Kwanini wakuu wa wilaya na mikoa wengi ni JWTZ na sio Polisi au Magereza?

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Kuna mtu jana au juzi alidokeza kwamba wakuu wengi wa wilaya na mikoa ni watu waliotoka JWTZ. Ila sijasikia wala kumuona mkuu wa mkoa au wilaya ambaye kitaaluma ni askari Polisi au Magereza, why?

Mwenye kujua ukweli huu anielewesha sababu wakuu, biafsi sijui wala kukukmbuka au kusikia kama ilishatokea askari polisi au magereza kuwa mkuu wa wilaya au magereza ktk nchi hii!
 
Halafu wengi wao ni weupe kichwani yani ni amri tu hawajui kingine, kama aliyemfukuza diwani wa cdm jukwaani wakati issue inawahusu wa tz wote, wapelekwe somalia ndio fani yao ingewa keep busy for the rest of their lives
 
Na kutoka usalama wa taifa na washkaji, labda kwa kuwa wanaongoza kamati za ulinzi na usalama.

Maendeleo wengi yamewashinda hata usalama wenyewe kwao moto, wizi, ujambazi na usalama barabarani si muhimu sana kama kulinda viongozi.

Jeshi inawezekana pia umri wa kustaafu ni mdogo kulinganisha polisi na magereza.
 
Polisi wangeweza kufanya kazi nzuri kuliko wanajeshi kwasababu wanajua kufanyakazi na wananchi zaidi. Sababu ya jeshi ni kitendawili!!
 
Kuna mtu jana au juzi alidokeza kwamba wakuu wengi wa wilaya na mikoa ni watu waliotoka JWTZ. Ila sijasikia wala kumuona mkuu wa mkoa au wilaya ambaye kitaaluma ni askari Polisi au Magereza, why?

Mwenye kujua ukweli huu anielewesha sababu wakuu, biafsi sijui wala kukukmbuka au kusikia kama ilishatokea askari polisi au magereza kuwa mkuu wa wilaya au magereza ktk nchi hii!
Ni wasiwasi wa Utawala kuogopa kupinduliwa
 
Nachukia sana hizi sera za CCM kulipana fadhila na kupeana vyeo. Wakuu wa mikoa miaka nenda rudi wao tuu! nchi hii hakuna watu wengine jamani? Kwanza Vyeo hivi vifutwe tuu mara mkuu wa Mkoa mara mkuu wa wilaya, mara mkurugenzi wa Mkoa khaaaaa kutafutiana tu ulaji
 
Kuna mtu jana au juzi alidokeza kwamba wakuu wengi wa wilaya na mikoa ni watu waliotoka JWTZ. Ila sijasikia wala kumuona mkuu wa mkoa au wilaya ambaye kitaaluma ni askari Polisi au Magereza, why?

Mwenye kujua ukweli huu anielewesha sababu wakuu, biafsi sijui wala kukukmbuka au kusikia kama ilishatokea askari polisi au magereza kuwa mkuu wa wilaya au magereza ktk nchi hii!
uhamiaji, zimamoto na mgambo vipi?
 
Muhimu weka ramani ya Tanzania hapa yenye mikoa

kisha weka dots nyekundu kuonyesha mikoa ipi imewekwa jamaa wa JWTZ kisha utapata jibu lako
 
Zamani ilikuwa mikoa na wilaya za mipakani,hilo lingeeleweka, lakini sasa hata maeneo ya kati ya nchi kunani?
 
Kamundu huna akili,kutumwagia maji ya kuwasha na pilipili ni akili hiyo au matope?
 
Polisi wangeweza kufanya kazi nzuri kuliko wanajeshi kwasababu wanajua kufanyakazi na wananchi zaidi. Sababu ya jeshi ni kitendawili!!

Mkuu hiki si kitendawili ni jambo la wazi kabisa. Unatakiwa kuelewa kuwa katika nchi zote ambazo civilian administration wanafanya fyongo jeshi ndio linakuwa la kwanza kuwarescue wananchi wasio na nguvu. Na mara nyingi kutokana na discpline ya jeshi hali baada ya wao kuchukua uongozi huwa inakuwa nafuu (not necesarry better). Jaribu kuangalia mfano wa Ghana na Nigeria.

Hapa Tanzania si bahati mbaya kuona wanajeshi wanachukuliwa na CCM, au wanateuliwa kwenye nyadhifa za kisiasa. Sababu ni kuwa wanajua jeshi lina uwezo wa kuwaondoa kiurahisi(si polisi au askari magereza0, kwa hiyo wanataka jeshi liwe sehemu yao, nalo limegewe keki kubwa. Ndio maana hata serikali ikifanya fyongo namna gani unasikia wanajeshi wanailinda [Shimbo], na siri zote za jeshi zinakuwa mikononi mwa chama.

Hapa Tanzania si jeshi tu hata usalama wa taifa nao wamemezwa na CCM, they work for CCM not for the country.
 
mijutu ya hovyo sana hii.huyo wa kahama ananitia kichefuchefu mpaka basi...yaaani linavaa suti na misandozi yake ya kichina
 
Fadhila ni muhimu hata cdm wakichukua nchi ni lazima sabodo wamwangalie kwa karibu sana ili kulipa fadhila
 
Back
Top Bottom