Kwanini waislam wa tanzania wanawachukia ndugu zao wakristo?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
377727_398428533544714_732915119_n.jpg


"...And nearest among them in love to the believers will you find those who say, 'We are Christians,' because amongst these are men devoted to learning and men who have renounced the world, and they are not arrogant" (5:82). It's good to see nice people still exist -kash

Ona huo ubao wa Wakristo unawapongeza ndugu zao Waislam kwa kusheherekea sikukuu ya eid kwanini huko Tanzania Waislam jambo dogo wakifanyiwa na Wakristo wanachukuwa majukumu ya kuchoma moto Makanisa? hicho kitu mimi kinaniudhi sana ingawa mimi mwenyewe ni Muislam nawachukia wale vijana wa kiislam wanaye fanya vitendo vya kihuni ndani ya dini ya kiislam.
 
Mkuu huu ndio utamaduni tunahitaji Bongo
Mkuu Mbuzi Mzee muwe kitu kimoja Waislam na Wakristo muangalie Nchi inakwendaje kiuchumi, ulaya wanaendelea mbele kwa kila kitu sisi Wa Afrika tunarudi nyuma siku zote kazi yetu sisi WaAfrika mambo ya Uchawi wizi,rushwa ,Ufisadi,ngono na ulevi je kweli tutaendelea kiuchumi kweli?
 
Last edited by a moderator:
305026_359992107417175_1855092065_n.jpg


West's dual standards: Anti-Islam film allowed, Anti-Roman Catholic ad banned


Pakistani social media users have been criticizing the West for its dual standers in allowing the certain elements to mock Islam and imposing ban on an advert in UK displaying a pregnant nun.
 
252439_358071507609235_663611156_n.jpg

Interesting how the UK public/media endlessly view the hijab as a sign of OPPRESSION...But the moment the Princess is indecently exploited by French paparazzi, the newspapers use PICTURES LIKE THESE: Now all of a sudden, having a headscarf is ELEGANT, INNOCENT, MODEST. the proof in the beauty and wisdom of the hijab...and the double standards / hypocrisy of the media.
 
Nahisi mada inabadilika taratibu! ntarudi baadae, ngoja kwanza nikabidhi lindo

mimi pia, mwanzo tumeoneshwa tuige torelance ya west; baadaye tunaoneshwa jinsi gani kuna double standard huko west, .........???????
 
Mkuu Baba V Mada ipo pale pale ila haiwezi kujibika kirahisi kaka.

Change begins with you and I, tukionesha mfano wengine watajifunza toka kwetu, unapokuwa na wazo zuri usipoliweka wazi wenye mawazo mabaya wataendelea kutamalaki, tunatakiwa TUJITAMBUE
 
Last edited by a moderator:
Change begins with you and I, tukionesha mfano wengine watajifunza toka kwetu, unapokuwa na wazo zuri usipoliweka wazi wenye mawazo mabaya wataendelea kutamalaki, tunatakiwa TUJITAMBUE
bahati mbaya tanzania ya leo wapumbavu wanazidi kuongezeka na bahati mbaya hata tuliokuwa tunahisi ni werevu wanaangukia kwenye upumbavu hali inayopelekea hali ya tanzania na dunia kwa ujumla kuzidi kuwa sio salama.
 
I salute you.
Najua wewe ni Muislam, I wish na hawa waliochoma moto kanisa la Kigoma wangekuwa kama wewe.
377727_398428533544714_732915119_n.jpg


"...And nearest among them in love to the believers will you find those who say, 'We are Christians,' because amongst these are men devoted to learning and men who have renounced the world, and they are not arrogant" (5:82). It's good to see nice people still exist -kash

Ona huo ubao wa Wakristo unawapongeza ndugu zao Waislam kwa kusheherekea sikukuu ya eid kwanini huko Tanzania Waislam jambo dogo wakifanyiwa na Wakristo wanachukuwa majukumu ya kuchoma moto Makanisa? hicho kitu mimi kinaniudhi sana ingawa mimi mwenyewe ni Muislam nawachukia wale vijana wa kiislam wanaye fanya vitendo vya kihuni ndani ya dini ya kiislam.
 
377727_398428533544714_732915119_n.jpg


"...And nearest among them in love to the believers will you find those who say, 'We are Christians,' because amongst these are men devoted to learning and men who have renounced the world, and they are not arrogant" (5:82). It's good to see nice people still exist -kash

Ona huo ubao wa Wakristo unawapongeza ndugu zao Waislam kwa kusheherekea sikukuu ya eid kwanini huko Tanzania Waislam jambo dogo wakifanyiwa na Wakristo wanachukuwa majukumu ya kuchoma moto Makanisa? hicho kitu mimi kinaniudhi sana ingawa mimi mwenyewe ni Muislam nawachukia wale vijana wa kiislam wanaye fanya vitendo vya kihuni ndani ya dini ya kiislam.
Bahati mbaya hukufuatilia tatizo hili tangu mwanzo. Huyu mtoto aliyekojolea huo msahafu waislamu wengi ukiongea nao wanasema ni mtoto katika utashi wake alikua anacheza na mwenzie kwa kigezo cha kwamba hicho kitabu hakina miujiza kama mwenzie alivyokua anamtisha. Ukifuatilia hata mtu wa kwanza kuona hilo tukio alichukua subira kwa kwenda kwa mzazi wa yule mtoto kushitaki. Ila baada kushitaki tatizo ndio lilianza hapo. Yule mzazi alimjibu ndivyo sivyo yule mkubwa aliyekwenda kumstaki yule mtoto kwa yule mzazi. Kuwa " Mimi nilidhani ameua kumbe kakojolea msahafu kwani unauzwa shs. ngapi niwape pesa mkanunue mwingine."

Sasa kwa majibu hayo yule mzazi hakutumia busara wala kutegemea kuwa jambo la imani si la kuchezea namna hiyo mtoto akapelekwa polisi. Na polisi nae asione kuwa jambo hili linahitaji busara za kuwaita wale wazazi washirikiane kumkanya yule kijana. Siku tatu zilipopita ikabidi waislamu husika wajadili na katika kujadili jambo likihusishwa na watu wengi kila mtu ana akili yake ndio hapo vurugu za kwenda polisi zilipoanza na kumbuka unapokua na maandamano kama haya kuna watu wanakua na nia tofauti.

Laiti kama yule mzazi angemkanya kijana wake hata kwa kumtisha nadhani jambo lile lisingefikia hatua ambayo ilifikia.

Bado jambo hili wa kulaumiwa sana ni yule mzazi naamini kama angetumia busara lisingefikia hapo lilipofikia. Mbona Waisalam na wakristo katika nchi hii tunaoleana tunafanya mambo mengi ya kijamii bila kujali tofauti za dini. Hapo pepo alifanya kazi yake kwa kupitia binadamu.

Pole kwa wote walioguswa na jambo hili kwa namna moja au nyingine. Dini zote tunafundishwa kusamehe hivyo hili tulisamehe kama Raisi na viongozi wa dini walivyosema, na tugange yajayo.
 
I salute you.
Najua wewe ni Muislam, I wish na hawa waliochoma moto kanisa la Kigoma wangekuwa kama wewe.
Mkuu Bujibuji hawa waliochoma moto kanisa ni Wahuni Vijana wa Watoto wa kiislam Muislam halisi

hawezi kuchoma moto Kanisa Kwa sababu Eti mtoto Mmoja wa Kikristo kakojolea Quran kwani huko kwetu hakuna Serikali? Serikali

kazi yake ni nini? Serikali inafanya kitu gani kwa hawa wanaoharibu Amani ya nchi yetu?Mambo kama hayo

hayakuwepo wakati wa Enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere iweje yawepo kwa sasa?Serikali haina

uwezo wa kuwathibiti hawa wanaochafua amani ya nchi yetu?Huyo mtoto aliyekojolea Kitabu cha Waislam

angelikamatwa na polisi na kupelekwa kwenye vyomba vya Sheria sio wahuni wachache katka dini ya kiislam

wanataka kuvuruga amani ya nchi yetu Wajichukulie sheria mikononi mwao. Mimi nina laani kitendo cha huyo mtoto kukojolea kitabu cha Waislam Quran na pia nina laani

kitendo cha Wahuni wachache katika Dini ya kiislam kuvuruga amani ya nchi yetu na ninawapongeza ndugu zetu

Wakristo kwa uvumilivu wao wanao onyesha katika kila hali Mungu ndio atakao walipa wema wao.


RAIS JK ATEMBELEA KANISA LILILOSHAMBULIWA NA WAISLAMU MBAGALA




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es salaam na Pwani Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Mawe yametoboa vioo vingi

Ofisi ya Kanisa imechomwa moto


 
Last edited by a moderator:
[h=3]ASKOFU AMUOMBEA RADHI MTOTO ALIYEKOJOLEA QURAN, VIONGOZI WENGINE KUKUTANA LEO[/h]

Archbishop-Dr-Valentino-Mokiwa.jpg
Askofu mkuu Dkt. Valentino Mokiwa wa kanisa Anglican nchini.

<tbody>
</tbody>
Askofu mkuu wa kanisa la Anglican nchini Dkt.Valentino Mokiwa ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Dar es salaam amewaomba radhi waumini wa dini ya kiislamu kumsamehe mtoto Emanuel Josephat (14) aliyekojolea kitabu chao cha Quran pamoja na kuwasamehe wakristo kwa kitendo kilichofanywa na mtoto huyo kwakuwa ametenda hayo katika hali ya utoto pia amewataka waumini wa dini ya kikristo kuishi kwa mshikamano na waumini wa dini ya kiislamu lakini pia wawe na tahadhari kwakuwa wenzao hawana subira linapotokea jambo.

Askofu Mokiwa ameyasema hayo katika ibada maalumu iliyofanyika katika kanisa kuu la St. Albans na kuhudhuriwa na maaskofu wengine wa kanisa hilo ikiwa ni maalumu kwa matukio ya uchomaji moto na uharibifu wa makanisa uliofanywa na waumini wa dini ya kiislamu huko mbagala, ambapo ameitaka serikali kuchukua hatua kali jambo linapotokea ama kupelekewa taarifa kama hizo ili kuokoa mali na maisha ya watu mara moja bila kuchelewa kwakuwa imekuwa ikichelewa kuchukua hatua madhubuti pindi wakristo wanapotokewa na matukio ya aina hiyo na mengine kama ilivyotokea ijumaa iliyopita.

Amesema kama wakristo wanasamehe kwakuwa watu hao hawajui walitendalo, lakini ametoa onyo kwa serikali na waislamu kwamba jambo lililotendeka liwe mwisho na lisijirudie tena na kutojisahau na kudhani kwamba nchi hii ni yao wenyewe kwakuwa ni mali ya waumini wa dini zote na kukumbusha enzi za uongozi wa hayati mwalimu JK Nyerere waumini wa dini zote waliachiwa uhuru wakuabudu watakavyo lakini waislamu wamekuwa wakiwanyanyasa wakristo ni kama nchi hii wameumbiwa peke yao.

Wakati huohuo askofu huyo amesema kanisa hilo litayakarabati makanisa yao yaliyoharibiwa bila kuhitaji msaada na kuzindua namba tatu za simu kutoka makampuni ya Tigo, Vodacom na Airtel ambazo zitatumika kukusanya fedha za kukarabati makanisa hayo(habari hii ni kupitia Yaliyotokea Wapo Radio Fm ikiripotiwa na Amos Kalani.).

Nao viongozi wa baraza la makanisa ya kipentecoste nchini wanatarajia kukutana asubuhi ya leo katika kanisa la Naioth Gospel Assembly kwa askofu David Mwasota ambaye pia ni katibu wa baraza hilo ili kujadili mambo yaliyotokea huko mbagala kikao ambacho kimeitishwa na mwenyekiti wa baraza hilo askofu Bruno Mwakiborwa wa E.A.G.T Mito ya baraka jijini Dar es salaam.
 
Vurugu za Kidini Mbagala: Mtoto akojolea msahafu; makanisa yachomwa




Kanisa baada ya kuchomwa moto




Taarifa na maoni ya watu mbalimbali


Chanzo cha fujo hizo ni mabishano ya watoto wawili wenye imani tofauti mmoja akimwambia mwenzake kwamba eti


ukikojolea msaafu unakua chizi yule dogo mwingine kaukojolea kweli na hajawa chizi, Yule mwenzake alivyoona kashindwa

ikabidi aende msikitini akawatonya waislamu kwamba kuna dogo kakojolea msaafu, Si unajua tena wakatoka waislamu

wenye siasa kali wakataka kumuua dogo polisi wameingilia kati na kumuokoa huyo dogo sasa ni vita ya mabomu ya machozi

ya Polisi na mawe yanayorushwa na waislamu, Hali sio shwari kabisa magari kibao yamevunjwa vioo na fujo bado inaendelea mpaka sasa


Polisi wanapiga mabomu ya machozi kuwatawanya Waislamu waliokwenda kuchoma moto kituo cha polisi na kumtoa mtoto alie kojojea Kuran.

Huyo mtoto ni wa kidato cha kwanza walikua wanabishana na mwezie kwamba ukikojolea Kuraan utakuwa kichaa ndipo

huyo kijana alipokojolea na hakuwa kichaa na mwenzie alivoona hivo akawataarifu watu kuwa mwenzie kakojolea kuraani,

watu wakamkimbiza polisi kumwokoa na ndipo wananchi walipokwenda kituo cha polisi kutaka kutoa kipigo kwa mtoto huyo

na polisi wakaja kumlinda na mabomu yakatumika kutawanya watu.


PakaJimmy ]

Nimesikiliza Redio Cloudz hapa taarifa zinasema hadi sasa makanisa 3 yameshachomwakutokana na vurugu huko Mbagala.

Makanisa hayo ni pamoja na Anglikana, Sabato na Pentekoste yote ya Mbagala.

Taarifa inasema vurugu zinazidi kusambaa maeneo mbali ya jirani


A VILLAGER

Ni kweli waislamu wameharibu mali katika makanisa matatu Mbagala - Kova on ITV
- Vurugu sasa zimehamia Chang'ombe karibu na Uwanja wa Taifa kwenye kiwanja kilichouzwa na Bakwata.
- Polisi wamefika wameona hakuna tatizo Waislamu wamevunja ukuta wameweka jukwaa wanahutubia; polisi wapo jirani wanawafuatilia

Gurudumu
Kova, mkuu wa Mkoa wa DSM, na Shehe mkuu wa mkoa wa DSM wako live ITV kipindi maalum wanaelezea hilo tatizo na mkuu wa mkoa anakemea watu wachache ambao wanavizia matatizo madogo madogo na kuchochea chuki za kijamii

Pumba
Mkuu wa mkoa anawasihi dini zote kutolichukulia jambo hili kwa jazba kwasababu ni jambo lililoanzishwa na watoto katika hali yao ya utani....pia anasema kuna watu watachukulia advantage hii kufanya uharibifu...

Shehe mkuu anasema kila mtu anabeba mzigo wake mwenyewe hivyo si haki kuuhukumu ukristo kwa jambo lililofanywa na mtoto hata kama ni mkristo si wakristo waliomtuma






FFU kila kona


Magari yavunjwa

FFU wakiwadhibiti watu mbalimbali
 
Back
Top Bottom