Kwanini Wakenya wengi humsifia Rais Dkt. John Magufuli?

M
Ulishawahi kumsikia akiizungumza, au unakisia tu?

Mimi nilishawahi kumsikia, na kwa hakika niliyosikia ilinipa ushahidi tosha kwamba haijui hiyo lugha.
Mkuu Kalamu naona tuko lindo night Kali😂😂

Yule Bwana ana lafudhi ya kisukuma TU KATIKA hicho KIINGEREZA....

By da way HIVI NI WATANZANIA WANGAPI HATA WENYE PHDS WANAOONGEA KIINGEREZA KWA MIZANIA YA fluency?!!!

Kiswahili TU watu ndo hivyo,Leo ijekuwa lugha ya mwenzako?!!!
 
Wasomi wa Tanzania.
Kenya iliyoingia Kipato cha Kati mwaka 2013, tumeizidi?
Unajua Bajeti ya Kenya kwa mwaka ni mara ngapi ya Bajeti ya Tanzania?
Usiongelee usiyoyajua.
mkuu mi nimesema ukuaji wa uchumi tu megine ni ya Wakenya!!’, what i know ni kuwa Magufuli anapindua meza na tayari amewasha indiketa!!! sasa Wakenya watapisha watake wasitake Tanzanite na Dhahabu si zao tena!!
 
mkuu mi nimesema ukuaji wa uchumi tu megine ni ya Wakenya!!’, what i know ni kuwa Magufuli anapindua meza na tayari amewasha indiketa!!! sasa Wakenya watapisha watake wasitake Tanzanite na Dhahabu si zao tena!!
Itapendeza sana tukizungumzia ya nchi yetu ya Tanzania.
Nafurahia upendo ulionao kwa nchi yetu.
Lakini unakosea unapoitaja nchi nyingine ambayo huijui. Nchi ambayo tayari inauza mafuta, "crude petroleum" duniani.
Ni kweli kabisa hata mimi sifurahii kuona dawa za miswaki, na muswaki toka Kenya zimejaa kwetu, wakati sisi tunachopeleka kwao ni nafaka na Matunda, kwa maana ya "un processed products"!!
Hii maana yake ni kwamba Tanzania ya Viwanda iko nyuma " kiviwanda" kuliko Kenya.
Lakini iko siku!!
 
sababu wanakijua kikombe kwa nje,ni hadi waje walalie kitanda ndo watajua kunguni wake
 
Mleta mada kuna Kiongozi aliyekuwa anasifiwa na waafrika kama Mugabe???? Je nchini kwake ilikuwaje?? Mwisho wake ulikuwaje?

kuna kiongozi alikuwa anasifiwa na waafrika kama Gaddafi?? Je nchini kwake hali ilikuwaje hasa mtazamo wa wananchi wake juu yake??? Na mwisho wake ulikuwaje???

Mnapotoa pambio zenu za kusifu na kuabudu jiulizeni Pia kwa wengine ilikuwaje?
madikteta wote uzuia mabaya yao yasijulikane nje
 
Akiaifiwa mnapata bichwaaaa!!! Zile siyo sifa funguka!!!!

Yaani wanashangilia anavo didimiza uchumi wetu.Kuteka na kuua watanzania hovyo. wanampa hapohapo mzeeee! Na renyewe halijiulizi why???

Walijua atakufa faster tu kucheza na kitumbua cha mabeberu.

Rais lazima asafiri mara kibao akaemee wewe!! Akae tu humu akimbizane na vitu vidogo! machinga mtakula nini?

Shida zako hizo unahesabu vijisafari na tu suti twa Rais????!! Hizo shida zako usituletee humu! Ukome kabisaaa!
Suti tu nikiwa mdogo nilikuwa nabadili kila jumamosi navaa tofauti mwaka mzima sembuse Rais??? Cammon be seriousy!!!

Rais lazima aondoke akatembeze kopo! Kukidhi haja zenu nyambaf! Mna nini humu africa? ??? Kuombaomba tuuu!! Hizo fedha anazoitumia mmezichapa wapi???

Unadhani wanapenda kupaa????.kwa umaskini wako huo unaona kupanda pipa rahaaaa!!! Wanabembea??? Mtu km uhuru k.amezaliwa kwenye mafuta ya rojo ikulu tena mara baada ya mkoloni amekuzwa na mabaki ya mkoloni!!! Nini hajui???
au hujui?? Yaani kwao mapipa ya private jet ni km uchochoro!!! Hana ulimbukeni wa hivo! Anafanya kazi.

Ebu nambie mara ya mwisho ulipanda ndege lini weye????
 
KWANINI WAKENYA HUMSIFIA RAIS MAGUFULI?

Na Thadei Ole Mushi

Tumekuwa tukiona Mara kwa Mara Prof Lumumba wa Kenya akimsifia Sana Rais Magufuli. Watu wengi hujiuliza kanunuliwa? Au ana interest gani na Rais Magufuli au na Tanzania? Leo nitawapitisha katika eneo Moja tu la kwa Nini huwa wanaona Mh Magufuli ni Rais Bora wa kipindi hiki wakilinganisha na wa kwao Uhuru Kenyata. Twende sawa.

David Ndii mwanauchumi wa Kenya aliwahi kusema Kuna haja ya kutafiti kama Ziara za Rais Kenyatta nje ya Nchi zina Manufaa. Duru za Kibajeti nchini Kenya zinaonyesha kuwa Rais Kenyata ametumia matrilioni ya Shilingi katika safari zake nje ya Nchi.

Kwa miaka sita tu Rais Kenyata kufikia 2019 alikuwa ameshakwea pipa Mara 92 kuhudhuria shughuli mbalimbali nje ya nchi shughuli nyingi zikiwa Ni kuaapishwa na kutafuta Mikopo kwenye mataifa ya Kibepari.

Mwaka 2015 pekee Rais Kenyata alisafiri safari 21 katika mwaka mmoja. Kwa miaka mitano ya Kwanza Kenyata alisafiri zaidi ya Mara 43 nje ya Nchi huku mtangulizi wake Mwai Kibaki kwa miaka 10 alisafiri Mara 33 tu. Wachambuzi wa Mambo nchini Kenya wanakosoa vikali Sana Kitendo Cha Rais Kenyata kusafiri Mara kwa Mara na kuligharimu Taifa Hilo mabilioni ya Shilingi.

Hali ipoje kwa Tanzania?

Kwa miaka Mitano Rais Magufuli katoka nje ya mipaka Mara 8.

Safari ya kwanza aliifanya Tarehe 6-8 Mwezi wa nne mwaka 2016 ambapo nchi ya kwanza kuitembelea ilikuwa Rwanda. Siku ya kwanza Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Rais Kagame mpakani Rusumo ambapo walizindua one stop border na kufungua Daraja la Rusumo. Siku ya Pili Rais Magufuli alihudhuria maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.

Safari ya Pili alikwenda Uganda ambapo alisafiri Tarehe 12 Mwezi wa tano 2016. Wakati Rais akipanga kwenda Uganda Mezani kulikuwa na mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa Ant-Corruption uliokuwa ufanyike London Ila alikataa mwaliko huo akaelekea zake Uganda kwa Jirani yetu Museven. Lengo la Safari hii ilikuwa Ni mazungumzo ya Bomba la mafuta toka Uganda kuja Tanzania. Wakati Kenyata anarudi akakuta tayari Rais Magufuli na Museven washasinishiana mkataba.

Safari ya Tatu Rais Magufuli alitembelea Kenya kwa Jirani Mwingine hii ilikuwa safari ya Mwisho kwa mwaka 2016 ambapo alisafiri Tarehe 31-1 Mwezi wa kumi. Ziara ya siku Mbili. Safari hii ilikuwa na lengo la kuimarisha biashara ya Kenya na Tanzania.

Safari ya nne ilifanyika 2017 ambapo Rais Magufuli alielekea Ethiopia Tarehe 29-2 Mwezi wa pili. Mh Rais alihudhuria mkutano wa 28 wa nchi za Africa. Hii ilikuwa safari yake ya kwanza njee ya Africa Mashariki toka awe Rais.

Mwaka huo huo 2017 Tarehe 9-11 Mwezi November Rais Magufuli alifanya Ziara ya tano ambapo alisafiri kwenda Tena Uganda. Uganda ndio nchi pekee ambayo ilipata bahati ya kutembelewa na Rais Magufuli Mara mbili. Hakuna nchi nyingine kwa kipindi Cha miaka mitano umepata bahati hiyo. Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Mtukula ambapo walizindua one stop border na baadaye alielekea Ruzingwa kuweka jiwe la Msingi la bomba la mafuta. Mwaka 2017 alifanya Ziara mbili tu na hii ilikuwa Ni ya Mwisho kwa mwaka huo.

Mwaka 2018 Rais Magufuli hakutoka kabisa nchini.

Mwaka 2019 Rais Magufuli alifanya Ziara ya sita ambapo alihudhuria kuapishwa kwa Cyril Ramaphosa Africa Kusini Tarehe 25-26 Mwezi wa tano. Kwenye Ziara hii waliongozana na Rais Kikwete kwenye ndege Moja.

Ziara ya Saba aliifanya Namibia wakati akirudi toka Afrika Kusini ambapo alipitia Namibia. Hii ilikuwa Tarehe 27-29.

Ziara ya Mwisho kabisa aliifanya kipindi hicho hicho akirudi nyumbani tokea Afrika Kusini ambapo alipitia Zimbabwe Tarehe 29-30
Mwezi wa tano. Hii ni Ziara yake ya nane.

Safari za Rais hugharimu Nini?

Wakati wa JK alipokuwa akisafiri kila safari moja ya nje alikwenda na watu 50. Hawa walikuwa wanausalama, waandishi wa habari, na watendaji mbalimbali wa serikali kutegemeana na Safari.

Kila Mtu kwenye safari moja alilipwa kiasi cha chini dola 400 kwa Siku. Huyu ni ofisa wa ngazi za chini kabisa.

Gharama za Kila safari ilikuwa inategemea ni sehemu gani Rais anakwenda. Mfano nchi za Ulaya na America posho kwa siku hulipwa kwa Daraja A ambazo ni Dola 420 kwa Siku kwa mtu mmoja.

Nchi za Asia na Africa hulipwa daraja B ambapo hulipwa dola 380 kwa siku.

Kwa hiyo kama safari itachukua siku tano utazidisha dola hizo Mara tano.... Iwe ni kwa daraja A Au B.

Gharama hizi hazijumuishi kitu kinachoitwa pocket Money,Nauli, Fedha za Suti kwa kila Safari nk. Yaani kila safari ni lazima vitu hivyo viwepo.

Mfano Leo wakienda Kenya lazma upate Suti kesho wakienda Uganda unapata nyingine. Vivyo hivyo kwa mahitaji mengine.

Hili ni eneo ambalo tulikubaliana kwenye Ilani yetu ya chama Kuwa tutalidhibiti ili fedha hizi tuzitumie kuondoa umaskini wa watanzania.

Ole Mushi
0712702602

Wamezoea unyapara.
 
Back
Top Bottom