Kwanini walimu na wastaafu ndio wahanga wa Utapeli wa QNET, DECI, D9 nk?

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,276
17,983
Bila kuwakosea heshima, nimekuwa nikijiuliza kwa nini wengi wa wanaoingia mkenge kwenye michezo hiyo ni Walimu- wastaafu na waliopo kazini.

Busara ya kawaida inaonyesha wangekuwa ndiyo waelewa wa kuwastua wengine wasiingie kwenye mitego hiyo.

Tatizo liko wapi?
 
Kwani wewe hujui walimu wengi ni form four failures??huonagi pia wanatumika km mtaji wa wanasiasa...inshort walimug wengi sio wote hawajielew especially wa primary ndo kabisaa...Pia mazingira wanyofanyia kazi hasa vijijin hata akili haichangamki kureason things
 
Naiona hoja yako Kiongozi.
 
"Wengi wa wanaoingia mkenge ni walimu" hususan wa primary schools. I.Q. ndogo. Na ndio wamepenyapenya kwa ujanja na cheap degrees za lugha, sijui psychology n.k. sasa ni wakurugenzi wa Halmashauri, maDC, DAS, n.k. Hali ni mbaya huko.
 
Dah! Nakumbuka kipindi kile D9,walivyo wapeleka baadhi ya members wao wa Africa wale wenye donnlers wengi.

Lkn mwisho wasiku walikimbia na Pesa zote

Tangia hapa sikujaribu Tena kushiriki hi michezo ya Upatu.
 
Mishahara kiduchu na hamna marupurupu...plus makato ya mabank na microfinance uchwara.... mtu akisikia fursa ya kuingiza ela bila kufanya kazi mashetani yote yanaamka na anaaingia kichwakichwa.....
 
Mwalimu asielewe hakuna hela ya aina hiyo?
 
Kwani wewe hujui walimu wengi ni form four failures??huonagi pia wanatumika km mtaji wa wanasiasa...inshort walimug wengi sio wote hawajielew especially wa primary ndo kabisaa...Pia mazingira wanyofanyia kazi hasa vijijin hata akili haichangamki kureason things
Kumbuka kila fani ina hao unaowaita form four failures kuanzia afya, sheria, elimu, kilimo, uhandisi, habari n.k
Hoja hapa sio kufeli form four ila maisha duni kwa kundi husika
 
Mishahara kiduchu na hamna marupurupu...plus makato ya mabank na microfinance uchwara.... mtu akisikia fursa ya kuingiza ela bila kufanya kazi mashetani yote yanaamka na anaaingia kichwakichwa.....
😅 😅 😅 😅 😅 😅 😅 mashetani yote yanaamka! Jamani nimecheka!

Mtu akisikia hatokula vumbi la chaki wala kushikia fimbo watoto wa watu, ambao wazazi wachawi! Anaona atafute kitu kingine.

Everyday is Saturday.............................:cool:
 
Back
Top Bottom