Kwanini wakati wa mfungo wa Ramadhani biashara nyingi hudorora?

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,331
14,257
Bhandugu,

Kama kichwa kinavyosema.

Hivi ni kwanini kipindi cha mfungo biashara mbalimbali (isipokuwa zinazohusika kutengeneza futari) huwa zinakwenda vibaya? Yaani nenda bar mambo huwa sio shwari kabisa, nenda kule kwa mkuu wa meza huko ni kulala siku mbili na kuendelea, sijui ni kwanini?.

Cha ajabu baada ya mfungo kuisha mambo huwa yanakuwa bam! bam! Yaani mimi sijui ni kwanini hebu tupeana elimu ni kwanini inakuwa hivyo?

Karibuni sana wadau: Matusi, kejeli, dharau, havina nafasi kama una hasira vaa barakoa nawa mikono kwa maji na sabuni zitaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waislamu ni wengi sans hapa Tanzania kuliko waumini wa dini zengine.
Hii sio sababu ya msingi, hata kama wangekuwa 20%ya wakazi wa Dar, inapofika mwezi mtukufu, 20%ikitoka, kwa kuacha kula hotelini, lazima impact kwenye biashara itaonekana na biashara zinazodorola zaidi ni za vyakula.

Nilikuwa Zenji wakati mfungo unaanza, asubuh hoteli zote, masupermarket yamefungwa, ila biashara za simu, nguo zinaendelea kama kawaida.

Na wingi sio hoja, UK ipo kama Dar tu, lakini iliitawala Dunia na wanatupa misaada,
Ukwasi wa watu 1000 hapa bongo ndio ukwasi wa mtu mmoja UK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waislamu ni wengi sans hapa Tanzania kuliko waumini wa dini zengine.
Maweeee!
65% ya Watanzania ni Wakristo. Uko dunia gani wewe?

Waislamu ni rahisi kuwafanyia sensa kuliko unavyofikiri, mna maeneo yenu mmejazana (sitayataja) ukifika hadi unaboeka yani unahisi uko Somalia.

Mwanza inakadiriwa kuwa na watu million 2 na point alafu laki sita ni wakatoliki tu sasa jiulize madhehebu mengine yana wangapi na imani yako ina wangapi
 
Mwaka 2014 Jimbo la Kigoma Iina eneo la kilomita za mraba 45 066 kukiwa na idadi ya watu milioni
2, ambao kati yao 515 701 ni Wakatoliki.

Ndugu Shaibu Kigoma kwenye maulamaa kuna wakatoliki laki tano je Lutheran, Anglican, AICT na makanisa ya ki-pentecostal?
 
Waislamu ni wengi sans hapa Tanzania kuliko waumini wa dini zengine.
By 2018 kwa sensa inayofanywa na makanisa yenyewe ili kujua waumini wao ni wangapi na ni very easy kujua.

Wakatoliki na Walutheri walikuwa zaidi ya 20 million na Mbatia alisema hili hadharani.
 
Back
Top Bottom