Kwanini walio nje huwawia ngumu kurudi nyumbani? Tuwasaidiaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini walio nje huwawia ngumu kurudi nyumbani? Tuwasaidiaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Jun 15, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda mrefu sana bila kupata jibu, ingawa mimi pia nilikuwa huko lakini nilibahatika kurudi nyumbani. Uzoefu wangu unaniambia kuwa ukiona mtu amekaa nje zaidi ya miaka mitatu kama si mwanafunzi au mwana diplomasia kama vile balozi basi ujue kuna tatizo, baadhi ya sababu au matatizo ninayodhani yamemfika mtu kama huyo ni haya yafuatayo;

  1. Amejilipua (kaomba ukaazi wa ukimbizi kwa kutumia nchi nyingine Asylum seekers)
  2. VISA imeleta matatizo wakati huo huo hataki kurudi anaogopa immigrations (wengi wa type hii ni waliokuwa na student visa ime-expire).
  3. Hana elimu kiasi kwamba akirudi nyumbani atafikia kazi aliyoiacha (wengi wa type hii ni wazamiaji wa meli nk).
  4. Hana uzalendo na nchi yake anaona bora abebe box na kulipa kodi kule (carefree).
  5. Ameoa au ameolewa na mzungu (nafikiri hawa ni njaa tu).
  6. Aliondoka nyumbani TZ kwa matatizo wanasema kakimbia soo mfn (kutoroka kesi, mauaji, kubaka, uhaini, political issues, kukorofishana na familia kama kuuza nyumba, nk)
  7. Anaona aibu kurudi kwa sababu aliyotegemea na aliyoyakuta ndivyo sivyo (miaka saba sasa imekatika hata shule aliyoahidi hakuna)
  8. Hana thamani tena nyumbani labda hana wanaomtegemea (baba, mama, watoto) yeye ndiye familia kwahiyo anaona bora afie huko huko.
  9. Hana makaratasi kabisa hajaomba asylum seekers wala nini anaishi kwa kukwepa immigrations maisha ya wasiwasi.
  10. Kuna waliosema potelea mbali bora kuteseka Ulaya kuliko kuteseka Tanzania.
  11. Mbaya zaidi ni wale wanaoona ujiko kuishi majuu ingawa hawana sababu yoyote ya kuzidi kukaa huko mali wanayo na uwezo wa kurudi wanao.

  Ndugu wanaJF hizi ni baadhi tu ya sababu nilizoona kwanini wenzetu hawarudi nyumbani JE tuwasaidiaje?

  Nawasilisha- Naomba samahani kwa nitakaowakwaza kwa namna yeyote ile.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du mzee kama ndiyo mtazamo ulio nao kuhusu kuishi nje ya nchi basi you are very wrong na ulifanya vizuri sana kuchukua hatua ya kurudi Tz mapema.
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuniambia sababu za kuendelea kuishi nje kama wewe si mwanafunzi au mwanadiplomasia baada ya miaka mitatu mfano.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kikubwa ni kwamba Watanzania wengi huko ughaibuni hawafanyi kazi profesional, kwahiyo wengi ni watu wa deiwaka maarufu kama wapiga box, sasa pesa inayopatikana nyingi inaishia katika kugharamia maisha yako pale kwenye nchi husika.

  Kumbuka huwezi kutoka ughaibuni kuja kutembelea ndugu Tanzania ukiwa na dola 1000 kama ndio pocket money yako, hili ndilo taizo kubwa, lakini nakuhakikishia mtu yeyote ambae anafanya kazi profesional ughaibuni ana uhakika wa kuja Tanzania kila December na kusherehekea mwaka mpya na familia yake.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu sitaki kuamini kwamba unaamini ni vitu viwili tu vinavyomfanya mtu aishi nje ya nchi. Kwa hiyo akina Drogba, Essien, Prof. Materu, Prof Mbele, Wajasiriamali, even myself kwa sababu si wanafunzi au wanadiplomasia basi we belong to your list.....duh?

  Mkuu kuishi nje ya nchi siku hizi hakuna tofauti na wewe amabaye say kwenu ni Musoma ukaenda kuishi Mtwara au kwenu Sumbawanga ukaishi Dar likewise kwenu Zenji ukenda kuishi Mwanza. Sasa kwa nini iwe ni ishu kwa mtu wa Shinyanga kuishi NY? Au mtu wa Mbeya kuishii Monaco?

  Mkuu kuna watu wako hapo Dar kwao Dodoma wanakaa miaka hadi 5 bila kukanyaga kwao if that is the concept na response time ya ishus za kwao inaweza kuchukua hata wiki au mwezi wakati kuna mtu yupo Seattle home kila mwaka na response time ya matatizo au community ishuz ni ndani ya siku moja. Anywayz inategemea lakini na nje uliyokuwepo wewe na experience uliyoipata hence ukaamua kugeneralize.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa mkuu hata huyu the so called mbeba box akija hapo bongo atabeba box wapi?
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  @new york ,usa
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Luteni,

  Na wewe una mawazo kama hayo kuhusu wanaokaa nje ya nchi? Basi tuna kazi kubwa sana ya kuwaelemisha Watanzania.

  Wanaokaa nje ya nchi hawana tofauti na wanaohama wilayani kwao kuhamia miji mikubwa Tanzania. Kuna mchanganyiko mbalimbali wakiwa na matatizo na mafanikio mbalimbali.

  Bila kujali huyu Mtanzania yuko wapi, kama ana uwezo wa kujilisha yeye mwenyewe au na familia yake basi ni nafuu mno.

  Tusiwe negative sana na watu wanaohama makwao na kwenda kujitafutia opportunities sehemu zingine. In fact kama vijana wetu wengi watahama na kutapakaa duniani wakitafutia chakula yao itakuwa nafuu zaidi kuliko kulundikana sehemu ambazo hawana hata uwezo wa kujilisha.

  Stereotyping kama hizi sidhani kama zinamsaidia mtu yeyote.

  kwa mawazo yangu mimi baada ya kukaa nje kwa muda mrefu, kutembea TZ sehemu mbalimbali, kutembelea nchi mbalimbali zingine, naona Tanzania kama nchi iwe na utaratibu ambao ni rahisi kwa watu wake kwenda kuishi popote pale duniani kwa faida yao wenyewe.

  Hao watu hata wasiporudisha senti tano TZ bado kwa nchi ni faida maana angalau wanakuwa sio mzigo au wanakuwa hawana mzigo wowote kwa taifa TZ.

  Tanzania tulichelewa sana kuanza kutoka shauri ya siasa zile za zamani na hilo limetu cost kwenye mambo mengi.

  Tumchukulie kila mtanzania kama mtu mzima mwenye utashi wa kuamua akae wapi, aende kwao mara ngapi au aishi na nani. Hata kuoa Wazungu nako ulivyokuelezea uko wrong sana. Binadamu hukamata opportunities zinazomzunguka, ndio maana Mnyakyusa anayeanzia kazi Kagera mara nyingi utakuta ameoa Mhaya, anayeanzia Kilimanjaro, anaoa mtu wa Kilimanjaro. Hata nje ni hivyo hivyo, vijana wengi wanakuja umri ambao wanakuwa hawana wake, hivyo wanapoanza kutafuta watu wa kuishi nao wanajikuta walio wengi ni hao wanaowazunguka na kama ni Ulaya basi ni wazungu. Mimi sijaoa mzungu kwasababu kwenye darasa langu kulikuwa na Mtanzania mwenzangu na ndiye tukaoana. Lakini siwalaumu wenzangu wengine wengi ambao mwanamke pekee ambaye angeweza kumwona na kumtongoza alikuwa Mzungu. Sasa ulitaka mtu kama huyo afanye nini?

  Kutatokea mtu mmoja ataoa kwasababu ya makaratasi kama ambavyo nyumbani kutatokea mtu ambaye anaoa au kuolewa kwasababu ya utajiri wa mpenzi wake au familia ya mtu anayetaka kumwoa. Lakini hiyo haifanyi ndoa zote zionekane ni kutafuta ulaji. Hii ni stereotyping nyingine ambayo ni upotoshaji.

  waacheni vijana wafanye wanachotaka bila kuanza kuja na maneno maneno ambayo hayajafanyiwa hata utafiti mdogo.

  Siku hizi sio mchangiaji mzuri hapa lakini nilipoona hili nikaona nina wajibu wa kusaidia kuelemisha hasa kwa wale wapotoshaji.
   
 9. womanizer

  womanizer Senior Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani arudi kwenye ardhi ya mafua na ukurutu. Sisi tunaendelea kula bata ughaibuni nyie endeleeni na jua lenu la Kariakoo, kama mna shida ya vijisenti basi mni PM niwarushie.
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Umegusa pabaya bwana...ha ha
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh wewe mwenyewe huna uhakuka wa lunch, halafu unauliza uwasaidieje?
  Watakuwa hawana mipesa ya kurudi home ndio kitu pekee unachoweza wasaidia.
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mentalic slave statement, kwahiyo hawa wazungu wanaokuja kila siku Bongo ambao wanatoka ughaibuni wanafata ukurutu? hapa sina haja ya kukuuliza hata umri wako, kwani tayari mawazo yako yameshanionesha mpaka umri wako.
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wenzako wanakuja kuchuma wakipata wanakwenda Malta kutanua......na utakula vumbi sana bwamdogo
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mko wengi wenye kasumba kama hizi...ila danganyeni wasowajua na mkataa kwao mtumwa
   
 15. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Na bado inakuja East African Community, sijui nikihamia Uganda mtanisemaje??? Dunia mtaa siku hizi, kutoka kona moja ya mtaa kwenda kona nyingine.
   
 16. s

  shosti JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  achana nae huyo.....hawa ndio akina unatoka nchi gani anakwambia Afrika.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Wewe Yo Yo si mtu wa viwango vyangu, bahati nzuri hata Moderators na Invisible wanajuwa fika kwamba unahitaji ushauri nasaha, wewe ni mtumwa namba moja kwa kuwa proudly kama mkenya wakati wewe ni mtanzania.
  Umri wa mtu huwa unajulikana hata kwa kuangalia keyboard pale mtu anapokuja na matango pori kama wewe, kama wewe unaona Ughaibuni ni bora kwa nini huwa unamponda William @ New york, USA?
  wewe ni FALLA tu.
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nyambala

  Jaribu kunielewa kuwa sikatai watu kwenda nje na kuishi nje lakini najaribu kuonyesha sababu zipi za msingi zinazokufanya uishi huko miaka mingi na nyumbani kuwa unakuja likizo tu (holiday) na kurudi zako. Kina Drogba kama ulivyosema wanajulikana wanafanya biashara gani na huko nyumbani kwao wanafanya maendeleo gani. Mimi ninaozungumzia ni wale wasiona shughuli maalumu kazi kukimbizana na polisi wa kule mfano visa imekwisha na sababu nilizozitoa hapo juu kwanini wasirudi nyumbani? Hata huyo wa Dodoma ambaye yuko Dar kwa miaka mitano na hajarudi nyumbani ni wa kusaidiwa kama hawa ndugu zetu lakini hiyo ni topic nyingine.
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Angalia usijefikiri unakula bata kumbe bata wako analiwa.
   
 20. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mmmnnnhhh...sidhani kama hiyo analysis yako ina ukweli. Kama upo ukweli bas may be ni 1%
  Kama mtu alimaliza shule na akapata kazi nzuri tu, then employer wake akamfailia papers na akapata premanent residency. The same person anakuja bongo kila X-Mass kuwaona ndugu zake. Huyu nae utamweka ktk category gani?
  Inaonekana ulichoongelea ni personal experience yako wewe mwenyewe na uko in denial to the point umeamua kugeneralize kwamba watu wote walioko ughaibuni wako kwenye hiyo situation iliyokupata. I'm convinced kabisa wazee walikubeba na ukarudishwa.
  There are thousands of Tanzanians in every corner of the globe. So sio vizuri na sahihi kugeneralize kwamba wabongo woote walioko ughaibuni hawarudi bongo kutokana na sababu ulizozisema. Kila mtu ana maisha yake na choices zake. Akibaki ughaibuni ruksa, akiamua kurudi sawa. Usipende kuongelea maisha ya watu bana!
   
Loading...