Kwanini wakihamia CCM ndio iwe wamenunuliwa kwani Chadema mnauza hisa?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,753
2,000
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukila nyama ya mtu huwezi kuacha utaendelea tu, na hii ndio inayowatokea wapinzani leo. Tujikumbushe tu 2010 Chadema walimlazimisha Dr Slaa agombee urais baada ya rip Sitta kuwatosa dakika za lala salama, na yeye Slaa akatoa masharti yake ya " kimaslahi" endapo angeshindwa kuwa Rais. Baada ya kushindwa katibu mkuu Slaa akawa analipwa maslahi kama ya mbunge ilhali yeye siye. Kituko kingine ni uchaguzi wa 2015 pale Kigoma baada ya kujua wameshachokwa kwenye majimbo yao, Zitto wa ACT na Serukamba wa CCM wakabadilishana majimbo na kufanikiwa kurejea mjengoni. Kwahiyo hii michezo ya wanayotuchezea wanasiasa bila kujali mzigo wa gharama wanaoitwisha serikali ama kwa kutumia vibaya ruzuku au kurudia chaguzi iliasisiwa na wapinzani wenyewe. Leo unasemaje mbunge anayejiunga na CCM amenunuliwa wakati wewe juzi tu umekesha na mbunge wa CCM Nairobi na aliporejea tu nchini akatangaza kuhamia Chadema. Binafsi sipingani na mbunge kuhama kwani hiyo ni haki yake ya kikatiba, kinachoumiza ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi kwa kurudia chaguzi ilhali kuna wanafunzi wamekosa " mikopo" kutokana na ufinyu wa bajeti. Ni upunguani tu kumshutumu mbunge aliyehamia CCM na kumshangilia yule aliyehamia Chadema wakati wote wawili wametenda dhambi ile ile ya kuwasaliti wananchi waliowapigia kura au wanaokuja Chadema wananunua hisa maana ni mabepari nyie. Niwe mkweli katika hili la wanasiasa kuiingiza serikali katika matumizi yasiyo ya " haki" ya bajeti kwa kugharamia chaguzi ndogo, nasema Tanzania kwanza vyama baadae. Nawasilisha!
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,469
2,000
Kwa nini wakihamia CCM wanasema wanamuunga mkono Pombe Magufuli ilihali hamna la maana alilolifanya?
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,844
2,000
Kipi kipya kutoka kwa magufuli na CCM yake?
Kama maisha ni Yale Yale.
Umasikini ULE ULE.
maendeleo ya speed ya Kobe.
Uchumi unashuka.
Demokrasia hamnaa.
Wanasiasa wanataka kuuawa.
Kwenye uchaguzi mnatumia ubabe
WANACHOMUUNGA NI NINI?
kama mafisadi CCM ndo kwao
WANAMUUNGA MKONO KUPAMBAN na MAFISADI GANI?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom