Kwanini walimu wengi wanaotokea DUCE na MUCE wawapo field au kazini hung'ang'ania kutaja UDSM?

Ntandaba

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
922
1,472
Habari zenu wakuu?
Kama kichwa cha thread kinavyojipambanua kwa nini hawapendi kujitambulisha kwa kutaja majina halisi ya branch zao?
Mwenye kujua sababu tafadhali tiririka kidogo
 
Habari zenu wakuu?
Kama kichwa cha thread kinavyojipambanua kwa nini hawapendi kujitambulisha kwa kutaja majina halisi ya branch zao?
Mwenye kujua sababu tafadhali tiririka kidogo
Hivi ni vyuo vya kipuuzi tu ndiyo maana hawataki kujinasibu navyo. Kuna mmoja amenikaba koo humu kuwa ana div 2 alikwenda ualimu, na amepata 2ND UPPER alipomaliza DUCE. Nikamuuliza DUCE mbona ni kama chuo cha Advanced diploma, walimu waliobobea wamewatoa wapi? Ni wale wale waliokuwa wanafundisha diploma, sasa lecturers waliobobea wanatoka wapi? Akanitukana.
 
Yupo sawa kusema anasoma chuo cha UDSM lakini ukimuuliza upo branch gani akisema nipo UDSM branch huyo muongo maana hakuna branch inayoita UDSM. Na akiogopa kutaja branch yake basi mpime akili kama yupo salama kwa kuangalia vyeti vyake isije ikawa ni sawa na wale 480 waliofutiwa udahili wao sababu ya kufeli.
 
Wako sawa kabisa! Kwani vyeti vyao vimeandikwaje? Mfano pale DUCE kitengo cha science kinaendeshwa na lectures kutoka mlimani, kisha ukimaliza cheti kinaandikwa University of Dar es Salaam kwa herufi kuubwa! Sasa kosa lao li wapi?
Lazima ujitetee, DUCE MUCE havina hadhi ndiyo maana wanangagania UDSM
 
Nchi hii kuna watu wengi hawajielewi, hao wanaosoma hivyo vyuo wengi wao hawakujua hata nini watasoma baada ya A Level. Wengi wao hawa ni majanga na hawajiamini. Kwani akisema kuwa anasoma DUCE au Mkwawa anafikiri heshima itapungua? Chuo cha afya muhimbili nao walikuwa na element hizohizo kabla hawajajitambua na kujikubali. Kwa sasa wameshajitambua na wanajiamini. Hawa nao ipo siku watajitambua tu, pengine ni sababi ya ujinga na ushamba unawasumbua.
 
Chili suala lipo sana.. Kuna dogo alifaulu kuja Chuo akaniambia anakuja UDSM...nikajua yess.. Nmepata mbebaji.. Siku anafika ati anadai ati ye amechaguliwa UDSM tawi la DUCE..
Kaliniboa
 
Inaitwa main campas lakini bila college zake haiwezi kuwa na sifa ilizonazo sasa! Ata ranking inayofanyika inazingatia pia research zinazofanywa na waalimu wa DUCE ambao hishinda DUCE na kulala main campus!
 
Mwimbili, Sua pamoja na Ardhi for now ni universities zinazojitegemea lakini nazo zilikua ni School au idara au constituent colleges baada ya kujikamilisha kwa resource zote ndio zikajitenga. Hope sasa umeelewa kwa nini mwanafunzi anasema nimemaliza UDSM na sio DUCE au MUCE?
 
bora mshahara na upande madaraja vizuri tu ! hayo ya duce nn cjui hayahusu saaaana ! maliza degree kako pata pay 716 wakukate ubaki na 571 ingia CRDB/BOA chukua loani mil.20 zako wakukate 282 , jenga banda lako na inayobaki chukua toyo maisha yanaenda.WATU hawatajua umesomea wap watajua tu ualimu siku hizi unalipa.
 
Back
Top Bottom