Kwanini walevi mitaani na hata vijijini wanaishi miaka mingi kuliko watu makini?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
Habari wadau

Kuna swali najiuliza sana.. kuanzia kijijini kwetu wale wazee walevi sana wengi bado wapo hai kazi kusumbua tu vilabuni kwa makelele na wana miaka zaidi ya 70 kibao

Kuja mtaani dar pia . Wale vijana wa zamani wategemea nyumba za urithi wengi wao walevi walevi tu.. wao ni double kick na konyagi kila siku na wapo hai na wana afya teleee...

Pia kuna wazee mabaharia wa zamani wengine makuli wa zamani nao wengi walevi walevi tu hapa mjini ila nao wapo hai wanaishi na afya tele huku kila siku wanalewa tu

Nikija kwa watu naowajua mimi ambao ni makini, watu wa dini, wao kila siku nasikia vifo vyao tu.


Swali kwa nini walevi wanaishi sana?
 
Stress mingi, unataka uwe na status huwezi unaishia kuugua, mara unafuatilia maneno ya watu, stess! Mkeo hakusuka vizuri stress, unataka gari nzuri stress! Unataka nyumba nzuri, stress! Bado hamjalogana na wafanyakazi wako na mabosi wenzio pumbaf!! Mkeo hajakupa limbwata na kimada anataka gari mpya, stress!

Mlevi akipiga gongo akalala mtaroni kwake kawaida tu! Sijui utamsema na nini ashtuke tena si ajabu anajiita mzungu wa roho hahahaaa! Lazima aishi sana tuu
 
Kwasababu walevi wengi hutowa ya moyoni yaani ukishalewa tu 100% maisha yako hapohapo yanakuwa ya ukweli. Ukitoa yalio moyoni husafisha sumu moyoni


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Walevi siku zote wanaishi maisha yao wapo huru na maisha yao hawana stress za ajabu ajabu na mara nyingi wao ni watu wa kufurahia maisha tu.Hii ni tofauti na vijana makini maana wana stress nyingi na hawana muda wa kuyaishi maisha.
 
KUPANGA NI KUCHAGUA,KAMA NA WEWE UNATAKA UNATAKA KUWA MLEVI UISHI MAISHA MAREFU,ITS UP TO YOU
 
Ukienda kwenye shamba la maua utaanza kuchuma yapi kwanza? bila shaka ni yale yaliyokomaa vizuri na yenye kupendeza .
hope umenielewa
 
Very simple, ni kwasababu hawanaga stress wao wanaishi kama mtoto mdogo, always wanafurahi na attention yao ipo kwenye kinywaji tuu.
 
Back
Top Bottom