Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Leo nimemuona Salim Ahmed Salim akikabidhi tuzo ya Mo Ibrahim kwa mshindi wa tuzo hiyo Pedro Verona Pires, Rais Mstaafu wa visiwa vya Cape Verde. Kwa jinsi alivyokuwa anaongea na kujistahi nikajiuliza ilikuwaje mara mbili (1985 na 2005) wanachama wa chama chake walikataa asiwe mgombea wa chama chao kwenye nafasi ya Urais. Ina maana yeye sifa zake ni pungufu kuliko za Ally Hassani Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete?
Mapungufu ya Salim ni nini na ubora wao kina Mwinyi na Kikwete ni upi? Huyu jamaa kama taifa tunaweza kumtumia vipi kwani kwa inavyoelekea haiwezekani tena kwa yeye kugombea urais 2015.
Mapungufu ya Salim ni nini na ubora wao kina Mwinyi na Kikwete ni upi? Huyu jamaa kama taifa tunaweza kumtumia vipi kwani kwa inavyoelekea haiwezekani tena kwa yeye kugombea urais 2015.