Kwanini Wakili Fatma Karume ataendelea kuwaangusha wanaharakati wenzake?

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
KWA NINI WAKILI FATMA KARUME ATAENDELEA KUWAANGUSHA WANAHARAKATI WENZAKE?

_Na Ally Jiriwa Esq._

Ukimsikiliza Wakili aliyesimamishwa Bi Fatma Karume utakubaliana nami kuwa wapinzani na wanaharakati wanaomtegemea wamepotea na wamepata pigo.

Kutoka wapinzani nchini kutetewa na mawakili wabobezi na "vichwa" kama akina Dr. Lamwai, Dr. Mvungi, Prof. Mwaikusa, Israeli Magafu hadi wakali wa masuala ya katiba kama Julius Ndyanabo na Mpare Mpoki hadi kuanza kuwatumia mawakili "vichwa maji" kama Fatma Karume ni anguko la kistratejia.

Leo nitaeleza sababu kadhaa, kwa kutumia kadhia ya juzi Fatma kusimamishwa uwakili, lakini kwa rejea ya kesi kadhaa alizozisimamia, kuonesha udhaifu wa uwakili wa Karume na udhaifu pia wa kesi za kiharakati anazosimamia.

*1 FATMA SI MBOBEZI KATIKA MASUALA YA KIKATIBA*

Hili wanaomjua wanawaonea huruma wanaoendekeza kumpa kesi za kikatiba, hana utaalamu, weledi wala uzoefu nazo.

Kwa miaka mingi ya uwakili wake tangu awe kwa Mkono Advocates hadi alipohamia IMMMA Advocates, Fatma amekuwa akishughulikia kesi za biashara na hasa mikataba ya madini na uwekezaji. Ambako amefaidika sana na huenda leo watu wa madini kubanwa na Serikali kunamuuma na kuwa hasidi dhidi ya Serikali.

Ndio maana tunamuona ghafla kawa wa kuropoka mitandaoni na kuonekana ana itikadi sawa ya pingapinga ya wapinzani na hata taasisi za haki za binadamu zinazoingiziwa hela kuendesha mashauri ya kikatiba nchini wanaingia mkenge kumpa kesi kubwa kubwa.

Yapo maeneo kwa kuongozwa na mawakili wengine anaokoteza vibaadhi ya orders au hukumu kamili, lakini maeneo mengi Fatma kwa kukosa ubobezi mahsusi ameanguka.

*2. HAJUI KUWA KATIBA INAMKINGA RAIS?*

Kwa kutokuwa na uzoefu katika masuala ya Katiba ndio sasa kaingia katika balaa la kufungua kesi ambayo Mahakamani inaitwa "frivolous case" yaani ya kuipotezea tu muda Mahakama.

Frivolous kesi ni zile unakwenda tu Mahakamani ama kula hela ya mteja au kujionesha tu upo lakini unajua kabisa hauna pointi za kisheria.

Mfano, kikatiba, na katika kesi nyingi tu nchini, ikiwemo ile maarufu ya Mwalimu Paul John Mhozya v AG ya 1993 enzi za Mwinyi, ni msimamo wa wazi wa Mahakama kuwa Rais anakinga kwa suala aliloliamua akiwa madarakani.

Fatma kaingia chaka Mahakamani kwenye kuhoji uteuzi wa Rais kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni uteuzi wa Rais kwa mujibu wa Katiba sasa unamshtaki vipi Rais eti kwa kuvunja Katiba. Haijui sayansi ya Katiba.

Akajikuta kakutana na mapingamizi ya kisheria yaliyokuwa na nguvu kutoka kwa Wanasheria wa Serikali na sasa kesi imefutwa na yeye na kijana wake wa ACT wametakiwa kulipa gharama zote za kesi. Lazima apaniki.

*3. HAJUI YEYE NI AFISA WA MAHAKAMA?*

Shida kubwa katika uwakili inayowasumbua mawakili wa kiharakati ni nidhamu.

Mfumo wa uwakili kote duniani umeweka nidhamu sana kuanzia katika mavazi na hata lugha za kimahakama.

Fatma Karume ana tatizo kubwa na nidhamu muda mrefu tu na amekuwa akikwaruzana na mawakili wenzake, mahakimu na hata majaji na maafisa wa mahakama.

Lakini hajui kuwa kwa mujibu Sheria ya Mawakili yeye ni Afisa anayetakiwa kuwa na nidhamu kubwa Mahakamani lakini amezoea kuogopwa.

Nadhani hamjui Jaji Feleshi, bingwa wa kuendesha mashataka anayejulikana nchini na mtu wa viwango na nidhamu. Yamemkuta.

*4. FATMA ATOFAUTISHE UWAKILI NA HARAKATI*

Kama nilivyosema hapo awali Mahakama zina taratibu zake sio mbwembwe.

Yapo maneno unaweza kuyaandika mitandaoni lakini huwezi kuyasema Mahakamani au kuyaandika kwenye plaint, writ, application au viapo (affidavits).

Kuandika kwenye kiapo maneno mazito tena ya uongo na kuituhumu Mahakama eti unaiambia "nikishindwa kesi hii leo, nitaendelea kupambana nanyi 2020 au 2025 kwani nyie majaji mlioteuliwa na Magufuli mtakuwa hampo."

Ni dharau kubwa tena kwa wakili ambaye juzi tu katoka kashinda kesi ya Wakurugenzi kuzuiwa kusimamia uchaguzi tena akishinda mbele ya majaji hao hao "wa Magufuli" anaowatusi leo baada ya kuona katika kesi hii hoja za kisheria zimembana.

*5. HAJUI KUWA JAJI ANAWEZA KUMSIMAMISHA UWAKILI?*

Nimesoma matusi na dharau ambazo Fatma ameziandika kwa Mahakama na anaendelea kuzisema hadharani.

Namfahamu Jaji Feleshi na nikasema mawakili tumekosea wapi, tunakwama wapi?

Inaonekana Fatma hakujua kuwa Sheria ya Mawakili inampa Jaji iwezo wa moja kwa moja wa kumsimamisha Wakili kazi na kisha kulipeleka suala lake kwenye Kamati ya "roho mbaya" ya Nidhamu za Mawakili?

Hakujua, Jaji anao uwezo huo tena bila kupepesa macho. Lakini pia ukimsikiliza Fatma anavyolalama mitandaoni kabisa unaona kuwa hakujua hili maana analalamika Jaji hakumsikiliza.

Kwenye Sheria ile ya Mawakiki Jaji ana uwezo wa kutoa uamuzi huo kisha akalipeleka suala husika kwenye Kamati ya Mawakili ambako ndiko mlalamikiwa atasikilizwa.

Fatma wa kesi za mikataba na Fatma mtoto wa Rais aliyekuwa akitukana Mahakimu na Majaji, kuvaa vikukuu mguuni akiwa kortini na kuogopwa akibaki kuangaliwa tu hajui hizi process kwa sababu alikuwa juu ya sheria wakati mawakili wengi wakisimamishwa tu kwa makosa mbalimbali huko nyuma. Leo ataona anaonewa na wafuasi wake watamshangilia kuwa kaonewa.

*6. MATUSI, UZUSHI NA UMBEA WA MITAANI KORTINI?*

Nilisema hapo juu kuwa kesi yake yenyewe ya kuhoji uwezo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na uteuzi wa Rais ni frivolous unless anabifu binafsi na Prof. Kilangi na Rais.

Maana hata hoja zake zinajikanganya..eti anasema Kilangi si Wakili mzoefu katika Mahakama hivyo anatoa ushauri mbovu akiwa AG.

Huyu dada aombewe..kwanza ajue AG sio lazima awe wakili ni Mwanasheria Mkuu wa serikali.

AG anasifa za Kikatiba na kwamba lazima awe Mwanasheria sio lazima wakili hata hivyo Kilangi pia ni wakili.

Pili anakwenda kuongoza taasisi yenye wataalamu mbalimbali chini yake. Mwanasheria Mkuu ni taasisi sio mtu.

Tatu, AG hamtumikii Fatma ni mshauri wa Serikali sasa yeye Fatma lini kaona na wapi kajiridhisha kuwa kuba ushauri mbovu wa AG?

Lakini kama AG anatoa ushauri mbovu si ndio ingekuwa furaha kwa Fatma na wanaharakati wenzake kutumia kutumia ubovu huo kufanya siasa zao? Sasa vipi anakwenda kortini kuisaidia Serikali anayoipinga kila siku?

*7. SASA ANAKWENDA KWENYE KAMATI YA WATAALAMU WA NIDHAMU ZA MAWAKILI*

Nimemsikia jana akisema hakusikilizwa na Jaji Feleshi na akamrushia madongo kadhaa.

Sasa suala lake linakwenda kwenye Kamati ya Mawakili kujadiliwa zaidi ambako atasikilizwa na anaweza kurejeshewa uwakili wake au kufutwa kabisa moja kwa moja.

Ubaya wa matusi ni huku nje ndani ya taratibu najua atakwenda akiwa mnyonge na akumbuke Kamati hiyo ina majaji (aliowatukana) na mjumbe kutoka ofisi ya AG (anayoitusi) na kuna mawakili wenzake (anaowadharau kila siku hasa alipokuwa mtoto wa Rais).

Kwa kifupi tu amelalamikia kusikilizwa, huko kwenye Kamati, kama Jaji Feleshi alivyohukumu, atapelekwa na atasikilizwa kwa kina tu.

Ushauri wangu: kule akatoe hoja za kisheria kama anazo kutetea dharau na matusi yake kwa Mahakama au akaombe radhi kama ni muungwana, la sivyo akiendeleza tabia yake ya kufokea watu, kudharau wenzake kwa sababu tu ya hadhi yake ya kifamilia akijisahau kwamba yeye ni Afisa wa Mahakama, akaendeleza umbea, uzushi na vijineno vya mitaani, nabashiri, yatamkuta makubwa zaidi.

Alamsiki.
 
Angeendelea kukaa ofisini akiandika na kushauri kuhusu mikataba. Kama anataka kuwa wakili hasa wa kusimama kortnini, anatakiwa akubali kubadilika pakubwa sana.

Mwisho aachane na hizi harakati za kisiasa kwani zinamharabia mazima. Fatma hana utashi na Stamina ya kuchanganya Siasa na taaluma yake, anajiharibia sana.

Nimemsikia akiongea kwa kujiuliza kama aingie kwenye siasa au laah, mimi katika siasa wala simshauri, hajafanya chochote cha maana au cha kipuuzi kwenye siasa na jamii kiasi cha kuweza kufikiri anaweza kuingia kwenye siasa na kuzimudu.

Kinachombeba ni jina la baba yake tu basi.
 
Yaani haka kataaluma nyenzo kuu ni lugha na mwonekano Bora niendelee na kilimo cha mchicha siku 21boom
 
Jina la baba yake lilikua linambeba sana ,Chadema wakazani atafaidika nao
 
Hata mimi bibie huyu ananitatiza sana kumuelewa
Anachanganya sana madesa wakati mwingine
 
KWA NINI WAKILI FATMA KARUME ATAENDELEA KUWAANGUSHA WANAHARAKATI WENZAKE?

_Na Ally Jiriwa Esq._

Ukimsikiliza Wakili aliyesimamishwa Bi Fatma Karume utakubaliana nami kuwa wapinzani na wanaharakati wanaomtegemea wamepotea na wamepata pigo.

Kutoka wapinzani nchini kutetewa na mawakili wabobezi na "vichwa" kama akina Dr. Lamwai, Dr. Mvungi, Prof. Mwaikusa, Israeli Magafu hadi wakali wa masuala ya katiba kama Julius Ndyanabo na Mpare Mpoki hadi kuanza kuwatumia mawakili "vichwa maji" kama Fatma Karume ni anguko la kistratejia.

Leo nitaeleza sababu kadhaa, kwa kutumia kadhia ya juzi Fatma kusimamishwa uwakili, lakini kwa rejea ya kesi kadhaa alizozisimamia, kuonesha udhaifu wa uwakili wa Karume na udhaifu pia wa kesi za kiharakati anazosimamia.

*1 FATMA SI MBOBEZI KATIKA MASUALA YA KIKATIBA*

Hili wanaomjua wanawaonea huruma wanaoendekeza kumpa kesi za kikatiba, hana utaalamu, weledi wala uzoefu nazo.

Kwa miaka mingi ya uwakili wake tangu awe kwa Mkono Advocates hadi alipohamia IMMMA Advocates, Fatma amekuwa akishughulikia kesi za biashara na hasa mikataba ya madini na uwekezaji. Ambako amefaidika sana na huenda leo watu wa madini kubanwa na Serikali kunamuuma na kuwa hasidi dhidi ya Serikali.

Ndio maana tunamuona ghafla kawa wa kuropoka mitandaoni na kuonekana ana itikadi sawa ya pingapinga ya wapinzani na hata taasisi za haki za binadamu zinazoingiziwa hela kuendesha mashauri ya kikatiba nchini wanaingia mkenge kumpa kesi kubwa kubwa.

Yapo maeneo kwa kuongozwa na mawakili wengine anaokoteza vibaadhi ya orders au hukumu kamili, lakini maeneo mengi Fatma kwa kukosa ubobezi mahsusi ameanguka.

*2. HAJUI KUWA KATIBA INAMKINGA RAIS?*

Kwa kutokuwa na uzoefu katika masuala ya Katiba ndio sasa kaingia katika balaa la kufungua kesi ambayo Mahakamani inaitwa "frivolous case" yaani ya kuipotezea tu muda Mahakama.

Frivolous kesi ni zile unakwenda tu Mahakamani ama kula hela ya mteja au kujionesha tu upo lakini unajua kabisa hauna pointi za kisheria.

Mfano, kikatiba, na katika kesi nyingi tu nchini, ikiwemo ile maarufu ya Mwalimu Paul John Mhozya v AG ya 1993 enzi za Mwinyi, ni msimamo wa wazi wa Mahakama kuwa Rais anakinga kwa suala aliloliamua akiwa madarakani.

Fatma kaingia chaka Mahakamani kwenye kuhoji uteuzi wa Rais kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni uteuzi wa Rais kwa mujibu wa Katiba sasa unamshtaki vipi Rais eti kwa kuvunja Katiba. Haijui sayansi ya Katiba.

Akajikuta kakutana na mapingamizi ya kisheria yaliyokuwa na nguvu kutoka kwa Wanasheria wa Serikali na sasa kesi imefutwa na yeye na kijana wake wa ACT wametakiwa kulipa gharama zote za kesi. Lazima apaniki.

*3. HAJUI YEYE NI AFISA WA MAHAKAMA?*

Shida kubwa katika uwakili inayowasumbua mawakili wa kiharakati ni nidhamu.

Mfumo wa uwakili kote duniani umeweka nidhamu sana kuanzia katika mavazi na hata lugha za kimahakama.

Fatma Karume ana tatizo kubwa na nidhamu muda mrefu tu na amekuwa akikwaruzana na mawakili wenzake, mahakimu na hata majaji na maafisa wa mahakama.

Lakini hajui kuwa kwa mujibu Sheria ya Mawakili yeye ni Afisa anayetakiwa kuwa na nidhamu kubwa Mahakamani lakini amezoea kuogopwa.

Nadhani hamjui Jaji Feleshi, bingwa wa kuendesha mashataka anayejulikana nchini na mtu wa viwango na nidhamu. Yamemkuta.

*4. FATMA ATOFAUTISHE UWAKILI NA HARAKATI*

Kama nilivyosema hapo awali Mahakama zina taratibu zake sio mbwembwe.

Yapo maneno unaweza kuyaandika mitandaoni lakini huwezi kuyasema Mahakamani au kuyaandika kwenye plaint, writ, application au viapo (affidavits).

Kuandika kwenye kiapo maneno mazito tena ya uongo na kuituhumu Mahakama eti unaiambia "nikishindwa kesi hii leo, nitaendelea kupambana nanyi 2020 au 2025 kwani nyie majaji mlioteuliwa na Magufuli mtakuwa hampo."

Ni dharau kubwa tena kwa wakili ambaye juzi tu katoka kashinda kesi ya Wakurugenzi kuzuiwa kusimamia uchaguzi tena akishinda mbele ya majaji hao hao "wa Magufuli" anaowatusi leo baada ya kuona katika kesi hii hoja za kisheria zimembana.

*5. HAJUI KUWA JAJI ANAWEZA KUMSIMAMISHA UWAKILI?*

Nimesoma matusi na dharau ambazo Fatma ameziandika kwa Mahakama na anaendelea kuzisema hadharani.

Namfahamu Jaji Feleshi na nikasema mawakili tumekosea wapi, tunakwama wapi?

Inaonekana Fatma hakujua kuwa Sheria ya Mawakili inampa Jaji iwezo wa moja kwa moja wa kumsimamisha Wakili kazi na kisha kulipeleka suala lake kwenye Kamati ya "roho mbaya" ya Nidhamu za Mawakili?

Hakujua, Jaji anao uwezo huo tena bila kupepesa macho. Lakini pia ukimsikiliza Fatma anavyolalama mitandaoni kabisa unaona kuwa hakujua hili maana analalamika Jaji hakumsikiliza.

Kwenye Sheria ile ya Mawakiki Jaji ana uwezo wa kutoa uamuzi huo kisha akalipeleka suala husika kwenye Kamati ya Mawakili ambako ndiko mlalamikiwa atasikilizwa.

Fatma wa kesi za mikataba na Fatma mtoto wa Rais aliyekuwa akitukana Mahakimu na Majaji, kuvaa vikukuu mguuni akiwa kortini na kuogopwa akibaki kuangaliwa tu hajui hizi process kwa sababu alikuwa juu ya sheria wakati mawakili wengi wakisimamishwa tu kwa makosa mbalimbali huko nyuma. Leo ataona anaonewa na wafuasi wake watamshangilia kuwa kaonewa.

*6. MATUSI, UZUSHI NA UMBEA WA MITAANI KORTINI?*

Nilisema hapo juu kuwa kesi yake yenyewe ya kuhoji uwezo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na uteuzi wa Rais ni frivolous unless anabifu binafsi na Prof. Kilangi na Rais.

Maana hata hoja zake zinajikanganya..eti anasema Kilangi si Wakili mzoefu katika Mahakama hivyo anatoa ushauri mbovu akiwa AG.

Huyu dada aombewe..kwanza ajue AG sio lazima awe wakili ni Mwanasheria Mkuu wa serikali.

AG anasifa za Kikatiba na kwamba lazima awe Mwanasheria sio lazima wakili hata hivyo Kilangi pia ni wakili.

Pili anakwenda kuongoza taasisi yenye wataalamu mbalimbali chini yake. Mwanasheria Mkuu ni taasisi sio mtu.

Tatu, AG hamtumikii Fatma ni mshauri wa Serikali sasa yeye Fatma lini kaona na wapi kajiridhisha kuwa kuba ushauri mbovu wa AG?

Lakini kama AG anatoa ushauri mbovu si ndio ingekuwa furaha kwa Fatma na wanaharakati wenzake kutumia kutumia ubovu huo kufanya siasa zao? Sasa vipi anakwenda kortini kuisaidia Serikali anayoipinga kila siku?

*7. SASA ANAKWENDA KWENYE KAMATI YA WATAALAMU WA NIDHAMU ZA MAWAKILI*

Nimemsikia jana akisema hakusikilizwa na Jaji Feleshi na akamrushia madongo kadhaa.

Sasa suala lake linakwenda kwenye Kamati ya Mawakili kujadiliwa zaidi ambako atasikilizwa na anaweza kurejeshewa uwakili wake au kufutwa kabisa moja kwa moja.

Ubaya wa matusi ni huku nje ndani ya taratibu najua atakwenda akiwa mnyonge na akumbuke Kamati hiyo ina majaji (aliowatukana) na mjumbe kutoka ofisi ya AG (anayoitusi) na kuna mawakili wenzake (anaowadharau kila siku hasa alipokuwa mtoto wa Rais).

Kwa kifupi tu amelalamikia kusikilizwa, huko kwenye Kamati, kama Jaji Feleshi alivyohukumu, atapelekwa na atasikilizwa kwa kina tu.

Ushauri wangu: kule akatoe hoja za kisheria kama anazo kutetea dharau na matusi yake kwa Mahakama au akaombe radhi kama ni muungwana, la sivyo akiendeleza tabia yake ya kufokea watu, kudharau wenzake kwa sababu tu ya hadhi yake ya kifamilia akijisahau kwamba yeye ni Afisa wa Mahakama, akaendeleza umbea, uzushi na vijineno vya mitaani, nabashiri, yatamkuta makubwa zaidi.

Alamsiki.
Mkuu kwani lazima awe wakili? Msimtishe kazi ni nyingi hapa duniani
 
Back
Top Bottom