Kwanini wakala wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money hawataki pesa itolewe na mtu wa mbali?

Kutoa hela mbali haikubaliki kwa sababu matapeli wanatumia hii mbinu kuiba:

Tapeli yupo Mwanza, wala haendi kwa wakala, anawasiliana na tapeli mwingine Dar na kumwambia aende kwa wakala. Huyu tapeli wa Mwanza anapewa details za wakala - namba ya kutolea hela, anafanya mwamala kutoa hela kwa wakala aliyepo Dar. Transaction inafanyika Mwanza, hela anachukua tapeli aliyepo Dar. Baada ya tapeli aliyepo Dar kuchukua hela, huyu tapeli wa Mwanza anapiga simu kwenye mtandao husika, tuseme Tigo, na kuwaambia kuwa amekosea kutoa hela anaomba irudishwe.

Wahudumu wa mtandao husika wakiangalia kwenye mfumo wao wataona ni kweli huyu mtu yupo Mwanza lakini amefanya transaction ambayo imeenda kwa wakala aliyepo Dar.

Wahudumu na mitandao ambayo haipo makini mara kadhaa wamesababisha mawakala kuibiwa kwa namna hii kwa sababu huwa wanazuia miamala ya namna hiyo na kumrudishia hela tapeli (wa Mwanza).

Ningependa kupata maelezo kutoka mitandao ya simu namna wanavyoshughulikia hili tatizo la utapeli.

Sababu zingine kama vile transaction boundaries na mgawanyo wa faida kati ya wakala, wakala mkuu, serikali na mtandao husika zimekwishaelezwa na wadau.
 
Back
Top Bottom