Kwanini wakina Fatuma Karume wafungue kesi Mahakama kuu hasa katika nyakati hizi za utawala wa awamu ya tano?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Hivi karibu taasisi tatu zinazojihusisha na utetezi wa sheria na haki za binadamu, zitafungua jumla ya kesi 10 ndani ya miezi mitatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kupinga sheria kandamizi zinazominya demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Taasisi hizo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

Taasaisi hizi wakishirikiana na watetezi wa demokrasia nchini wanafungua kesi katika nyakati ambazo.

Kwanza, wakurugenzi wa halmashauri ambao ni wasimamizi wa uchaguzi, wengi wao wameteuliwa wakiwa ni makada kindakindaki wa CCM.

Pili, wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wateule wa mwenyekiti wa CCM taifa kwa cheo cha urais, wanamaelekezo ya kutowatangaza wapinzani kuwa wameshinda kwa sababu aliyewateua, anayewalipa mshahara na magari anatokana na CCM.

Tatu, kuna matukio mengi yanayofanywa na wakurugenzi wa halmashauri (wasimamizi wa uchaguzi) yenye kuminya haki kwa vyama vya upinzani na kupendelea chama tawala CCM. Mathalani kunyimwa barua za utambulisho kwa mawakala wa chadema katika jimbo la kinondoni.

Nne, kukithiri kwa vitendo vya kiharifu kama mauaji, kukamatwa, kutekwa na kuumizwa kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani. Matharani mgombea udiwani wa kata ya Mhandu Mwanza na meneja kampeni wake walikamatwa na kupelekwa gereza kuu la Butimba Mwanza wiki mbili kabla ya uchaguzi ili kutoa mwanya kwa CCM kufanya kampeni. Huku washindani wa CHADEMA wakiwa gerezani.

Kati ya sheria ambazo wameanza kupambana nazo kwa kufungua kesi ili zifanyiwe marekebisho, ni Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Uchaguzi.

Wanaharakati hawa wanachukua hatua nyakati ambazo tubashuhudia unyama wa kutisha ukifanywa kwa viongozi wa upinzani, utekaji, ubambikiwazi kesi, mashambulizi ya risasi za moto, mauaji yamegeuka na kuwa sehemu ya utamaduni mpya wa siasa zetu.

Wakati haya yakiendelea viongozi wetu wakina mzee Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Warioba nk. Wamekaa kimya kabisa huku mambo yakiendelea kwenda mlama

Tayari wanaharakati wanaendelea na mapambano haya katika mamlaka za kisheria ( Mahakama), hata hivyo Fatuma Karume anasisitiza akisema, "Hatutakata tamaa kwenye hili," "Tumeshuhudia vitendo vingi ndani ya nchi vinavyowanyima wananchi demokrasia na uhuru wa kujieleza.Hii ni kinyume na katiba na ndiyo maana tumeunganika kupinga sheria hizo kwa mustakabali wa taifa"

Karume anasisitiza kuwa hawatakata tamaa, anasisitiza kuwa hatakata tamaa kwa sababu anajua fika kwamba sio rahisi watawala kufurahishwa na mapambano hayo. Hivyo wanaweza kuweka vizingiti na vikwazo vya kila namna.

Fatuma na wenzake wanafanya haya kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Ni muda muafaka wa kuwaunga mkono kwa kila namna ili kulinasua taifa letu na kila hila na uonevu.
 
Dhalimu DU hana hati miliki ya Tanzania. Tanzania ni ya Watanzania hivyo ni lazima kupambana naye ili kumpinga kuhusu udhalimu na dhuluma kubwa anayofanya nchini, ubaguzi, utekaji, upoteaji na uuaji wa Watanzania anaoufanya ni lazima upingwe kwa nguvu zote. Ukiukaji wake wa katiba, kudharau Bunge, mahakama, sheria za nchi, na kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge vyote ni lazima vipingwe kwa nguvu zote.

Alutta Continua! Continua!
 
Dhalimu DU hana hati miliki ya Tanzania. Tanzania ni ya Watanzania hivyo ni lazima kupambana naye ili kumpinga kuhusu udhalimu na dhuluma kubwa anayofanya nchini, ubaguzi, utekaji, upoteaji na uuaji wa Watanzania anaoufanya ni lazima upingwe kwa nguvu zote. Ukiukaji wake wa katiba, kudharau Bunge, mahakama, sheria za nchi, na kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge vyote ni lazima vipingwe kwa nguvu zote.

Alutta Continua! Continua!
Hasta la victoria siempre
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kati ya upinzani na CCM ni wepi viongozi na wanachama wake wengi wameuawa? Au roho za CCM hazina thamani?

Lini wakurugenzi hawakuwahi kuwa watu wa CCM?

Huu utaratibu umekuwepo hivi majuzi tu?

Kuna kipindi gani watanzania wengi wameuawa kwa pamoja katika mambo ya kisiasa kama ilivyofanyika kule Zanzibar?

Janjweed na mazombie wako Zanzibar mwaka wa ngapi huu mbona kesi kama hizo hazijafunguliwa.?

Akina Sheikh Farid na wenzake wana iaka mingapi leo? Mbona hawapigiwi kelele wala hakuna taasisi za kuwatetea?

Unafiki, unafiki unafiki. Unafiki huu ndio utafanya mambo yasifanikiwe kwani unafiki ni ugonjwa unaotafuna ndani kwa ndani. Wanafiki watajikuta wanafanyiana unafiki wao kwa wao
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Kwa yanayoendelea nchini MTU pekee anayeweza kupambana NAyo kwa vitendo ni Tundu Lissu. Pona haraka Lissu urudi kwenye mapambano kwani tumeelemewa kwa sasa
 
Back
Top Bottom