani kwake, hata kama sigara inaweza kusababisha kansa.
 
Umeme! wewe utarudi kwenye giza wakati una-chance ya kukwepa hiyo adha?
 
Kiranga na wengine nashukuru kwa maoni yenu ila sasa nakwenda kubeba box nitarudi baadae nijibu maswali yenu likiwemo la SA anayetaka kujua nilikuwa ulaya ipi. Box nalokwenda kubeba ni la hapa hapa bongo nalipa kodi hapahapa bongo ingawa inaishia kwa matumbo ya wengine.CIAO.
 
Back
Top Bottom