Kwanini walimu wa kumfundisha mwanamke aishi vipi kwenye ndoa ni wanaume na sio wanawake?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Wanaume wengi wawe viongozi wa dini au wa kijamii au wa mitaani ndio huwa wanakomalia kufundisha mwanamke anavyotakiwa kuishi na mwanaume.

Ukienda Misikitini unakuta Maimamu na Mashehe ndio walimu wa kumsomesha mwanamke aishije na mwanaume. Ukienda kwa Wasabato unakuta wanaume ndiyo walimu wakuu. Kwa Wakristo unakuta Mchungaji au Padri ndiye kinara wa kutundisha mwanamke aishije na mwanaume. Ukienda mitaani na Vijijini wanaume ndio hujifanya waalimu wa kufunza wanawake jinsi ya kuishi na mwanaume.

Hivi kwani wanawake huwa hawapewi nafasi ili wafunze wanawake wenzao jinsi ya kukaa na mwanaume? Wanaume wanaogopa nini kuwapa maiki wanawake wafunze wanawake wenzao?
 
Wanaojua vizuri kuwa mwanaume anataka nini kwenye ndoa ni wanaume wenyewe so ni vizuri kuwaacha wanaume wenyewe wafundishe kazi inakuwa ya uhakika ni sawa na kuvujisha mtihani.
 
Binafsi huwa naona hata zile kitchen party ni upuuzi tu. Kwa upande wangu naona ni vema sana na yafaa pia mwanamke afundwe na mwanamume maana ndiye anayeenda kuishi naye na ndiye atamuelekeza aenende vipi. Ukisikiliza ufundaji wa mwanamke kwa mwanamke mwenzie utagundua kwa nini ndoa hazidumu,huwa wanakazia vitu visivyo maana. YEHODAYA,
 
YEHODAYA, 1. Mwenyewezi MUNGU mwenyewe alianza kuumba mwanaume ndio akafuata mwanamke
2. Ukiangalia taifa tukufu ISIRAEL huwa wanawake hawaesabiwi ndio maana ukisoma hata Bible inaonesha kizazi cha Adam nasio Eva au Hawa.
3. Mwanaume kaubwa kuwa kiongozi ndio maana unaona kote huko yy ndio anatawala anaongoza tu.
 
Mwanamke nikama kifupa flan zaifu ambacho kimepinda ukikiacha tu juwa kitazidi kupinda na ukikinyoosha kwa nguvu basi jua utakivunja tu
 
Back
Top Bottom