Kwanini wahindi, wazungu na waarabu hawapati ajali za bodaboda?

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Ukiangalia barabarani ajali zinazotokea au ukienda Wodi za hospital nyingi hapa nchini hutakuta Wahindi, Waarabu au Wazungu wamepata ajali ya Bodaboda (pikipiki) japo wao ni watuamiaji wazuri sana wa usafiri wa aina hii.

Mfano mzuri, jijini Dar wahindi wengi wanatumia zaidi pikipiki kuliko daladala na magari binafsi lakini watu hawa huwakuti wamepata ajali ovyo ovyo tofauti na watanzania ambao kila siku wanakatwa miguu na kufariki. Tatizo ni nini? watanzania hawatumii akili katika kuendesha bodaboda? wanapenda kushindana na kutofuata sheria? Nini mtizamo wako.?

KARIBUNI.
 
acha waje wenyewe,
pia mbona zanzibar sisikii ajali za vespa?
au wapemba na waunguja kukatwa miguu kwa ajali ya pikipiki?
 
Ukiangalia barabarani ajali zinazotokea au ukienda Wodi za hospital nyingi hapa nchini hutakuta Wahindi, Waarabu au Wazungu wamepata ajali ya Bodaboda (pikipiki) japo wao ni watuamiaji wazuri sana wa usafiri wa aina hii.

Mfano mzuri, jijini Dar wahindi wengi wanatumia zaidi pikipiki kuliko daladala na magari binafsi lakini watu hawa huwakuti wamepata ajali ovyo ovyo tofauti na watanzania ambao kila siku wanakatwa miguu na kufariki. Tatizo ni nini? watanzania hawatumii akili katika kuendesha bodaboda? wanapenda kushindana na kutofuata sheria? Nini mtizamo wako.?

KARIBUNI.

kuna tofauti kati ya BODABODA na PIKIPIKI.....ajali nyingi zinahusisha bodaboda[commercial] wazungu wahindi wanaendesha pikipiki[binafsi] na wana discipline.

pikipiki zipo tangu enzi na enzi na ajali zilikuwa za kuhesabu chache sana,lakini bodaboda zimeanza juzijuzi tu ajali kibao kwasababu madereva wake ni machizi na walevi wa bangi/viroba/unga
 
Mtu ananunua boda boda leo anajifunza leo hiyo hiyo anaanza kubeba abiria leo hiyo hiyo ataacha kukatwa miguu?

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Viroba mkuu ndio chanzo, hebu fikiria jamaa linazimua hata viroba 6 then anaingia road huku jua kali hapo unategemea nini?
 
kuna tofauti kati ya BODABODA na PIKIPIKI.....ajali nyingi zinahusisha bodaboda[commercial] wazungu wahindi wanaendesha pikipiki[binafsi] na wana discipline.

pikipiki zipo tangu enzi na enzi na ajali zilikuwa za kuhesabu chache sana,lakini bodaboda zimeanza juzijuzi tu ajali kibao kwasababu madereva wake ni machizi na walevi wa bangi/viroba/unga

mkuu umemaliza. pia na mtu anajifunza leo kesho anataka aende spidi 100 na hata sheria za
barabarani hazijui
 
Ukiangalia barabarani ajali zinazotokea au ukienda Wodi za hospital nyingi hapa nchini hutakuta Wahindi, Waarabu au Wazungu wamepata ajali ya Bodaboda (pikipiki) japo wao ni watuamiaji wazuri sana wa usafiri wa aina hii.

Mfano mzuri, jijini Dar wahindi wengi wanatumia zaidi pikipiki kuliko daladala na magari binafsi lakini watu hawa huwakuti wamepata ajali ovyo ovyo tofauti na watanzania ambao kila siku wanakatwa miguu na kufariki. Tatizo ni nini? watanzania hawatumii akili katika kuendesha bodaboda? wanapenda kushindana na kutofuata sheria? Nini mtizamo wako.?

KARIBUNI.

Hivi hao "Wahindi, Waarabu au Wazungu" uliowataja si Watanzania? katika "uchunguzi wako huru" ulikuwa ukiwauliza Uraia wao?
 
kuna tofauti kati ya BODABODA na PIKIPIKI.....ajali nyingi zinahusisha bodaboda[commercial] wazungu wahindi wanaendesha pikipiki[binafsi] na wana discipline.

pikipiki zipo tangu enzi na enzi na ajali zilikuwa za kuhesabu chache sana,lakini bodaboda zimeanza juzijuzi tu ajali kibao kwasababu madereva wake ni machizi na walevi wa bangi/viroba/unga

Kwa hiyo unasema madereva wa bodaboda wana uhusiano na chadema.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom