Kwanini walimu wa shule binafsi wasirudishwe serikalini

kichwabox

Senior Member
Feb 14, 2016
152
40
Kufeli kwa wanafunzi shule za serikali ni sababu ya walimu kukimbilia shule binafsi kwa kuwa wana ujuzi kwanini wasipewe uchaguzi warudi serikalini hata kama waliacha? Wadau naombeni mchango wenu.
 
Itategemea ikiwa kile walichokikimbia hakipo tena basi waweza rudi vinginevyo hata sekta binafsi inawafaa wale wenye kumudu. Jambo la maana ni kwamba serikali inatakiwa kutazama upya picha ya mwalimu wa Tanzania ili afanane na dira ya taifa. Ukiona paka amekimbia nyumbani ili akajitafutie porini jiulize mara tatu kama unabisha hodi vile!:rolleyes:
 
Nakupa mfn,mwalimu wa msingi alie ajiliwa 2009 serikalini analipwa 430000/-makato anabakiwa na 380000 -nauli ya kuufata mshahara bank-mazingila magumu ya kazi..huku private analipwa 560000+posho+pesa za motisha pindi wanafunzi wakifanya vizur somo lake
 
private hakuna tija sana,shule chache sana za binafsi zinazolipa vizuri na kuzingatia kanuni za kuajiri.
 
Unadhani walimu waliopo serikalini hawatoshi? Au unadhani hawana ujuzi wa kutosha? Mbona walimu hao hao wakifundisha private wanafaulisha ila wakifundisha serikalini hawafaulishi? Tafakari chukua hatua.........
 
Achen ujinga,shule binafsi tunawekaga usaili,na mara nyingi hawa waalimu kama hawajui kiswahili,english hawajui tunawaacha,Tunachukua wenye ngeli,Pia nimeshawafanyia baadhi tukawaacha kwa kitu kidogo tu anashindwa tofautisha "r" na "l" anasema Alusha" ,dalesalama, Matofari"
 
Serikalini kuna siasa za elimu kuliko taalauma. Kuna maslahi duni na uongozi wa fitina na kupeana madaraka bila kujali ushindani wa uwezo taaluma na utendaji.

Shabikia chama chetu kesho ni mkuu wa shule isiyo na madawati wala vyoo.
 
binafsi kuna mchujo, kila mwisho wa muhula mwanafunzi anatakiwa afkishe avarage ya shule, kwahvo wanabaki wale brighter na si kweli walimu wao nitofauti na serkalini, hata shule za serkak zingeweka wastan wao kwa kila kidato mbona wengi wangefaulu.
 
Unapozungumzia kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne hasa kwa shule za serikali ni muhimu ukatambua kuna makundi takribani matano yanahusika kutoshirikiana ipasavyo mfano walimu,wazazi,serikali,jamii inayozunguka shule na wanafunzi wenyewe.

Utambue pia shule nyingi za o level ni za kata zilizojengwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 na zina changamoto lukuki zinazofahamika, zinachukua pia karibia 90% ya wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba ktk eneo husika.

Utambue pia wanafunzi hao wanakua familiar na mazingira husika zilipo shule hivyo kama kuna ujinga wowote walioka wakiufanya walipokua primary basi huhama nao kuja sekondari.Wanafunzi wa aina hii wanakua pia hawapati changamoto mpya za kimasomo na ni wepesi wa kuchukulia mambo kwa wepesi sana.

Sasa aina hii ya wanafunzi, ukachanganya na aina ya wazazi na jamii isiyojali au kuwekeza ktk elimu ya mtoto, unakutana na walimu ambao wengi wao wanatambua hawathamini kwa kiwango kinachostahili toka kwenye serikali yao; unategemea muujiza utokee?

Kwa hiyo si kweli kwamba eti walimu wa private ni bora sana kuliko wa serikali! ishu hapa ni kwamba makundi haya mawili yanatofautiana tu ktk utendaji wao kazi. mfano mwalimu wa private anafanya kazi kwa presha ya kufaulisha(ukifelisha huna ajira) na akifanya vizuri anatuzwa, private kuna mchujo kwa wanafunzi wao hivyo muda wote wanafunzi inawabidi kusoma kwa bidii wasifeli (na hii ni tangu unaanza moama unamaliza) wakati huku upande wa pili ni bora liende tu. pia mazingira ya ufundishaji kwenye shule nyingi za private ni bora zaidi kuliko shule za serikali. Mwalimu aliyefit ni lulu shule za private wakati upande wa pili anaonekana ni mpinzani(maana walimu wa aina hii hujiamini sana na wapo wengi tu)

Mwisho kabisa natoa rai kwa serikali ijipange na iwekeze kwa dhati na kwa vitendo ktk shule zake na itaona mabadiliko badala ya kutumia nguvu kuuuubwa kuwabana walimu kujaza fomu nyiiingi! mara opras mara lesson plan! Haitasaidia sana badala yake iwaboreshee tu mazingira yao ya kufanyia kazi then hapo ikiamua kuwabana poa. Pia ule mchujo wa 30% kidato cha pili urudishwe na sio kuwapitisha tu kwenda kidato cha 3 wanafunzi wasio na sifa. Wapo wanafunzi kwenye shule zetu za kata hawataki kusoma lakini wanalazimishwa tu na sera ya elimu! mtoto wa aina hii utegemee afaulu? hata uwe mwalimu bora kiasi gani huwezi kufanya muujuza.
 
mkuu sina cha kuongeza nimekupa asilimia 100
 
Back
Top Bottom