Kwanini walevi wakiambiwa wamelewa wanachukia?

kaligopelelo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,764
3,940
Bila shaka wote humu ni wazima.
Na wale wenye changamoto za hapa na pale nizidi tu kuwaombea Kwa Allah awatatulie shida zao.

Moja Kwa moja niingie kwenye lengo la kuuliza swali langu hili ni Kama ifuatavyo.

Iko wazi kuwa Kila mtu anafurahia Kila anapofanya kitu ambacho anaona kiko sawa. Na mara nyingine haiwi aibu kujinadi Kwa watu kuwa yeye ni mtu wa namna gani. Mtu akila chakula kizuri haiwi aibu kwake Kama ataulizwa amekula nini ikawa hawezi kujibu wazi wazi.

Sio jambo la aibu Kwa mtu mswaliji kujibu narudi msikitini endapo ataulizwa ulikuwa wapi hali kadhalika wakristo nao watakujibu kuwa wanarudi kanisani bila aibu na Kwa furaha tele.

Iweje hawa walevi na wanywaji wanapenda kuvunga wanapoulizwa maswali inayoendana na taratibu na mazingira Yao Kwa muonekano wao wa nje?

Kwani ulevi kwao wao sio sehemu ya furaha?
Kwanini hawapendi kuambiwa kuwa wamelewa wakati kilabuni/bar wanaenda Kwa hiyari yao?
Kwani nyie walevi mnatuchukuliaje sisi tusiolewa katika jamii?

Naomba kuwasilisha swali langu Kwa masikitiko makubwa sana.

Ahsanteni...
 
Attachments

  • 9b5d3682f52ce38ff36c9c8bb73558f4.png
    9b5d3682f52ce38ff36c9c8bb73558f4.png
    27.4 KB · Views: 20
Uliza swali lako kwa nidhamu kijana, walevi ndio wanafanya barabara, reli , mahospitali, shule na huduma zote za jamii zinakufikia hapo ulipo.

Hao ndio wanaolipa mikopo mikubwa ya nchi, ndio maana nikasema kua na nidhamu ohooo.

Mlevi hata sheria ipo upande wake, akifanya kosa akiwa kwenye hali ya kilevi basi serikali inaweza hata kumsamehe, kwanini?? Kwasababu ni mlipakodi mwaminifu na makini kuliko wote nchi hii.

Karibu tupate kvant hapa.
 
Kumbe ndio maana hawapendi kuambiwa wamelewa
 
Utaniitaje mlevi wakati ndio mlipa kodi mkubwa nchi hii.Utaniitaje mlevi wakati nina usafiri binafsi,utaniitaji mlevi wakati watoto wangu wanasoma shule sio za kata,utaniitaje mlevi wakati nina nyumba ya kuishi nzuri tu,Utaniitaje mlevi wakati nimekuzidi wewe mnywa kahawa kijiweni,hebu nionyeshe maendeleo yako sababu tu hunywi.
Tuheshimiane braza usiingie anga zetu kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake nyie ndio mkiona mtu kaendelea huku anakunywa mnamuita ni FREE MASON.
WAITER ONGEZA K-VANT NA PELEKA MOJA MOTO MEZA ILE
 
Bila shaka wote humu ni wazima.
Na wale wenye changamoto za hapa na pale nizidi tu kuwaombea Kwa Allah awatatulie shida zao.

Moja Kwa moja niingie kwenye lengo la kuuliza swali langu hili ni Kama ifuatavyo.

Iko wazi kuwa Kila mtu anafurahia Kila anapofanya kitu ambacho anaona kiko sawa. Na mara nyingine haiwi aibu kujinadi Kwa watu kuwa yeye ni mtu wa namna gani. Mtu akila chakula kizuri haiwi aibu kwake Kama ataulizwa amekula nini ikawa hawezi kujibu wazi wazi.

Sio jambo la aibu Kwa mtu mswaliji kujibu narudi msikitini endapo ataulizwa ulikuwa wapi hali kadhalika wakristo nao watakujibu kuwa wanarudi kanisani bila aibu na Kwa furaha tele.

Iweje hawa walevi na wanywaji wanapenda kuvunga wanapoulizwa maswali inayoendana na taratibu na mazingira Yao Kwa muonekano wao wa nje?

Kwani ulevi kwao wao sio sehemu ya furaha?
Kwanini hawapendi kuambiwa kuwa wamelewa wakati kilabuni/bar wanaenda Kwa hiyari yao?
Kwani nyie walevi mnatuchukuliaje sisi tusiolewa katika jamii?

Naomba kuwasilisha swali langu Kwa masikitiko makubwa sana.

Ahsanteni...
Umewahi kukutana na kichaa ukamwambia "WEWE NI KICHAA?"
 
Walevi ni kama VIMBWENELEHI tu, yaani kijitu kifupi chafika magotini, halafu ukikiambia kuwa ni kifupi kinakupiga mangumi, ebo!!?
 
Kila mtu ana nadharia yake ya maisha katika jamii inayo tuzungukaa..
Lakini linakuja swala la nadharia kuu za iijamii ni yale makatazo ya Allah juu ya sheria zake ndani ya jamii hiyoo.

Au nizile kanuni sheria na amri za kidini ndani ya jamii hiyoo

Liponakuja swala la mtu kufanya kitu aidha binafs au la kijamii linapaswa pia lisiwe la aibuu..
Hapo tunajifunza kua watu wengi tunapenda kuisshi katika maisha ya kuipendeza jamiii ila pili ya kuipendeza mungu..

Hataka mtuu huyo atakua tofauti na kanuni au sheria za dini au jamii hatapenda kuonenaka ni mkosaji.

1.. hakuna binaadamu aliyewahi kupenda kutharirishwa katika ukosaji wake.
Ingawaje atapenda umwambie ukweli Tena kwa mazingira mengine yaliyo na hali ya utulivu na pasiwe na watu wengine wano muheshimu..

2.. hakuna anaejisifia kwa mabaya duniani kuwe yeye ndio bingwa wa kitu fulani ambacho jamiii au dini hazipendi..

Mf:- ulisha wahi kusukia mtu anakwambia

"Mimi mlevi bwana.. nimeshindikana au uliza mtaa mzima wananijua mi sifai yaani natishaa"

Isipokua kaulii hi itakua kinyume yaan itakua kauli taarifaa nafsi ya tatu umoja kwa wale walio soma kiswahili watanielewa..

"Yule mlevi bwana ...ameshindikana au uliza mtaa mzima wanamjua hafai yule anatisha".

Hapa utaweza kugundua aina hizi mbili za sentence..

Lakini pia neno mlevi limetumika kubebaa dhaana ya wavunjao sheria za kijamii katika maudhui ya maelezo yangu..

Tunaweza kutumia mwizi tapali Malaya jambazi mgomvi n.k

Kwa mantiki hi hatuwezi kukubali madhaifu yetu pale tuu mmoja ambae sio mwenye mapungufu mringano akakusoa ukakubali..

On the point na hitimisho..msubiri bombe zimtoke nenda ukamwambie kua sister au brother au dogo au uncle aisee janaa ulilewa sanaa.

Majibu utakayo yapata Bado yatakua katika utetezii wakee tuu.

Fikiria pia kuhusu mtuu mlevi kwanini awe analia akiwa amesha lewa.??

Fikiria pia kuongea lugha nyingine zaidi ya moja??

Fikiria pia kwanini awe anapiga makelele au kukeraa watu ovyoo.??

Fikiria pia hoja zao wanapo jadili mada fulani..

Nenda ukasome sheria na amri kumi za injili juu ya maisha ya mwaanaadamu.. ukikuta sehemu imeendikwa

usinywe pombe. Nilitee

Nenda soma nguzo tano za uislamu na usome nguzo sita za imani. Jumla nguzo kumi na moja..

Ukikuta waarabu wamekwambia usinywe pombe njo tujadili..

Wako jini mtuu

Mjenzi huru wa fikra yakinifu
ูˆู‡ุฐุงุณู„ู… ุนู„ูŠูƒ ูˆุฑุญู…ุชู„ู„ู‡
 
Back
Top Bottom